Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfanyakazi akamatwa sakata la kuwaibia wachezaji wa Nigeria

NIGERIA Pict

Muktasari:

  • Katika malalamiko yake, Okoronkwo aliishutumu hoteli hiyo kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka baada ya tukio hilo kuripotiwa, akidai uongozi wa hoteli haukuonyesha ushirikiano wa kutosha katika kushughulikia malalamiko ya wachezaji.

BAADA ya wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria, Super Falcons kulalamika kuibiwa fedha zao na wahudumu wa hoteli ya Marriott jijini Casablanca, inaelezwa mfanyakazi mmoja amekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na wizi huo.

Kukamatwa kwa mfanyakazi huyo kumejiri ikiwa siku chache baada ya mshambuliaji wa Nigeria, Esther Okoronkwo kuchapisha taarifa kwenye mitandao ya kijamii akidai kuwa baadhi ya wahudumu wa usafi wa hoteli hiyo waliingia kwenye vyumba vya wachezaji na kuiba fedha walizokuwa wameziacha kwenye pochi zao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mamlaka za Morocco, mtuhumiwa alikamatwa juzi Jumatatu na kuwekwa mahabusu huku akifanyiwa uchunguzi chini ya usimamizi wa ofisi ya mwendesha mashtaka.

Wakati wa operesheni ya kumkamata, polisi walidai kumkuta akiwa na dirham 10,000 za Morocco, fedha ambazo uchunguzi wa awali unaonyesha zinaaminika kuwa sehemu ya fedha zilizoibwa kwa wachezaji wa Nigeria baada ya kubadilishwa kutoka sarafu ya kigeni kwenda sarafu ya nchini hiyo.

Bado hakuna uthibitisho moja kwa moja lakini uchunguzi unaendelea ili kubaini mazingira ya tukio hilo kama kuna watu wengine waliohusika katika wizi huo.

Awali, Okoronkwo, anayekipiga AFC Toronto ya Canada, alidai kupoteza Dola 700 huku akisema jumla ya fedha zilizoibwa kutoka kwa baadhi ya wachezaji zilifikia takribani Dola 1,000.

Miongoni mwa wachezaji aliowataja kuathirika na tukio hilo ni beki Osinachi Ohale, kiungo Joy Omewa, nahodha Rasheedat Ajibade na kiungo Halimatu Ayinde, ambao wote walidai kupoteza kiasi tofauti cha fedha.

Katika malalamiko yake, Okoronkwo aliishutumu hoteli hiyo kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka baada ya tukio hilo kuripotiwa, akidai uongozi wa hoteli haukuonyesha ushirikiano wa kutosha katika kushughulikia malalamiko ya wachezaji.