Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Trump amsifia tena Harry Kane

Kane Pict

Muktasari:

  • Trump alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya England kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico katika mechi ya Kombe la Dunia iliyopigwa Uwanja wa Estadio Azteca.

LOS ANGELES, MAREKANI: RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kumpa sifa nahodha wa England, Harry Kane, akimtaja kuwa mmoja wa wachezaji bora na kufichua kuwa aliwahi kucheza naye mchezo wa gofu.

Trump alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya England kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico katika mechi ya Kombe la Dunia iliyopigwa Uwanja wa Estadio Azteca.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval, Trump amesema alikuwa amevutiwa sana na kiwango cha Kane.

"Ilikuwa mechi nzuri sana kati ya England na Mexico. Siwajui wachezaji wengi, lakini nadhani Harry Kane ni mchezaji mkubwa. Nilicheza naye gofu na ninampenda sana. Ni mzuri kwenye gofu, lakini uwanjani ni bora zaidi. Hukuweza kuiondolea macho mechi hiyo," amesema Trump.

Trump, ambaye anamiliki viwanja kadhaa vya gofu nchini Marekani, pamoja na Kane wote ni wapenzi wa mchezo huo, ingawa haijaelezwa walicheza pamoja lini au wapi.

Hii si mara ya kwanza kwa Trump kumsifia mshambuliaji huyo wa Bayern Munich. Baada ya Kane kufunga kwa penalti dhidi ya Mexico, Rais huyo aliandika kwenye mtandao wake wa Truth Social:

"Harry Kane wa England ni MCHEZAJI MKUBWA!!!"

Katika mchezo huo, England ilitinga robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 3-2. Jude Bellingham aliifungia timu hiyo mabao mawili ndani ya dakika mbili za kipindi cha kwanza kabla ya Kane kuongeza la tatu.

Mexico ilijaribu kurejea kupitia penalti ya Raul Jimenez, lakini haikutosha kuizuia England kusonga mbele.

Sasa kikosi cha kocha Thomas Tuchel kinajiandaa na mchezo wa robo fainali dhidi ya Norway, ambayo ilifuzu baada ya kuifunga Brazil mabao 2-1 huku Erling Haaland akifunga mabao yote mawili ya ushindi.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa jijini Miami wikiendi ijayo.

England ilikabiliwa na changamoto za hali ya hewa, mwinuko wa Jiji la Mexico pamoja na kelele za mashabiki waliokesha nje ya hoteli ya timu, lakini hilo halikuwazuia kuonyesha kiwango bora na kupata ushindi muhimu.

Ushindi huo tayari umeanza kutajwa kuwa miongoni mwa mechi bora zaidi katika historia ya Kombe la Dunia na umeongeza matumaini ya England kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1966.