Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LeBron James avunja rekodi ya Kareem  NBA

LEBRON Pict

Muktasari:

  • LeBron, akiwa katika msimu wa 23 akiwa na umri wa miaka 41, aliweka historia hiyo katika robo ya kwanza dhidi ya Denver Nuggets, Colorado ambapo mtupo wake ‘turnaround jumper’ ulimfanya kufikisha mipira 15,838 kiujumla katika maisha yake iliyotumbukia kwenye kikapu.

COLORADO, MAREKANI: SUPASTAA wa Los Angeles Lakers, LeBron James, ameandika rekodi mpya leo, Ijumaa, katika Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), baada ya kuivunja ile iliyowekwa mrefu na Kareem Abdul‑Jabbar kwa kuwa na idadi kubwa ya mipira yote iliyofungwa (field goals) katika historia ya ligi hiyo maarufu duniani.

LeBron, akiwa katika msimu wa 23 ndani ya umri wa miaka 41, ameweka historia hiyo katika robo ya kwanza dhidi ya Denver Nuggets mjini Colorado ambapo mtupo wake ‘turnaround jumper’ ulimfanya kufikisha mipira 15,838 kwan ujumla katika maisha yake iliyotumbukia kwenye kikapu.

Kareem Abdul‑Jabbar, ambaye aliweka rekodi hiyo miaka mingi iliyopita, aliondoka NBA akiwa na 15,837  baada ya miaka 20. Rekodi hii ilidumu kwa zaidi ya miaka 37 kabla ya LeBron kuiivunja usiku wa kuamkia leo.

Katika mchezo huo, Lakers ilikiona chamoto mbele ya Nuggets kwa kupoteza kwa pointi 120–113, licha ya LeBron kuvunja rekodi hiyo.

LeBron pia alikumbana na jeraha dogo la kiwiko wakati wa mchezo huu, lakini alirudi baadaye akaendelea na kukamilisha mchezo huo.

Kwa upande wake, kocha wa Lakers, J.J. Redick, amempogeza LeBron kwa jinsi anavyoendelea kuwa na mchango mkubwa katika kikosi licha ya umri kumtupa mkono, hivyo anaweza kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa NBA.

Wachezaji wengine kama Nikola Jokic na Jamal Murray kutoka Nuggets pia wameonyesha kiwango bora katika mchezo huo, licha ya uzito wa tukio la LeBron.