Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Etihad wajitosa kwa William Saliba

Fununu Pict

Muktasari:

  • Saliba ambaye amekuwa akihusishwa na Real Madrid kwa muda mrefu, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027 na mara kadhaa amenukuliwa akisema hana mpango wa kuondoka.

MANCHESTER City itajaribu kutuma ofa kwenda Arsenal katika dirisha lijalo ili kuipata saini ya beki kisiki wa Washika Mitutu hao na timu ya taifa ya Ufaransa, William Saliba, 24.

Saliba ambaye amekuwa akihusishwa na Real Madrid kwa muda mrefu, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027 na mara kadhaa amenukuliwa akisema hana mpango wa kuondoka.

Licha ya msimamo wake, timu hizo mbili zimepanga kumuwekea mezani ofa nono ambayo zinaamini itakuwa ngumu kuikataa.

Benchi la ufundi la Man City limependekeza jina la staa huyo kwa sababu ya mipango ya kutaka kufanya maboresho ya kikosi msimu ujao baada ya kufanya vibaya katika msimu huu hadi kufikia sasa.

Real Madrid imewahi kutuma hadi wawakilishi wake kwenda London kwa ajili ya kumtazama beki huyo kisiki akiwa anacheza.


Milos Kerkez

BOURNEMOUTH imeweka wazi kuwa inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 45 milioni katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa timu yoyote itakayotaka huduma ya beki wake wa pembeni na timu ya taifa ya Hungary, Milos Kerkez, 21, ambaye anahitajika sana ndani ya Liverpool. Kerkez amewavutia vigogo wengi kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu msimu uliopita.



Tijjani Reinders

MANCHESTER City imefanya mawasiliano na AC Milan kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo na Uholanzi, Tijjani Reijnders, 26, katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya la usajili wwa majira ya kiangazi. AC Milan ipo tayari kumuuza mchezaji huyo, lakini kwa kiasi cha pesa ambacho hakitapungua Pauni 70 milioni. Mchezaji huyo amezivutia timu kibao Ulaya zinazomtaka dirisha lijalo.


Cristiano Ronaldo

LICHA ya tetesi kudai kwamba, Cristiano Ronaldo anaweza kurudi tena Italia na kuichezea Inter Milan katika michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu, mabosi wa timu hiyo wamesisitiza kwamba hawana mpango huo wa kumsajili staa huyo wa Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno, mwenye umri wa miaka 40. Mkataba wa Ronaldo unamalizika mwisho wa msimu huu.


Hugo Ekitike

ARSENAL imepanga kutuma ofa nono Eintracht Frankfurt katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kuipata saini ya straika wa timu hiyo na timu  ya taifa ya Ufaransa, Hugo Ekitike, 22. Hiyo ni ikiwa itafeli kumsajili straika wa Newcastle na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak, 25, ambaye anawindwa na timu nyingi kubwa Ulaya kutokana na kiwango chake.


Pedro Gonzalez

BARCELONA imesisitiza kuwa kiungo wake raia wa Hispania, Pedro Gonzalez hauzwi katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya Manchester City kudaiwa kuwa na mpango wa kutaka kumsajili wakati huo. Pedri ni mmoja kati ya wachezaji vijana tegemeo katika kikosi cha Barcelona na Manchester City inaamini ikimpata itakuwa imefanikiwa kuboresha zaidi eneo la kiungo.


Bukayo Saka

WINGA wa Arsenal na timu ya taifa ya England, Bukayo Saka  anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu zaidi. Mazungumzo juu ya suala hilo yataanza hivi karibuni ikidaiwa mkurugenzi mpya wa michezo, Andrea Berta ni miongoni mwa kazi zake za kwanza.


Djordje Petrovic

KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca huenda akazuia mpango wa timu hiyo kusajili kipa mpya katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na badala yake akamrudisha Mserbia, Djordje Petrovic, ambaye anaichezea Strasbourg kwa mkopo pamoja na kumtumia kipa raia wa Ubelgiji, Mike Penders, 19, kwenye eneo hilo wakashindania namba.