Wabaya wa Man City, Liverpool hawa hapa
Muktasari:
- Mabingwa mara 10 wa mashindano hayo Liverpool imefuzu kwa robo fainali hiyo kwa njia ya mikwaju ya penalti kwa kuitoa Chelsea, itaikaribisha Bournemouth kwenye Uwanja wa Anfield.
LONDON, ENGLAND: MABINGWA watetezi Manchester City watakuwa mwenyeji wa Bradford City ya Ligi Daraja la Kwanza England (League One), huku Liverpool ikiikaribisha Bournemouth katika robo fainali ya Kombe la Ligi England (Carabao Cup).
City wataikaribisha Bradford City kwenye Uwanja wa Etihad. City ilihitaji mikwaju ya penalti kuiondoa Brighton katika hatua ya 16 bora na kufuzu robo fainali.
Mabingwa mara 10 wa mashindano hayo Liverpool imefuzu kwa robo fainali hiyo kwa njia ya mikwaju ya penalti kwa kuitoa Chelsea, itaikaribisha Bournemouth kwenye Uwanja wa Anfield.
Hii ni mechi itakayomkutanisha kocha wa Liverpool dhidi boss wake wa zamani Bournemouth. Nayo Crystal Palace ikiikabili Sunderland kwenye Uwanja wa Selhurst Park.
Wababe wa Arsenal timu ya Fleetwood Town ya Ligi Daraja la Pili England (League Two) itakutana na Everton au Newcastle United katika robo fainali ya Carabao Cup, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Highbury.
Fleetwood, ambayo ndiyo timu inayoshiriki ligi ya chini zaidi kati ya zilizobaki kwenye mashindano hayo, imeandika historia kwa kutinga robo fainali baada ya kuitoa mabingwa wa Ligi Kuu England, Arsenal, kwa mikwaju ya penalti Jumanne iliyopita.
Mechi za robo fainali zinatarajiwa kuchezwa katika wiki inayoanza Desemba 14.
RATIBA
Manchester City v Bradford City
Crystal Palace v Sunderland
Liverpool v Bournemouth
Fleetwood Town v Everton au Newcastle United