Trossard aiteka Istanbul, mashabiki wapagawa kumshuhudia
Muktasari:
- Nyota huyo anatarajia kutambulishwa rasmi leo kwa mashabiki kwenye uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo, Tüpraş Stadyumu (zamani Vodafone Park), huku mamia ya mashabiki wenye shauku kubwa wakijitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Kiungo mshambuliaji wa Ubelgiji, Leandro Trossard, amegeuka kivutio kwa mashabiki wa Besiktas jijini Istanbul baada ya kukamilisha usajili wake akitokea kwa mabingwa wa England, Arsenal.
Nyota huyo anatarajia kutambulishwa rasmi leo kwa mashabiki kwenye uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo, Tüpraş Stadyumu (zamani Vodafone Park), huku mamia ya mashabiki wenye shauku kubwa wakijitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Baada ya utambulisho huo wa kifahari uwanjani, Trossard atapata wasaa wa kipekee wa kukutana na mashabiki na kusaini jezi zao kama sehemu ya kuwakaribisha na kuanza safari yake mpya nchini Uturuki.
Kuondoka kwa Trossard kumeisukuma Arsenal sokoni ambapo tayari imeshaziba pengo lake kwa kumsajili Christos Tzolis.
Ephraim Bahemu amepiga story na shabiki mmoja wa timu hiyo ambaye ameelezea furaha yake na matarajio yake kwa mchezaji huyo.