Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo tisa ya kuangalia EPL wikiendi

MAMBO Pict

Muktasari:

  • Achana na mchezo huo, leo na kesho kuna mechi bab’kubwa katika michuano hiyo, huku mambo tisa yakitarajiwa kushuhudiwa.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England iliendelea jana kwa mchezo kati ya Brentford na Chelsea waliokuwa wageni, ambapo matokeo unayo msomaji!

Achana na mchezo huo, leo na kesho kuna mechi bab’kubwa katika michuano hiyo, huku mambo tisa yakitarajiwa kushuhudiwa.


MAMB 01

Spurs, Villa mechi ya kukata na shoka

Nini hutokea nguvu inayoweza kuzuilika inapokutana na kitu kinachoweza kusukumwa? Kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur leo, Jumamosi kuna jibu wakati Aston Villa inayoshika nafasi ya 19 itakapowasili Kaskazini mwa London.

Timu zote mbili zimefunga bao moja tu katika ligi. Kurejea kwa Pedro Porro ni jambo kubwa kwa kocha Roberto De Zerbi na hilo linapaswa kumsaidia kumaliza ukame.


MAMB 02

Hurzeler anapokutana na mabingwa

Fabian Harzeler aliposema mafanikio ya Brighton yamejengwa juu ya mpangilio mzuri baada ya kurejea kwa kusisimua dhidi ya Manchester United Old Trafford, Jumatano kwenye Carabao, huenda alikuwa akimzungumzia supastaa wa kikosi hicho Malick Yalcouye.

Mchezaji huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 20 amegeuka kuwa mimba kwelikweli na leo anakutana Arsenal ambayo iko moto uwanjani. Lakini, Arsenal wanapaswa kuwa makini na tishio la Yalcouye na wenzake.


MAMB 03

Mykolenko nguvu mpya ya Moyes

Kuimarika kwa Vitalii Mykolenko mwanzoni mwa msimu kumepita bila kupewa uzito unaostahili, na huenda kutaendelea miongoni mwa wanaomkosoa, lakini wakati ambao kocha wa Everton, David Moyes anahitaji wachezaji wenye uzoefu kuchukua jukumu na kupambana na changamoto ya kuwa na kikosi kidogo, beki huyo wa kushoto wa Everton amefanya hivyo.

Hata hivyo, bado kuna tatizo la kukosekana kwa mchezaji wa kuziba nafasi ya beki wa kushoto baada ya uamuzi wa kumpeleka Adam Aznou kwa mkopo Malaga msimu huu, lakini Mykolenko, ambaye ni beki bora zaidi amepunguza makosa.

Washambuliaji wapya wa Ipswich, Emersonn na Zian Flemming, wataijaribu safu ya ulinzi ya Everton.


MAMB 04

Jaissle na Newcastle United

Kwa kuzingatia kwamba anapenda soka la moja kwa moja, kocha wa Newcastle United, Matthias Jaissle atakuwa na kazi nzito mbele ya wabishi Hully City walioanza na moto na baado wanauendeleza.

Jaissle anatarajia kuendelea kuboresha safu zote katika kikosi baada ya kuondokewa na mastaa wakali kama Bruno Guimaraes, Sandro Tonali na Anthony Gordon walioibeba timu hiyo msimu uliopita. Lakini, mbele ya Hull City wenye njaa ya mabao atafanikiwa?


MAMB 05

Delap kama Wood

Wengi walibeza ada ya Pauni 45 milioni iliyolipwa Chelsea ili kumnunua Liam Delap wakati wa majira ya kiangazi, lakini Nottingham Forest inaonekana kuwa mahali sahihi kwa mshambuliaji huyo kurejesha kiwango chake.

Forest hapo awali ilifanikiwa ikiwa na Chris Wood kama mshambuliaji na Delap ni kama mrithi wake. Katika ushindi wa ugenini dhidi ya Villa Jumamosi iliyopita, Morgan Gibbs-White na Delap walionekana kana kwamba tayari wanaelewana na wote watataka kutumia nafasi dhidi ya Coventry ambayo imeruhusu mabao manane katika mechi mbili zilizopita.


MAMB 06

Iraola anakabiliwa na mtihani

Kocha mpya wa Liverpool, Andoni Iraola anapambana kuiweka katika ramani ya ushindani timu hiyo na kesho atarejea katika klabu yake ya zamani, Bournemouth kwenda kuonyesha kwamba yupo EPL.

Lakini, Bournemouth chini ya mrithi wa Iraola, Marco Rose, watakuwa wapinzani wagumu. Rose alitumia saa kadhaa akiwa na Iraola kabla ya kuanza rasmi kazi yake Juni na wote wawili watakuwa wamejiandaa kwa mechi yenye kasi na nguvu.


MAMB 07

Calvert-Lewin mtu na nusu!

Straika wa Leeds United, Dominic Calvert-Lewin atakuwa katia ubora atakapokutana na Crystal Palace katika Uwanja wa Elland Road, leo Jumamosi.

Mshambuliaji huyo anatumaini kuwa mchezaji wa kwanza wa Leeds kufunga katika mechi sita mfululizo za ligi nyumbani tangu Arthur Hydes alipofanya hivyo 1932.

Makocha mara nyingi, na kwa usahihi, husema wachezaji ni muhimu zaidi kuliko mifumo, lakini kwa Calvert-Lewin, uamuzi wa kocha Daniel Farke kubadili mfumo kuwa 3-5-2 mwishoni mwa Novemba mwaka jana ulionekana kubadilisha kila kitu.

Kabla ya hapo alikuwa akipata wakati mgumu akiwa mshambuliaji pekee wa timu, lakini alipounganishwa na Noah Okafor au Lukas Nmecha, mabao yalianza kumiminika. Hata hivyo haitakuwa rahisi mbele ya Coventry inayojipapatua kupata ushindi wa kwanza.


MAMB 08

Le Bris atavuruga sherehe Etihad?

Pointi zote 12 za Manchester City katika mechi nne za kwanza za Ligi Kuu England zilijumuisha ushindi wa 1-0 dhidi ya Coventry na Manchester United, ushindi wa 2-1 dhidi ya Bournemouth na ushindi wa 4-1 dhidi ya Crystal Palace.

Kuruhusu mabao mawili huku wakifunga nane ni rekodi nzuri kwa Man City na inaonekana kuwa mwanzo mzuri kwa kocha Enzo Maresca. Hata hivyo, kocha wa Sunderland, Regis Le Bris anaweza kutia mchanga kwenye kitumbua cha furaha cha Man City.


MAMB 09

Bobb kufanya yake?

Supastaa wa Fulham, Oscar Bobb aliingia kama mchezaji wa akiba dhidi ya West Ham United na kuipeleka Fulham hatua ya nne ya Carabao Cup kwa kufunga bao la ushindi kwa ustadi mwishoni mwa mchezo katika Uwanja wa London, Jumanne iliyopita usiku.

Bobb tangu alipojiunga na Fulham Januari iliyopita amekuwa mchezaji tegemeo na hapaswi kuangaliwa kama mtu aisye na msaada kesho dhidi ya Man United.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ni hodari katika kupiga chenga na alionekana kuwa tayari kujijengea nafasi Man City kabla ya jeraha kubwa kukatiza maendeleo yake.