Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchakamchaka wa Barca! Mechi tisa, siku 28

BARCA Pict

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha kina Lamine Yamal kitakuwa na ratiba ngumu ya mechi za Ligi Kuu Hispania (LaLiga), Ligi ya Mabingwa Ulaya na Copa Del Rey mashindano ambayo hata wapinzani wake wakubwa, Real Madrid, wanashiriki, lakini wao watakuwa na ratiba nyepesi kiasi fulani.

BARCELONA, HISPANIA: KESHO Jumapili, Barcelona watakuwa uwanjani kuikaribiasha Villarreal katika Uwanja wa Spotify Nou Camp, lakini mtihani mkubwa kwa kikosi hicho ni ule wa mchakamchaka wa siku 28 watakapokuwa na mechi tisa za mashindano mbalimbali ukiwa ni mtihani wa kwanza kwa kikosi hicho baada ya kalenda ya Fifa ya mechi za kiamtaifa kumalizika wiki hii.

Kikosi hicho cha kina Lamine Yamal kitakuwa na ratiba ngumu ya mechi za Ligi Kuu Hispania (LaLiga), Ligi ya Mabingwa Ulaya na Copa Del Rey mashindano ambayo hata wapinzani wake wakubwa, Real Madrid, wanashiriki, lakini wao watakuwa na ratiba nyepesi kiasi fulani.

Baada ya mapumziko ya mwisho ya mechi za timu za taifa, Barcelona itakuwa na mchezo mmoja kila baada ya siku tatu katika kipindi cha mwezi mmoja ujao, na sasa inatarajia kuimarika kwa kikosi kutokana na kurejea kwa wachezaji waliokuwa majeruhi.

Eric Garcia na Christensen wanatarajiwa kurejea katika ushindani wa kawaida, huku Jules Kounde, Dani Olmo na Rodri wakiendelea vizuri katika kupona majeraha yao. Inaonekana Barcelona imefanikiwa kuondokana na kipindi cha kwanza cha misukosuko ya msimu huu, kilichohusisha vipigo dhidi ya PSG katika Uwanja wa Parque de los Príncipes na katika mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid.

BARC 04

Timu hiyo ilirejea katika ushindani kwa kupata ushindi mara mbili muhimu dhidi ya Aston Villa na Atletico Madrid katika  Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa kumalizika haina nafasi ya kupumzika, kwani sasa inakabiliwa na mfululizo wa mechi utakaomlazimu kocha Flick kufanya mabadiliko ya mara kwa mara katika kikosi ili kusimamia vizuri matumizi ya wachezaji.

Kuanzia Novemba 22 hadi Desemba 20, Barcelona itacheza mechi tisa ndani ya siku 28 na katika kipindi hicho, miamba hiyo ya Catalonia itakutana na Villarreal, Sabah, Deportivo, Atletico Madrid, Celta, Manchester City, Malaga, mpinzani ambaye atapangwa dhidi yao katika hatua ya 32 bora ya Copa del Rey, kabla ya kuhitimisha mfululizo huo kwa mchezo wa La Liga dhidi ya Real Sociedad.


BARC 01

RATIBA NGUMU KABLA YA KRISMASI

Mechi mbili zinaonekana kuwa na uzito mkubwa kuliko nyingine katika ratiba hiyo; Barcelona itakutana na Atletico Madrid, Desemba 2. Mchezo huo unachezwa mapema kutokana na ukweli kwamba timu hizo mbili zitakutana tena Februari 2 katika michuano ya Supercopa ya Hispania.

Ushindi ambao Barcelona iliupata katika Uwanja wa Metropolitano umeifanya iongeze pengo la pointi dhidi ya kikosi hicho cha kocha Diego Simeone hadi tano, huku Real Madrid ikiendelea kuwa mpinzani mkuu katika mbio za ubingwa.

Mchezo mwingine mkubwa kwa Barcelona ni dhidi ya Manchester City katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, utakaochezwa Desemba 8, ambapo timu hiyo ya England itakuwa mtihani mgumu kwa Barca, ambayo ina hamu ya kumaliza katika nafasi nane za juu ili kuepuka kucheza hatua ya mchujo kabla ya kufuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora.

BARC 02

Kwa sasa, Barcelona inashika nafasi ya tano katika msimamo wa kundi ikiwa na pointi tisa. Ipo nyuma ya PSG na Real Madrid, ambazo zina pointi 10, pamoja na Arsenal yenye 10 na Como, huku ushindani ukiwa mkubwa katika sehemu ya juu ya msimamo.

Ushindi dhidi ya Man City utakuwa muhimu kwa kikosi cha Flick kuelekea mechi mbili za mwisho za Ligi ya Mabingwa, ambapo kitakutana na wapinzani wagumu, Sporting CP na Como.


BARC 03

KUNA COPA DEL REY

Mfululizo huo wa mechi pia utahusisha Barcelona kuanza kampeni yake ya msimu wa 2026/27 katika michuano ya Copa del Rey.

Timu zote nne zinazoshiriki Supercopa ya Hispania zimepata nafasi ya kuruka hatua za awali na kuanza moja kwa moja katika raundi ya tatu, itakayochezwa kati ya Desemba 15 na 17.

Barcelona iliondolewa katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita na Atletico Madrid. Hata hivyo, michuano ya Copa del Rey imekuwa moja ya mashindano ambayo klabu hiyo huyapa kipaumbele.

Kwa kuzingatia mfumo wa mashindano hayo, Barcelona itakutana na timu inayoshiriki ligi ya daraja la chini. Hali hiyo inaweza kuifanya isafiri kucheza dhidi ya timu inayoshiriki madaraja ya 1A au 2A RFEF, jambo ambalo linaweza kuibua changamoto zisizotarajiwa.

Mapumziko ya Krismasi yatakuwa nafuu kubwa kwa Hansi Flick na kikosi chake, hasa baada ya kukabiliana na ratiba hii ngumu ya michezo itakayohitimisha mwaka 2026.