Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chaka jipya la mastaa Bongo kupigia soga

CHAKA Pict

Muktasari:

  • Hilo linaonekana kupitia vipindi vya A-List na The Royal Circle, vinavyoingia kwenye eneo la maudhui yanayowapa mastaa nafasi ya kuzungumza kuhusu maisha yao, kazi, mahusiano na mambo yanayowazunguka.

ZAMANI staa alihitaji filamu, muziki au kipindi cha televisheni ili awe karibu na mashabiki lakini sasa mambo yamebadilika. Mastaa wameanza kutengeneza majukwaa yao wenyewe na kuamua wao ni simulizi gani ziwafikie mashabiki.

Hilo linaonekana kupitia vipindi vya A-List na The Royal Circle, vinavyoingia kwenye eneo la maudhui yanayowapa mastaa nafasi ya kuzungumza kuhusu maisha yao, kazi, mahusiano na mambo yanayowazunguka.

Kwa upande wa A-List, kipindi kinawakutanisha waigizaji Kajala Masanja, Irene Uwoya, Aunty Ezekiel na Jacqueline Wolper, ambao tayari wana historia kubwa kwenye tasnia ya burudani.


CHAK 01

A-LIST WAFUNGUA MILANGO

A-List ilianza kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kupanuka na kuingia kwenye televisheni. Maudhui yake yanagusa maisha ya mastaa hao, urafiki, mahusiano na mambo ambayo yamewahi kuwa gumzo kwa umma.

Hapa ndipo tofauti yake inapopatikana. Badala ya mastaa hao kusubiri waandishi au watangazaji kuwauliza maswali kuhusu maisha yao, wanapata nafasi ya kusimulia wenyewe.

Kwa maana nyingine, wanamiliki sehemu ya simulizi yao.

Hapo ndipo A-List inapopata mvuto wake, kwa sababu mashabiki hawawaoni tu kama mastaa wanaowaangalia kwenye filamu, bali wanapata nafasi ya kuwafahamu zaidi kama watu wenye maisha, urafiki, changamoto na uzoefu wao.


CHAK 05

THE ROYAL CIRCLE

Kwa upande wa The Royal Circle, nayo imeingia kwenye uwanja huu wa mastaa kujenga majukwaa yao. Kipindi hiki kinawakutanisha Zailisa, Mulki, Dorry na Lissa huku kikifungua nafasi ya kuzungumzia maisha, mahusiano, kazi na mambo mbalimbali yanayowahusu.

K inachovutia ni namna wahusika wanavyokaa pamoja na kushirikishana mawazo na uzoefu wao, jambo linalompa mtazamaji nafasi ya kuwaona kwa upande mwingine tofauti na ule wanaouzoea kwenye mitandao au kwenye kazi zao za burudani.

Kwa mtazamo mpana, The Royal Circle inaingia kwenye wimbi la vipindi ambavyo mastaa wenyewe wanakuwa sehemu kubwa ya simulizi, wakitumia umaarufu wao kuvuta watazamaji na kujenga maudhui yanayowazungu.


CHAK 04

KWA NINI SASA?

Jibu kubwa linapatikana kwenye mabadiliko ya matumizi ya maudhui. Mitandao ya kijamii imefanya msanii aweze kuwasiliana na mashabiki moja kwa moja bila kutegemea televisheni.

Kwa hiyo, kuwa na kipindi chako maana yake ni kuwa na nafasi ya kujenga wasifu, kusimamia simulizi yako na kutumia umaarufu wako kutengeneza maudhui. A-List ni mfano wa safari hiyo, kwani ilianza kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kuingia kwenye televisheni.


CHAK 03

UMAARUFU UNAGEUKA BIASHARA

Hapa kuna jambo kubwa zaidi. Mastaa hawauzi tena kipaji pekee, wanauza pia brand zao. Mtu mwenye mashabiki wengi anaweza kutumia hadhira hiyo kwenye vipindi, matangazo, ubalozi wa bidhaa na miradi mingine ya kibiashara.

Kwa hiyo, A-List na The Royal Circle zinaweza kuonekana kama sehemu ya mabadiliko ambapo msanii anakuwa kwa wakati mmoja, mtayarishaji wa maudhui na brand.


CHAK 02

LAKINI KUNA WAJIBU

Kadiri mastaa wanavyofungua maisha yao kwa umma, ndivyo wajibu wa kuzingatia maadili unavyoongezeka. Hili limeonekana kwenye A-List baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kuwaita Kajala, Irene Uwoya, Aunty Ezekiel na Jacqueline Wolper na kuzungumza nao kuhusu weledi na maudhui ya kipindi.

Hii inaonyesha kuwa uhuru wa kutengeneza maudhui unaambatana na uwajibikaji, hasa kwa mastaa wenye ushawishi mkubwa kwa jamii. Kwa hiyo, A-List na The Royal Circle ni sehemu ya mabadiliko ya tasnia ya burudani.

Mastaa sasa hawataki kuwa wahusika wa simulizi zao pekee, wanataka pia kuwa wasimuliaji na watengeneza majukwaa yao. Swali kubwa sasa si kuanzisha kipindi. Swali ni nani ataweza kukifanya kiwe brand inayodumu, yenye watazamaji na thamani ndani ya tasnia.