Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Knueppel balaa jipya NBA, Curry aukubali mziki wake

NBA Pict

Muktasari:

  • Rookie katika ligi ya NBA, kama hukuwahi kufahamu, ni mchezaji ambaye anacheza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha msimu mmoja wa kawaida (regular season) wa NBA, na wala siyo wakati wote.

INDIANAPOLIS, MAREKANI: NDANI ya msimu wake wa kwanza tu katika NBA, chipukizi Kon Knueppel wa Charlotte ameendelea kufanya makubwa baada ya kuvunja rekodi ya idadi kubwa ya mitupo ya pointi tatu (3-pointers) iliyowekwa na ‘rookie’.

Rookie katika ligi ya NBA, kama hukuwahi kufahamu, ni mchezaji ambaye anacheza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha msimu mmoja wa kawaida (regular season) wa NBA, na wala siyo wakati wote.

Mchezaji huyo wa pembeni wa Charlotte Hornets ametupia mtupio wake wa 207 wa pointi tatu wikiendi hii dhidi ya Indiana Pacers, akivunja rekodi iliyowekwa na Keegan Murray katika msimu wa 2022–23. Murray alihitaji michezo 80 kuweka rekodi hiyo, lakini Knueppel ameivunja ndani ya michezo 59 pekee.

NB 01

Katika mchezo huo, Knueppel alitupia mitupo mitano ya pointi tatu katika kipindi cha kwanza kabla ya kuvunja rasmi rekodi hiyo katika robo ya tatu. Kabla ya wikiendi alikuwa na usahihi wa asilimia 43.6 wa kutupia kutoka umbali wa pointi tatu na kuongoza orodha hiyo. Rekodi ya jumla ya NBA ya pointi tatu nyingi zaidi katika msimu mmoja bado inashikiliwa na mwamba Stephen Curry wa Golden State Warriors, aliyefunga mitupo 402 katika msimu mmoja.

NB 02

TUZO YA ROOKIE WA MWAKA

Knueppel sasa anatajwa kuwa mmoja wa wagombea wakuu wa tuzo ya Kia NBA Rookie of the Year, akishindana vikali na mshikaji wake ambaye alisoma naye chuo, Cooper Flagg, chaguo namba moja wa Dallas Mavericks. Wote wawili waliwahi kucheza katika Chuo Kikuu cha Duke, ambako walijijengea sifa kabla ya kuingia NBA.

Mbali na mafanikio yake binafsi, Knueppel ameisaidia Hornets kuingia kwenye ushindani wa mchujo (playoffs), jambo ambalo halijafikiwa na klabu hiyo tangu msimu wa 2015–16. Akiwa amebakisha michezo 22 kumaliza msimu wa kawaida, matumaini ya mashabiki wa Charlotte yamefufuka upya.

Kocha wa Hornets, Charles Lee, alimpigia saluti mchezaji huyo kwa kusema; “Ni aina ya mchezaji anayebadilisha utamaduni wa timu. Ni bora lakini hana majivuno. Hilo linawaambukiza wachezaji wengine.”

NB 03

UBORA WA KUTISHA

Knueppel amekuwa sehemu muhimu katika mfumo wa kocha Lee, akicheza sambamba na LaMelo Ball. Anatajwa kuwa na matumizi makubwa ya akili ya kikapu (basketball IQ) kujipatia nafasi rahisi za kufunga, ujuzi ambao mwenyewe katika moja ya mahojiano yake anasema aliujenga tangu utotoni alipokuwa akicheza ligi ya baba yake huko Milwaukee dhidi ya wapinzani warefu zaidi.

Kwa mujibu wa takwimu, asilimia 93 ya mitupo yake ya pointi tatu msimu huu zimetokana na pasi za wenzake, jambo linaloonyesha ustadi wake wa kukamata pasi na kumaliza mchezo, yaani “catch-and-shoot”, na ushirikiano mzuri ndani ya timu.

Kwa kulinganisha, Curry alifunga mipira 166 ya pointi tatu katika majaribio 380 akiwa rookie mwaka 2009–10, ndani ya michezo 80. Knueppel, kabla ya mchezo wa wikiendi hii, alikuwa tayari amejaribu mitupo 461, idadi inayoonyesha ujasiri na nafasi kubwa aliyopewa ndani ya kikosi.

NB 04

Curry mwenyewe alikiri kuvutiwa na uwezo wa chipukizi huyo kwa kusema: “Anaweza kupiga kwa kiwango cha juu sana. Huwezi kumwacha wazi hata kidogo kwa sababu anaachia mpira haraka na kwa kujiamini. Pia uwezo wake wa kutengeneza nafasi ni wa juu kuliko wengi wanavyodhani. Mchezo wake unaendana na mtindo wa NBA wa kasi au hata mchezo wa taratibu.”

Knueppel pia alimzidi Donovan Mitchell katika orodha ya rookies wenye mitupo mingi zaidi ya pointi tatu, baada ya kumpita katika mchezo dhidi ya Cleveland mwezi Februari.


KAZI IPO

Kwa kasi hii, Knueppel si kwamba anaweka tu rekodi, bali pia anaashiria mabadiliko mapya ndani ya Hornets, timu ambayo imekuwa ikipambana kwa muda mrefu kurejea katika hadhi ya ushindani.

Ushindani kati yake na Flagg kwa tuzo ya Rookie of the Year unatarajiwa kuwa moja ya vitu vya kutazamwa msimu huu.