Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga Chelsea akaribia kifungo

WINGA Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine, ambaye amekanusha kutumia dawa hizo kwa kukusudia, hajacheza mechi yoyote tangu mwishoni mwa mwaka 2024.

LONDON, ENGLAND: WINGA wa Chelsea, Mykhailo Mudryk, anakabiliwa na uwezekano wa kufungiwa hadi miaka minne baada ya kushtakiwa rasmi na Chama cha Soka cha England  (FA) kuhusu ukiukaji wa kanuni za kupinga matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine, ambaye amekanusha kutumia dawa hizo kwa kukusudia, hajacheza mechi yoyote tangu mwishoni mwa mwaka 2024.

Msemaji wa FA alisema: “Tunaweza kuthibitisha Mykhailo Mudryk ameshtakiwa kwa kosa la ukiukaji wa kanuni za kupinga matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku, kwa mujibu wa Kanuni ya tatu na nne ya Kanuni za FA kuhusu Dawa za Kulevya.”

“Kwa kuwa kesi hii bado inaendelea, hatuwezi kutoa maelezo zaidi kwa sasa.”

 Desemba mwaka jana, Mudryk alitoa taarifa baada ya matokeo ya vipimo vilivyoonyesha ametumia dawa zisizoruhusiwa na aliandika katika ukurasa wake wa  Instagram akisema: “Ninaweza kuthibitisha nimetaarifiwa kuwa sampuli niliyotoa kwa FA imeonyesha kuwepo kwa viashiria vya dawa zilizopigwa marufuku.”

“Hili limekuwa ni jambo la kushangaza sana kwangu kwani sijawahi kutumia dawa zozote haramu kwa makusudi wala kuvunja kanuni yoyote. Nimekuwa nikishirikiana kwa karibu na timu yangu ya wataalamu kuchunguza jinsi hili lilivyoweza kutokea. Najua sijafanya makosa yoyote na bado nina matumaini nitarudi kiwanjani hivi karibuni.”

“Siwezi kusema zaidi kwa sasa kutokana na usiri wa mchakato huu, lakini nitazungumza zaidi pale nitakapokuwa huru kufanya hivyo.”

Kwa mujibu wa tovuti ya The Telegraph, Mudryk amemwajiri wakili kutoka Morgan Sports Law kushughulikia kesi yake. Kampuni hiyo hiyo ya sheria ndiyo iliyomtetea Paul Pogba baada ya yeye pia kupatikana na kosa la matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku.

Pogba, ambaye aliwahi kuichezea Manchester United, alipewa adhabu ya kufungiwa miaka minne, lakini baadaye ikapunguzwa hadi miezi 18 baada ya rufaa na kwa sasa Pogba ni mchezaji huru baada ya kusitisha mkataba wake na Juventus mwishoni mwa 2024.

Mudryk alicheza mechi 20 katika michuano yote akiwa na Chelsea na timu ya taifa msimu uliopita, kabla ya vipimo  kugundua ametumia dawa zilizokatazwa.

 Mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Heidenheim kwenye UEFA Conference League, ambako alifunga bao katika ushindi wa 2-0 kwa Chelsea.

Mchezaji huyo wa zamani wa Shakhtar Donetsk alijiunga na Chelsea  Januari 2023 kwa ada ya awali ya Pauni 62 milioni.

 Tangu wakati huo, amefunga mabao 10 katika mechi 73 alizoichezea timu hiyo. Mara ya mwisho kuingizwa kwenye kikosi cha mechi ilikuwa Desemba 2024, akiwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika dhidi ya Aston Villa katika Ligi Kuu, England.