Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wembanyama avunja rekodi NBA, mkataba mnono na ndoto ya ubingwa

WEMBANYAMA Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo kijana kutoka Ufaransa ameibuka kuwa moja ya majina makubwa zaidi katika ligi ya NBA huko Marekani, akionyesha uwezo unaowafanya mashabiki na wachambuzi wengi kuamini kuwa kizazi kipya cha mpira wa kikapu tayari kimechukua nafasi.

TEXAS, MAREKANI: KATIKA mpira wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), ni ngumu kuona mchezaji anayevutia macho ya wadau na mashabiki wengi kwa muda mfupi kama ilivyo kwa Victor Wembanyama maarufu Wemby. Unajua kwanini?

Nyota huyo kijana kutoka Ufaransa ameibuka kuwa moja ya majina makubwa zaidi katika ligi ya NBA huko Marekani, akionyesha uwezo unaowafanya mashabiki na wachambuzi wengi kuamini kuwa kizazi kipya cha mpira wa kikapu tayari kimechukua nafasi.

Kwa muda mfupi tangu aingie kwenye NBA, Wembanyama ameonyesha kuwa ana kila sifa ya kuwa mchezaji wa daraja la juu. Urefu wake unambeba, uwezo wa kulinda na kushambulia kwa ufanisi pamoja na utulivu wake uwanjani, vimemfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoangaliwa zaidi.

WEMB 01

Akiwa mchezaji wa San Antonio Spurs, Wembanyama amekuwa mhimili muhimu katika mafanikio ya timu hiyo msimu huu. Spurs imeanza kuonyesha ushindani mkubwa katika ukanda wa Magharibi wa NBA na mchango wa kijana huyo umeonekana wazi katika ushindi na maendeleo ya timu hiyo wakati akisaka ubingwa wake wa kwanza.

Matarajio juu yake yalianza tangu alipochaguliwa kama chaguo la kwanza katika NBA Draft 2023. Tangu wakati huo, amekuwa akionyesha makubwa tofauti kabisa na ilivyotarajiwa na wengi.

Leo hii akiwa bado na umri mdogo, Wembanyama tayari ameanza kuandika historia. Mashabiki wa kikapu duniani wanaendelea kufuatilia safari yake kwa karibu wakiamini kuwa huu ni mwanzo tu wa hadithi kubwa na nzuri ya kuvutia kwa miaka mingi ijayo.

WEMB 02

MWANZO NA REKODI

Katika msimu wa 2025/2026 wa NBA, Wembanyama ameanza kwa kishindo. Ndani ya michezo mitatu ya mwanzo wa msimu, aliweka rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi hiyo kufikisha pointi 100 pamoja na kufanya ‘blocks’ 15 katika michezo mitatu ya mwanzo wa msimu wa kawaida.

Michezo hiyo ilikuwa dhidi ya timu zenye ushindani mkubwa kama Dallas Mavericks, New Orleans Pelicans na Brooklyn Nets. Katika kila mchezo, Wembanyama alionyesha kiwango cha juu.

Katika mchezo mwingine muhimu, aliiongoza Spurs kushinda kwa pointi 121–106 dhidi ya Detroit Pistons baada ya kufunga pointi 38 na kukusanya reboundi 16. Ushindi huo uliimarisha nafasi ya Spurs katika msimamo wa ligi na kuonyesha umuhimu wa mchezaji huyo katika kikosi hicho.

Kiwango hicho cha juu kimeendelea kuwafanya mashabiki na wachambuzi wa michezo kuamini kuwa Wembanyama anaweza kuwa mmoja wa mastaa watakaotawala NBA kwa miaka mingi ijayo.

WEMB 03

TAKWIMU ZA UBORA

Katika msimu wake wa tatu NBA, Wembanyama ameendelea kuonyesha kiwango cha juu kinachowafanya wengi kumchukulia kama mmoja wa wachezaji bora wa kizazi chake. Kwa wastani wa kila mchezo, ana uwezo wa kufunga zaidi ya pointi 23 huku pia akisaidia timu yake kwa kuzuia mipira ya wapinzani.

Kwa mujibu wa takwimu za msimu huu, Wembanyama amekuwa akifunga wastani wa pointi 23.7 katika kila mchezo anaocheza. Hii inaonyesha uwezo wake mkubwa wa kushambulia na kuisaidia timu yake kupata ushindi katika michezo yenye ushindani mkali.

Mbali na kufunga pia amekuwa akikusanya wastani wa ‘rebound’ 11.2 kwa kila mchezo. Uwezo huu unampa nafasi ya kuisaidia timu yake kudhibiti mpira na kuanzisha mashambulizi mapya.

Pia katika upande wa kulinda, Wembanyama anafanya wastani wa ‘blocks’ tatu kwa kila mchezo. Takwimu hizi zinaonyesha wazi kuwa yeye ni mchezaji anayechangia kwa kiwango kikubwa katika mashambulizi na kulinda timu yake kwa wakati mmoja.

WEMB 04

MAUMBILE NA UWEZO

Moja ya mambo yanayomfanya Wembanyama kuwa mchezaji wa aina yake ni maumbile yake ya kipekee. Ana urefu wa futi saba na inchi nne, jambo linalomfanya kuwa mmoja wa wachezaji warefu zaidi katika NBA kwa sasa.

Kwa urefu huo, anashindana na wachezaji wachache tu katika ligi kama Zach Edey wa Memphis Grizzlies ambaye pia anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji warefu zaidi katika mchezo huo.

Zaidi ya hapo, Wembanyama ana urefu wa mikono unaofikia futi nane, jambo linalompa uwezo mkubwa wa kuzuia mipira ya wapinzani na kulinda eneo la kikapu.

Urefu huo wa mikono unamfanya kuwa tishio kubwa kwa wachezaji wanaojaribu kufunga karibu na kikapu. Kwa kulinganisha, mlinzi maarufu Rudy Gobert wa Minnesota Timberwolves ana urefu wa mikono wa futi saba na inchi tisa.

WEMB 05

MAFANIKIO NJE YA UWANJA

Mbali na mafanikio yake ndani ya uwanja wa mpira wa kikapu, Wembanyama pia ameanza kujijengea umaarufu mkubwa nje ya uwanja. Kampuni nyingi kubwa duniani zimeanza kumtazama kama sura mpya ya matangazo katika michezo.

Moja ya mikataba mikubwa aliyosaini ni ule wa ushirikiano na kampuni ya mavazi ya michezo Nike ambao unatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh257 bilioni.   Pia amekuwa balozi wa chapa ya kifahari Louis Vuitton.