Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Xavi Simons apigiwa mahesabu Liverpool

TETESI Pict

Muktasari:

  • Xavi ambaye dirisha lililopita pia alikuwa akihitajika na vigogo wa Ulaya kabla ya kuamua kusaini mkataba wa kudumu na Leipzig akitokea PSG, msimu huu amecheza mechi 25 za michuano yote na kufunga mabao nane.

Liverpool imeongeza juhudi katika harakati zao za kuiwania saini ya kiungo wa RB Leipzig raia wa Uholanzi, Xavi Simons, 21,  ambaye anauzwa kwa kiasi kisichopungua Euro 80 milioni.

Xavi ambaye dirisha lililopita pia alikuwa akihitajika na vigogo wa Ulaya kabla ya kuamua kusaini mkataba wa kudumu na Leipzig akitokea PSG, msimu huu amecheza mechi 25 za michuano yote na kufunga mabao nane.

Awali bei ya staa huyu ilitajwa ni Euro 100 milioni lakini Leipzig ipo tayari kumwachia ikiwa itapata Euro 80 milioni.

Kocha Arne Slot amevutiwa na fundi huyu kwa sababu mbali ya kucheza kama kiungo mshambuliaji pia anaweza kutumika kama mshambuliaji wa mbele.

Licha ya kupewa nafasi kubwa ya kumpata, Liverpool itatakiwa kushinda vita dhidi ya timu nyingine ambazo zinahitaji saini yake ikiwemo Bayern Munich na Manchester City. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.



Jarrad Branthwaite

MANCHESTER  United imepanga kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inaipata saini ya beki kisiki wa Everton raia wa England, Jarrad Branthwaite, 22, dirisha lijalo la majira ya kiangazi na mkataba wake utakuwa umebakisha miaka miwili.

Jarrad ambaye ni mmoja kati ya mastaa tegemeo wa Everton, alianza kuwindwa na vigogo mbalimbali barani Ulaya tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.


Marcus Rashford

ASTON Villa inafikiria kutumia kipengele kilichopo katika mkataba wa makubaliano yao na Manchester United juu ya kumchukua kwa mkopo mshambuliaji Marcus Rashford na inaruhusiwa kumsainisha mkataba wa kudumu ikiwa itaridhishwa na kiwango chake.

Kwa mujibu wa ripoti, Villa wanaweza kumsainisha Rashford mkataba huo ikiwa watalipa kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni.


Felix Nmecha

MANCHESTER United ipo katika mchakato wa kutaka kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund raia wa Ujerumani, Felix Nmecha, 24, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza mashetani hao wekundu wanataka kutumia Pauni 40 milioni kama ada yake ya uhamisho. Benchi la ufundi la Man United limevutiwa na staa huyo kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu huu.


Dean Huijsen

NEWCASTLE ipo tayari kulipa Pauni 50 milioni kwenda Bournemouth dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuipata saini ya beki wa timi hiyo na Hispania, Dean Huijsen, 19. Beki huyu ambaye anaichezea timu ya vijana ya taifa ya Hispania, msimu huu ameonyesha kiwango bora na mbali ya Newcastle, vigogo kama Chelsea na Arsenal poa wanahitaji saini yake.


Kepa Arrizabalaga

BOURNEMOUTH imewaweka makipa wawili katika rada zao ambao ni Mhispania kutoka Chelsea, Kepa Arrizabalaga, 30, na kipa wa Liverpool raia wa Ireland, Caoimhin Kelleher, 26, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Benchi la ufundi la Bournemouth limevutiwa sana na kiwango alichoonyesha Kepa tangu ajiunge nao kwa mkopo msimu huu.


Jorrel Hato

REAL Madrid inatarajiwa kuungana na Arsenal, Liverpool na Chelsea katika vita ya kuiwania saini ya beki kisiki wa Ajax raia wa Uholanzi, Jorrel Hato dirisha lijalo.

Hato mwenye umri wa miaka 19, anaonekana kuzivutia timu nyingi kubwa kutokana na ubora wake aliouonyesha kuanzia timu ya taifa na Ajax. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao matatu.


Darwin Nunez

LIVERPOOL inatarajiwa kutumia zaidi ya Pauni 100 milioni kutafuta mshambuliaji mpya dirisha lijalo la majira ya kiangazi na nyota wao wawili tegemeo Darwin Nunez na Mohamed Salah wanatarajiwa kuondoka. Mbali ya Salah ambaye inajulikana mkataba wake utakuwa imefikia ukomo, Nunez anaripotiwa huenda akauzwa kwa sababu kocha haridhishwi na kiwango chake.