Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usyk apiga marufuku simu za familia kuelekea pambano la Rico Verhoeven

USYK Pict

Muktasari:

  • Usyk anatarajiwa kutetea mkanda wake wa WBC kesho Jumamosi dhidi ya Verhoeven, ambaye licha ya kutoshindwa katika mchezo wa kickboxing kwa zaidi ya muongo mmoja, ana rekodi ya pambano moja tu la ngumi za kulipwa. 

CAIRO, MISRI: BINGWA wa dunia wa uzani wa juu wa WBC, Oleksandr Usyk, ameonyesha nidhamu ya hali ya juu baada ya kupiga marufuku matumizi ya simu na ukaribu wa familia yake kwenye kambi yake ya mafunzo, akijiandaa kumkabili gwiji wa kickboxing, Rico Verhoeven, nchini Misri.

Usyk anatarajiwa kutetea mkanda wake wa WBC kesho Jumamosi dhidi ya Verhoeven, ambaye licha ya kutoshindwa katika mchezo wa kickboxing kwa zaidi ya muongo mmoja, ana rekodi ya pambano moja tu la ngumi za kulipwa. 

Licha ya takwimu hizo kumfanya Verhoeven aonekane mpinzani dhaifu zaidi wa Usyk kwenye makaratasi, bingwa huyo wa mataji mawili asiyepigika hachukulii pambano hilo kirahisi hata kidogo.

USY 01

Mtu aliyeshuhudia maandalizi hayo ni ‘jitu’ la Serbia, Sanel Hasanovic (mwenye urefu wa futi 6 na inchi 9), ambaye amekuwa msaidizi mkuu wa Usyk katika masuala ya sparing (mazoezi ya ngumi) kwa mapambano yake saba yaliyopita.

Hasanovic amefichua kuwa hajawahi kumwona Usyk akiwa makini kiasi hicho katika kazi yake, huku akikata kabisa mawasiliano na usumbufu wowote wa nje.

Akizungumza kupitia mkalimani, Hasanovic amesema: "Usyk amejikita kwenye kambi tu. Hana familia hapa hakuna mke wala watoto. Yuko peke yake na timu yake kwenye nyumba moja. Huko nyuma tulikuwa tunajumuika na kwenda kula chakula cha jioni pamoja, lakini kambi hii, Usyk anaonekana ameelekeza akili yake yote kwa Rico.

USY 02

"Tunamwona gym pekee, lakini baada ya hapo anarudi kujifungia kujiandaa. Sijawahi hata mara moja kumwona akitumia simu mazoezini. Ana nidhamu ya hali ya juu sana."


Kauli hiyo imeungwa mkono na Sergey Lapin, mmoja wa washauri wa karibu wa Usyk anayesaidia kuendesha kambi hiyo, akisema: " Usyk anazingatia mpinzani wake kila sekunde. Hizi ni ngumi, usipokuwa makini mambo yanaharibika. Hakuna familia, hakuna simu. Ni ngumi tu."

Ingawa Verhoeven ana uzoefu mdogo wa ngumi za kulipwa, si mgeni wa mchezo huo. Amefundishwa na Peter Fury (mjomba wa Tyson Fury) kwa miaka 15 iliyopita na alikuwa msaidizi wa muda mrefu wa Tyson Fury katika mazoezi, bondia ambaye Usyk alimshinda mara mbili mwaka 2024.

USY 03

Silaha kubwa ya Verhoeven ni umbo lake kubwa la futi 6 na inchi 4 pamoja na uzito wa mawe 19 (stone 19). Hilo limemfanya Usyk kuweka mkazo mkubwa kwenye kuongeza nguvu za mwili na nguvu ya makonde.

Hasanovic ameeleza kasi ya mazoezi yao: "Anazidi kusukuma mbele nguvu yake ya kupiga na kila kambi Usyk anavuka mipaka yake. Inaonekana anakuwa imara zaidi kila kukicha. Wiki mbili au tatu za kwanza zilikuwa za mbinu, lakini baada ya hapo ‘mzuka’ ulipanda. Mazoezi yetu ya mwisho yalikuwa vita kali. Tulicheza raundi nne tu na mimi, lakini ilikuwa vita ya ‘kichaa’."

Kutokana na kipigo alichokipata kwenye raundi ya nne ya mazoezi hayo ya mwisho, Hasanovic ana mashaka makubwa kama Verhoeven atamudu dhoruba la Usyk.