Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Xabi Alonso apasua jipu Chelsea! Awashukia nyota wake

ALONSO Pict

Muktasari:

  • Chelsea ilikumbana na kipigo hicho katika mchezo ambao mabao yote matatu yalifungwa kipindi cha pili, matokeo yaliyofanya timu hiyo kukosa ushindi katika mechi tatu mfululizo kabla ya mapumziko ya wiki tatu ya mechi za kimataifa yanayotarajiwa kuanza keshokutwa.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Xabi Alonso, amewashukia nyota wake baada ya timu hiyo kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Brentford juzi na kukiri kuwa walipoteza “ushindani” katika kipindi cha pili cha mchezo huo mkali.

Chelsea ilikumbana na kipigo hicho katika mchezo ambao mabao yote matatu yalifungwa kipindi cha pili, matokeo yaliyofanya timu hiyo kukosa ushindi katika mechi tatu mfululizo kabla ya mapumziko ya wiki tatu ya mechi za kimataifa yanayotarajiwa kuanza keshokutwa.

Mbali na kipigo hicho, Chelsea pia ilishindwa kufunga bao kwa mara ya kwanza msimu huu, huku wachezaji wake wakionyesha kiwango cha chini zaidi kwa kipindi chote cha mchezo huo.

Alonso amesema timu yake haikuweza kudumisha kiwango na ari ya ushindani kwa dakika zote 90, jambo lililowapa Brentford nafasi ya kutawala kipindi cha pili.

ALO 01

“Tulipoteza uthabiti na ushindani katika kipindi cha pili,” amesema Alonso.

Kocha huyo amesema Chelsea ilifanya makosa madogo ambayo hatimaye yaliigharimu timu yake, huku akiwapongeza Brentford kwa kutumia vizuri nafasi walizozipata.

“Maelezo madogo yanaweza kuamua mchezo. Hupaswi kumpa mpinzani faida katika michezo ya aina hii, lakini wao walifanya kidogo na wakapata mengi hili siyo jambo ambalo linakubalika kwa sasa kwenye timu hii, hatukuwa vizuri na hilo lazima tuelezana wazi.”

Chelsea pia ilishindwa kumpa kipa wa Brentford, Caoimhin Kelleher, kazi kubwa katika kipindi cha pili, huku safu yake ya ushambuliaji ikionekana kushindwa kupata nafasi za maana za kumsumbua kipa huyo ambaye muda mwingi alionekana kutokuwa na kazi kubwa ya kufanya.

ALO 02

Alonso, hata hivyo, amesema bado ni mapema kutoa hitimisho kuhusu timu yake, akisisitiza kuwa Chelsea ipo katika mchakato wa kujenga timu yenye uwezo wa kudumu katika kiwango cha juu.

“Ni mchakato. Bado ni mechi tano tu katika Ligi Kuu ambayo kila mchezo ni mgumu. Tulijua haitakuwa rahisi na kazi haitakuwa rahisi hata kidogo.”

Haya ni matokeo kama mengine lakini lazima tuendelee kupambana ili kuhakikisha kuwa tunamaliza msimu huu vizuri kabisa.

Chelsea ambayo ilikuwa nafasi ya sita kabla ya mchezo wa jana, imeshinda michezo miwili tu kati ya sita ambayo imecheza hadi sasa msimu huu.

ALO 03

Kwa upande wa Brentford, kocha Keith Andrews alisifu juhudi za wachezaji wake, akisema walionyesha uvumilivu na dhamira kubwa katika kipindi cha pili.

Andrews amesema aliona mapema kuwa wachezaji wake walikuwa tayari kwa mchezo huo, hasa kutokana na namna walivyojiandaa katika siku zilizotangulia.

“Niliona kitu kizuri kikija. Niliweza kuona hilo machoni mwa wachezaji katika siku chache zilizopita.”

Amesema Brentford imekuwa ikikabiliana na wapinzani wanaokuja na mipango ya kuzuia aina yao ya uchezaji, lakini timu yake imekuwa ikitafuta njia za kuvunja mipango hiyo.

“Wapinzani wetu wanajiandaa kwa heshima kubwa kujaribu kuzuia tunachofanya, hivyo jukumu linabaki kwetu kutafuta namna ya kushinda changamoto hiyo.”

Andrews pia alifurahishwa na uhusiano unaozidi kujengwa kati ya timu hiyo na mashabiki wake.

“Kuna uhusiano mzuri kati ya mashabiki, wachezaji na klabu kwa ujumla unaozidi kukua. Kila mtu anafurahia safari hii.”

Kwa ushindi huo, Brentford ilionyesha nguvu katika kipindi cha pili na kuondoka na pointi zote, wakati Chelsea ikibaki na maswali ya kujibu kuhusu kiwango chake na uwezo wa kudumisha ushindani kwa dakika zote 90. Huu ni ushindi wa pili kwa Brentford katika michezo mitano ikiwa haijapoteza mechi yoyote baada ya kutoka sare tatu zilizopita.