Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapinduzi yalivyoubadilisha mchezo wa ngumi

NGUMI Pict

Muktasari:

  • Mabondia wa kipindi hiki walikuwa na mchanganyiko wa vitu vingi ikiwemo, nguvu na ujasiri. Kulikuwa na ushindani mkali kati ya mabingwa wak ub wa, jambo lililofanya kila pambano kuwa la hatari na lisilotabirika.

LONDON, ENGLAND: NDONDI za uzito wa juu (heavyweight boxing) zimekuwa moja ya michezo yenye mvuto mkubwa duniani kwa miongo kadhaa.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2020, ndondi za uzito wa juu au masumbwi kama wengi ambavyo wamekuwa wakiita, zimepitia mageuzi makubwa, kutoka enzi ya mabondia wakali waliotegemea nguvu na kasi ya kumaliza mapambano mapema, hadi zama za kisasa zilizojaa mbinu za kisayansi na maandalizi ya kibabe.

NGUM 05
NGUM 05

ENZI YA DHAHABU

Miaka ya 1990 inatajwa mara nyingi kama enzi ya dhahabu ya ndondi za uzito wa juu. Hiki kilikuwa kipindi ambacho kila pambano lilikuwa na mvuto wa kipekee na mashabiki walijaa viwanjani na mbele ya televisheni wakisubiri mapambano ya kihistoria.

Mabondia wa kipindi hiki walikuwa na mchanganyiko wa vitu vingi ikiwemo, nguvu na ujasiri. Kulikuwa na ushindani mkali kati ya mabingwa wak ub wa, jambo lililofanya kila pambano kuwa la hatari na lisilotabirika.

Miongoni mwa mabondia ambao walitikisa katika enzi ya dhahabu ni pamoja na Mike Tyson ambaye alitokea Brooklyn, New York, katika mazingira magumu yaliyojaa uhalifu. Alichukuliwa chini ya uangalizi wa kocha Cus D’Amato, ambaye alimjenga kisaikolojia, akimfundisha nidhamu ya  mapigano ulingoni.

Tyson alipanda kwa kasi ya ajabu na kuwa bingwa wa dunia akiwa na miaka 20, akivunja rekodi ya kuwa bingwa mdogo zaidi wa uzito wa juu katika historia.

Mtindo wake wa kupigana ulikuwa wa kutisha akiwa na kasi ya ajabu, mashambulizi ya karibu na nguvu za kumaliza pambano ndani ya raundi chache. Wapinzani wengi waliingia ulingoni tayari wakiwa na hofu.

Hata hivyo, maisha yake binafsi yaliambana na majanga, misukosuko ya kifedha na changamoto za kisaikolojia yalifanya utawala wake kuyumba. Licha ya hayo, Tyson anabaki kuwa sura isiyofutika katika historia ya ndondi.

Mwamba mwingine ni Evander Holyfield, anatajwa kuwa na moyo wa chuma huku akiwa na sifa ya uvum ilivu.

Evander alijijenga kupitia bidii, nidhamu na uwezo wa kustahimili maumivu makali. Akitokea familia ya kipato cha chini, alijituma hadi kufikia kuwa bingwa wa dunia.

NGUM 04

Tofauti na Tyson, Evander alitegemea akili, mbinu na uimara wa mwili. Alijulikana kwa uwezo wake wa kubadilisha mikakati katikati ya pambano na kuendelea kupigana hata alipokuwa amejeruhiwa.

Mapambano yake dhidi ya Tyson yalibeba historia kubwa, hasa tukio la kung’atwa sikio ambalo lilibadilisha taswira ya ndondi za uzito wa juu duniani.

Mbali na hao pia yupo, Lennox Lewis anatajwa kama mfalme wa mbinu na nidhamu. Lewis alizaliwa Uingereza na kukulia Canada.

Alijulikana kwa kutumia urefu wake, ngumi kali na akili ya mchezo kudhibiti wapinzani. Tofauti na mabondia wengi wa enzi yake, Lewis alikuwa mpiganaji mwenye utulivu mkubwa na mipango ya muda mrefu.

