Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji wa Chelsea hawatoboi Arsenal

Muktasari:

  • Kwa miaka kadhaa, kumekuwa na mtiririko mkubwa wa wachezaji kati ya klabu hizo mbili, huku wengi wakitoka Stamford Bridge na kuelekea Emirates.

LONDON, England: ARSENAL imetumia karibu pauni milioni 200 kusajili wachezaji msimu huu, lakini safari hii hakuna hata mmoja aliyenunuliwa kutoka Chelsea.

Kwa miaka kadhaa, kumekuwa na mtiririko mkubwa wa wachezaji kati ya klabu hizo mbili, huku wengi wakitoka Stamford Bridge na kuelekea Emirates.

Msimu huu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2022 kwa Arsenal kutomsajili mchezaji kutoka Chelsea.

Hapa tunawapitia wachezaji ambao Arsenal imewasajili kutoka Chelsea katika kipindi cha muongo mmoja uliopita na kuangalia kama walikuwa ni mali safi au mizigo.


RAHEEM STERLING

Mkopo, 2024 — MZIGO

Chelsea ilimsajili Sterling kutoka Manchester City kwa pauni47.5 milioni mwaka 2022, lakini baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa, alipelekwa Arsenal kwa mkopo wa msimu mmoja.

Ulikuwa usajili uliogeuka kuwa janga.

Sterling alicheza mechi 17 pekee za Ligi Kuu England, huku akianza saba tu. Kwa jumla alicheza mechi 28 katika mashindano yote na kufunga bao moja pekee.

Kwa sehemu kubwa ya msimu alionekana kutokuwa katika kiwango cha ushindani.

Arsenal ililipa nusu ya mshahara wake wa pauni 325,000 kwa wiki, lakini fedha hizo hazikuonekana kuwa na thamani yake.


KEPA ARRIZABALAGA

Pauni milioni 5, 2025 — MZIGO

Baada ya kucheza mechi 163 akiwa Chelsea na kushinda mataji manne makubwa, Kepa alihamia Arsenal ili kumpa ushindani Mhispania mwenzake David Raya.

Lakini uamuzi wa Mikel Arteta kumchezesha Kepa katika fainali ya Carabao Cup, baada ya kupewa nafasi katika hatua za awali za michuano hiyo, ulimgharimu.

Kepa alishindwa kuzuia krosi ya Rayan Cherki, akaupeleka mpira moja kwa moja kwenye njia ya Nico O’Reilly, ambaye alifunga na Manchester City kushinda 2-0.

Arsenal sasa imemsajili Illan Meslier kwa uhamisho wa bure kutoka Leeds.


NONI MADUEKE

Pauni milioni 48.5, 2025 — BADO HAKUNA UAMUZI

Madueke alikaa Chelsea kwa miaka miwili baada ya kusajiliwa kutoka PSV Eindhoven kwa pauni29 milioni mwaka 2023, lakini hakuwahi kufanikiwa kujihakikishia nafasi ya kudumu.

Uhamisho wake kwenda Arsenal haukupokelewa vizuri na baadhi ya mashabiki, ambao hata waliandaa ombi la kutaka klabu imrudishe London Magharibi kupitia kampeni ya #NOTOMADUEKE.

Msimu uliopita alianza mechi 27 kwa Arsenal, 16 kati yake zikiwa za Ligi Kuu, na alifunga mabao manane.

Kwa hiyo, si sahihi kusema usajili huo umefanikiwa, lakini pia bado ni mapema kumhukumu.

Msimu huu atapata nafasi zaidi upande wa kushoto kutokana na kuondoka kwa Gabriel Martinelli na Leandro Trossard.


KAI HAVERTZ

Pauni milioni 65, 2023 — MALI SAFI

Havertz alifanya vizuri chini ya kocha Thomas Tuchel akiwa Chelsea na akaandika historia ya klabu hiyo alipofunga bao la ushindi katika fainali ya Ligi ya Mabingwa 2021 dhidi ya Manchester City.

Lakini baada ya Graham Potter kuchukua nafasi Stamford Bridge, Havertz alijikuta akipambana na mfumo ambao haukumfaa.

Chini ya Arteta, amerejesha kiwango na uthabiti wake kila alipokuwa fiti kucheza. Tatizo kubwa limekuwa ni upatikanaji wake.

Ndiyo sababu msimu uliopita Viktor Gyokeres mara nyingi alipendelewa kuanza badala yake.

Hata hivyo, Havertz alimaliza msimu akiwa katika kikosi cha kwanza na ameanza mechi zote mbili za msimu huu.

Arsenal ni timu bora zaidi Havertz anapoanza.


DAVID LUIZ

Pauni milioni 8, 2019 — MZIGO

Luiz alikuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2016/17, lakini baada ya miaka mitatu Stamford Bridge alihamia Arsenal kucheza chini ya Unai Emery.

Alikaa Arsenal kwa takribani miaka miwili, akianza mechi 49 za Ligi Kuu na kutwaa Kombe la FA chini ya Arteta.

Luiz alicheza kwa kiwango bora katika fainali ya Kombe la FA 2020 dhidi ya klabu yake ya zamani, Chelsea.

Hata hivyo, alikuwa mchezaji ambaye kiwango chake kilibadilika badilika sana. Pia alipata kadi nyekundu kadhaa na hatimaye akaondoka Arsenal kwa uhamisho wa bure.

Mashabiki wa Arsenal hawakujuta kumuona akiondoka.


JORGINHO

Pauni milioni 12, 2023 — MALI KIDOGO

Jorginho alijiunga na Arsenal katika dirisha la Januari baada ya kuitumikia Chelsea kwa miaka minne na nusu.

Alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha Tuchel kilichotwaa Ligi ya Mabingwa na UEFA Super Cup mwaka 2021.

Aliongeza uzoefu na ubora katika eneo la kiungo Arsenal. Siku alipokuwa katika kiwango chake bora, Jorginho alikuwa mchezaji wa kiwango cha juu, huku pia akiwa kiongozi mzuri nje ya uwanja.

Hata hivyo, alitumia muda mwingi akiwa kwenye benchi la Arsenal.

Kwa ujumla, usajili wake ulikuwa wa kiwango cha 7/10.

Aliondoka Arsenal kwa uhamisho wa bure Juni 2025.


WILLIAN

Uhamisho wa bure, 2020 — MZIGO

Willian alifurahia miaka saba bora akiwa Chelsea, ambako hadi leo anaendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wanaopendwa na mashabiki.

Lakini akiwa Arsenal, usajili wake ulikuwa wa kukatisha tamaa.

Alifunga bao moja pekee katika mechi 37 na baadaye akaamua kuvunja mkataba wake, ambao ulikuwa bado una miaka miwili, ili kurejea Brazil kujiunga na Corinthians.

Willian mwenyewe aliwahi kukiri “Kwa bahati mbaya, kipindi changu Arsenal hakikuwa kizuri. Sikufurahia kuwa klabuni.”