Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utata VAR hadharani kwa mashabiki England

Muktasari:

  • Hatua hiyo ni miongoni mwa mikakati mitatu mipya iliyowekwa na Ligi Kuu England kuongeza uwazi kuhusu uamuzi wa waamuzi. Mikakati mingine ni kuchapisha maelezo ya moja kwa moja kutoka kwa waamuzi pamoja na kutumia RefCam yenye sauti ya mazungumzo kati ya mwamuzi na wachezaji.

LONDON, ENGLAND

LIGI Kuu England imeanza msimu huu kwa hatua mpya ya kuongeza uwazi, ikitangaza kuwa uamuzi wote ya Jopo la Matukio Muhimu ya Mechi (KMI Panel) kuhusu waamuzi na VAR yatawekwa wazi kwa mashabiki kwa mara ya kwanza.

Hatua hiyo ni miongoni mwa mikakati mitatu mipya iliyowekwa na Ligi Kuu England kuongeza uwazi kuhusu uamuzi wa waamuzi. Mikakati mingine ni kuchapisha maelezo ya moja kwa moja kutoka kwa waamuzi pamoja na kutumia RefCam yenye sauti ya mazungumzo kati ya mwamuzi na wachezaji.

Jopo la KMI lenye wajumbe watano limekuwa likikutana tangu msimu wa 2022/23 kutathmini maamuzi muhimu, lakini hadi sasa tathmini zake kamili zilikuwa siri, licha ya baadhi ya klabu kuhusishwa na kutoa taarifa hizo kwa vyombo vya habari.

Kila tukio kubwa hujadiliwa na kupigiwa kura, kisha mrejesho hutolewa kwa klabu na waamuzi.

Ligi Kuu inaamini kuchapisha nyaraka hizo kutawapa mashabiki picha kamili ya namna uamuzi yanavyotathminiwa.

Maelezo ya waamuzi kuwekwa wazi

Nukuu zilizochaguliwa moja kwa moja kutoka kwa mwamuzi na/au VAR zitachapishwa kupitia akaunti ya Premier League Match Centre kwenye X, tovuti rasmi ya Ligi Kuu na programu yake.

Hatua hiyo inalenga kuwapa mashabiki uelewa wa moja kwa moja kuhusu sababu zilizowafanya waamuzi kufikia uamuzi fulani.

Hapo awali, taarifa zilizokuwa zikichapishwa zilikuwa muhtasari wa tukio badala ya maelezo halisi ya wakati huo na namna mwamuzi au VAR walivyofikiri.

Mfumo huo mpya utajumuisha maelezo ya mwamuzi kuhusu sababu za kutoa uamuzi fulani au VAR kueleza moja kwa moja kwa nini haikuingilia tukio.

Aidha, matumizi ya RefCam yameongezwa, ambapo kwa mara ya kwanza mashabiki wataweza kusikia sauti ya mazungumzo kati ya mwamuzi na wachezaji wakati wa mchezo.

Hata hivyo, mazungumzo hayo hayatarushwa mubashara na hayatakuwa na mawasiliano kati ya mwamuzi na VAR. Badala yake, yatatumika mara moja au mbili kwa kila mzunguko wa mechi.

Ligi Kuu na Pro Ref zinaendelea kutafuta njia za kuongeza uwazi kuhusu maamuzi, ingawa bado zimewekewa mipaka na International Football Association Board (IFAB) ambayo haijaruhusu mawasiliano ya VAR kurushwa mubashara.

Ligi Kuu pia imeeleza kuwa itaendelea kufanya mazungumzo na IFAB ili kuruhusu taarifa zaidi za mawasiliano ya VAR kushirikishwa na umma.


KMI Panel inavyofanya kazi


Jopo hilo hukutana kila wiki kuchambua maamuzi mbalimbali, kuanzia mabao, penalti hadi kadi nyekundu.

Lina wajumbe watano, wakiwamo wachezaji na makocha watatu wa zamani, pamoja na mwakilishi mmoja kutoka Ligi Kuu na mwingine kutoka taasisi ya waamuzi ya Pro Ref.

Jopo hilo liliundwa na klabu za Ligi Kuu mwaka 2022 kwa lengo la kuhakikisha tathmini ya utendaji wa waamuzi haibaki mikononi mwa taasisi inayosimamia waamuzi.

Hata hivyo, KMI Panel hailichambui tukio kwa mtazamo wa shabiki au kocha pekee. Huangalia sheria za mchezo na, muhimu zaidi, namna Ligi Kuu inavyotarajia mechi zake zichezeshwe.


Ndiyo sababu idadi ya makosa inayobainishwa na jopo hilo wakati mwingine huwa ndogo kuliko ambavyo mashabiki wanavyotarajia.

Kwanza, jopo hutathmini uamuzi wa timu ya waamuzi waliokuwa uwanjani, kisha huangalia uamuzi wa VAR.

Kwa kuwa VAR inatakiwa kuingilia tukio pale ambapo kuna “kosa la wazi na dhahiri”, kuna nyakati ambazo jopo linaweza kubaini mwamuzi alikosea, lakini VAR ilikuwa sahihi kutokuingilia.

Jopo pia hutathmini matukio ambayo hayawezi kukaguliwa na VAR, ikiwamo kadi ya pili ya njano ambayo haikutolewa.

Baada ya hapo, kura ya wengi ndiyo huamua kama uamuzi ulikuwa sahihi au la.


Makosa ya VAR yapungua


Tathmini za msimu uliopita, zinaonyesha kuwa kulikuwa na makosa 25 ya VAR, ikiwa ni ongezeko kutoka 18 yaliyobainika katika msimu wa 2024/25.

Hata hivyo, idadi hiyo bado ni pungufu ikilinganishwa na misimu iliyotangulia, ambapo makosa 31 yalibainika msimu wa 2023/24 na 38 msimu wa 2022/23.

Matokeo ya tathmini hizo pia huambatana na maoni ya wajumbe wa jopo, wakieleza sababu zilizowafanya kufikia uamuzi husika.

Taarifa hizo pia hutumika katika kuamua malipo yanayohusishwa na utendaji wa waamuzi mwishoni mwa kila msimu.