Akiwa bingwa wa Olimpiki, alifanikiwa kujenga taaluma yenye mafanikio makubwa na alistaafu akiwa bado bingwa, jambo linalodhihirisha ubora wake.

Mwamba mwingine alikuwa Riddick Bowe alikuwa mmoja wa mabondia wenye kipaji cha asili kilichovutia sana. Aliweza kumshinda Evander Holyfield katika mapambano makubwa na kuonyesha uwezo wa juu wa kimwili na kiufundi.

Hata hivyo, ukosefu wa nidhamu, maamuzi mabaya nje ya ulingo na changamoto binafsi zilichangia kuporomoka kwa kasi.

NGUM 03

MAPINDUZI ULAYA MASHARIKI

Baada ya enzi ya Marekani kutawala, miaka ya 2000 ilileta mabadiliko makubwa ambapo mabondia kutoka Ulaya Mashariki walichukua nafasi ya juu.

Miongoni mwa miamba ya kizazi hiki ni pamoja na Wladimir Klitschko, anatajwa kuwa kati ya wababe wa ngumi za kisasa kwa wakati huo.

Klit schko alitumia urefu wake, nguvu ya ngumi zake kuwaangusha mabondia wengi.

NGUM 01

Mwamba mwingine alikuwa Vitali Klitschko alijulikana kwa mtindo wake wa kupigana kwa nguvu na uwezo wa kustahimili maumivu bila kusimama.

Alikuwa bingwa ambaye mara nyingi aliwazidi wapinzani wake kwa uimara na moyo wa kupigana. Baada ya kuacha ndondi, aligeukia siasa na kuwa kiongozi muhimu nchini Ukraine.

David Haye alileta msisimko mpya kwa uzito wa juu kupitia kasi, ujasiri na mtindo wa kushambulia kwa kustukiza.

Alikuwa tofauti na mabondia wa Ulaya Mashariki waliotegemea urefu na udhibiti wa umbali na hivyo kuongeza utofauti wa kimtindo katika kipindi hicho.

Nikolai Valuev, akiwa mmoja wa mabondia warefu na wakubwa zaidi kuwahi kuonekana, Valuev alitumia ukubwa wake kama silaha kuu.

Ingawa hakujulikana kwa kasi au ubunifu mkubwa, uwepo wake ulingoni uliwalazimisha wapinzani kubadili mikakati yao.

NGUM 02

KIZAZI KIPYA SASA

Katika miaka ya 2020, ndondi za uzito wa juu zimeingia katika kipindi cha ushindani wa wazi duniani. Hakuna taifa moja linalotawala na mabondia kutoka maeneo mbalimbali wameleta mitindo tofauti ya mchezo.

Kuna Tyson Fury  ambaye anatajwa kuwa ni bingwa wa akili, urefu na uwezo wa kurudi mchezoni hata pale ambapo anapoteza mwelekeo. Fury ni mmoja wa mabondia wenye hadithi ya kipekee zaidi. Baada ya kumshinda Wladimir Klitschko, alikumbwa na changamoto kubwa za afya ya akili na kuacha ndondi kwa muda.

Kurudi kwake kulikuwa kwa kishindo kikubwa. Mapambano yake dhidi ya Deontay Wilder yalibadilisha taswira ya ndondi za kisasa.

Usyk alitawala kwanza cruiserweight kabla ya kupanda uzito wa juu. Ana kasi ya miguu, mbinu na uwezo wa kusoma wapinzani kwa haraka.

Ushindi wake dhidi ya Anthony Joshua ulimweka miongoni mwa mabondia bora.

Joshua alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na nguvu zake, nidhamu ya mazoezi, na mvuto wake kwa mashabiki.

Alileta hamasa mpya katika ndondi za Uingereza na kuchangia kukuza umaarufu wa mchezo duniani.

Deontay Wilder anajulikana kwa uwezo wake wa kumaliza pambano kwa pigo moja la mkono wa kulia.