Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu bado wanaitaka Man United

MATAJIRI Pict

Muktasari:

  • Mfanyabiashara huyo kutoka Qatar alishindana na Sir Jim Ratcliffe katika mchakato wa kuinunua timu hiyo mwaka 2023 lakini alishindwa na  Ratcliffe, mwenye umri wa miaka 72, alishinda na kununua asilimia 25 ya hisa kutoka kwa familia ya Glazer kwa thamani ya Pauni 1.3 bilioni.

MANCHESTER, ENGLAND: INAELEZWA tajiri kutoka Qatar, Sheikh Jassim bado hajakata tamaa ya kuimiliki Manchester United  licha ya kufeli 2023.

Mfanyabiashara huyo kutoka Qatar alishindana na Sir Jim Ratcliffe katika mchakato wa kuinunua timu hiyo mwaka 2023 lakini alishindwa na  Ratcliffe, mwenye umri wa miaka 72, alishinda na kununua asilimia 25 ya hisa kutoka kwa familia ya Glazer kwa thamani ya Pauni 1.3 bilioni.

Hata hivyo, kipindi chake cha miezi 18 hadi sasa kimekuwa na changamoto kubwa, huku timu hiyo ikizidi kuanguka kutoka kwa matokeo ya kiwanjani.

Licha ya kuondoka kwa Erik ten Hag na mikoba yake kuchukuliwa na Ruben Amorim bado hakuna jambo jipya lilioonekana zaidi ya kuendelea kuzama na msimu uliomalizika walimaliza nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa ni nafasi mbaya zaidi katika historia yao.

Mbali ya matatizo ya ndani ya uwanja huko nje ya uwanja, matatizo ya kifedha yameendelea kuisumbua timu hiyo ambapo hadi sasa Ratcliffe anadaiwa kupunguza wafanyakazi 450 ili kubana bajeti ya uendeshaji.

Vilevile timu hiyo hadi sasa ina deni la Pauni 1 bilioni.

Sheikh Jassim kwa upande wake, alitaka kuinunua klabu hiyo kwa asilimia 100 na aliahidi kulipa deni lote kama sehemu ya mpango wa kuimarisha timu.

Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph, Sheikh Jassim na washirika wake bado hawajakata tamaa ya kuinunua Man United siku moja, ingawa hana uhusiano wowote wa moja kwa moja na viongozi wa timu hiyo kwa sasa.

Inaelezwa pia wanapanga kumtumia rais wa  Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi, ambaye ana uzoefu mkubwa katika soka la Ulaya  ili kufanikisha suala hilo.

Al-Khelaifi, mwenye umri wa miaka 51 anaimiliki PSG tangu 2011, anafanya kazi chini ya Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Qatar ambao ndio unataka kuinunua Manchester United.

Tetesi kuwa huenda Waarabu hao wakamtumia Nasser kuipata Man United zilishika hatamu mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya  kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kuonekana akiwa mgeni maalumu wa Al-Khelaifi jijini Munich siku chache kabla ya mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa.

 Ferguson mwenye umri wa miaka 83, alihudhuria hafla ya chakula cha jioni kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa mgeni wa Al-Khelaifi na pia alikuwepo katika viti vya heshima kwenye Uwanja wa Allianz Arena wakati PSG ilipoichapa Inter Milan na kutwaa taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa.

Katika mkataba wa mwaka 2023, familia ya Glazer bado inaweza kuuza hisa zake Manchester United bila kumshirikisha mmiliki mwenza, Ratcliffe.