Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Willian aanika madudu ya Arteta

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Willian, 38, alijiunga na Arsenal Agosti 2020, baada ya kuitumikia Chelsea kwa mafanikio kwa miaka saba. Ujio wake Emirates ulionekana kuwa usajili mkubwa kwa kikosi cha Arteta, lakini mambo yalikwenda tofauti na matarajio.

LONDON, ENGLAND: NYOTA wa zamani wa Arsenal, Willian, amefunguka kuhusu kipindi kigumu alichokipitia kwenye klabu hiyo, akidai aliahidiwa mambo makubwa na kocha Mikel Arteta ambayo baadaye hayakutimia.

Willian, 38, alijiunga na Arsenal Agosti 2020, baada ya kuitumikia Chelsea kwa mafanikio kwa miaka saba. Ujio wake Emirates ulionekana kuwa usajili mkubwa kwa kikosi cha Arteta, lakini mambo yalikwenda tofauti na matarajio.

Baada ya msimu mmoja pekee, Mbrazil huyo aliondoka Arsenal kwa makubaliano ya pande zote, akiwa amefunga bao moja tu katika mechi 37 alizoichezea timu hiyo.

Willian akizungumza kwenye Obi One Podcast akiwa na aliyekuwa mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea, John Obi Mikel alikiri kwamba kuondoka Chelsea na kujiunga na Arsenal lilikuwa kosa kubwa kwake. Willian amesema Chelsea ilitaka kumuongezea mkataba wa miaka miwili, lakini Arsenal ilimpa ofa ya miaka mitatu, jambo lililomfanya aamue kubaki London pamoja na familia yake.

“Arteta aliniambia, tutacheza hivi na nataka uwe mtu muhimu. Nitajenga timu kukuzunguka na nitakupa funguo za klabu,” amesema Willian.

ART 01

 Kauli hiyo, kwa mujibu wa Willian, ilimshawishi kuhamia Arsenal licha ya kuwa bado aliipenda Chelsea.

“Niliposikia hivyo, nilifikiri labda suluhisho bora ni kwenda Arsenal. Nilisaini mkataba wa miaka mitatu, lakini haikuwa vizuri.

“Baada ya miezi mitatu nilitaka kuondoka Willian amesema mambo aliyokutana nayo Arsenal hayakuwa kama alivyoelezwa kabla ya kusaini mkataba, hali iliyomfanya aanze kufikiria kuondoka mapema. Nilichanganyikiwa. Sisemi ni kosa lao, lakini unaposikia mambo mengi kabla hujaenda halafu unapofika mambo si kama ulivyoambiwa, unachanganyikiwa.”

Amesema kufikia Novemba, miezi michache tu baada ya kujiunga na Arsenal, alikuwa tayari amemwambia wakala wake kwamba anataka kuondoka. “Baada ya miezi mitatu nilimwambia wakala wangu nataka kuondoka na nilifanya kosa kubwa kuondoka Chelsea,” amesema.

ART 02

Willian alisisitiza kuwa tatizo halikuwa fedha, licha ya Arsenal kumpa mkataba bora zaidi kifedha katika maisha yake ya soka.

“Ulikuwa mkataba bora zaidi wa maisha yangu, lakini sikuwa na furaha. Ukiwa huna furaha huwezi kufanya vizuri. Fedha haziwezi kununua furaha.”

Mbrazili huyo pia alizungumzia tofauti ya mazingira kati ya Chelsea na Arsenal, akisema aliona pengo kubwa katika kiwango cha ushindani na matarajio ndani ya klabu hizo mbili.

Kiakili ilikuwa tofauti kabisa na Chelsea, huwezi kuzilinganisha.

Kwa mujibu wa Willian, wakati anaondoka Chelsea klabu hiyo ilikuwa ikipambana kwa ajili ya mataji kila msimu, lakini Arsenal ilikuwa katika kipindi cha mabadiliko, huku wachezaji wakiondoka na wengine wakija. Amesema hali hiyo ilimshangaza tangu siku za mwanzo.

ART 03

Willian pia alidai viwango vya uwajibikaji kwa wachezaji vijana havikuwa sawa na alivyovizoea Chelsea. Hakukuwa na mtu aliyekuwa akiwasukuma vijana. Hilo lilikuwa jambo gumu kwangu.


AMKOSOA ARTETA

Licha ya kumpongeza Arteta kwa uwezo wake wa kiufundi, Willian amesema uhusiano wao haukuwa mzuri na kocha huyo alikuwa na mapungufu katika upande wa usimamizi wa watu.

“Sina chochote dhidi yake. Ni kocha mzuri ndani ya uwanja na mawazo yake ni mazuri, lakini alikosa baadhi ya mambo katika namna ya kuisimamia timu,” amesema.

Willian ameongeza kuwa Arteta alihitaji kuboresha zaidi upande wa kibinadamu katika uongozi wake. Sehemu ya ubinadamu ilikuwa inakosekana. Ni muhimu. Lakini ndani ya uwanja ni mzuri. Baada ya msimu wake wa kwanza uliokatisha tamaa Arsenal, ambao uliishuhudia timu hiyo ikimaliza nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu England, Willian aliomba kuondoka na hatimaye akarudi Brazil kujiunga na klabu yake ya utotoni, Corinthians. Akikumbuka kipindi chake Arsenal, Willian amesema kwa mzaha lakini wenye ujumbe mzito, “kila mara huwa natania kwamba waliniuzia ndoto, lakini haikuwa ndoto nzuri.”