Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tevez afichua bifu na Ferguson

TEVEZ Pict

Muktasari:

  • Carlos Tevez aliwahi kumchana  Ferguson, baada ya Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England miaka 14 iliyopita, akishikilia bango lililoandikwa “RIP Fergie” katika sherehe za ubingwa huo.

LONDON, ENGLAND: CARLOS TEVEZ amedai kuwa aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, alivunja ahadi aliyompa kuhusu mkataba wake, jambo alilosema lilichangia uamuzi wake wa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na wapinzani wao wa jadi, Manchester City, mwaka 2009.

Tevez, aliyekuwa akiichezea United kwa mkopo, alihamia City na baadaye kutwaa taji la Ligi Kuu England  mara ya tatu. Katika sherehe za ubingwa wa City mwaka 2012, mshambuliaji huyo alionekana akiwa ameshikilia bango lililoandikwa ‘RIP Fergie’, kitendo kilichozua mjadala mkubwa.

Carlos Tevez aliwahi kumchana  Ferguson, baada ya Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England miaka 14 iliyopita, akishikilia bango lililoandikwa “RIP Fergie” katika sherehe za ubingwa huo.

TEVE 01

Tevez, ambaye alihama United na kujiunga na wapinzani wao wa jadi, City, mwaka 2009, alitetea kitendo chake akisema Ferguson alikuwa akiwakosoa wachezaji bila kulazimika kuomba msamaha, lakini wengine walipotania walitakiwa kufanya hivyo.

“Ni kama Ferguson ndiye rais. Anapozungumza vibaya kuhusu mchezaji, hakuna anayesema anatakiwa kuomba msamaha. Lakini mtu mwingine akifanya mzaha, anatakiwa kuomba msamaha. Mimi siombi msamaha,” amesema Tevez.

Kwa muda mrefu, Tevez amekuwa akijaribu kueleza sababu za kitendo hicho. Sasa amefichua kuwa uhusiano wake na Ferguson ulianza kuharibika baada ya kocha huyo kushindwa kutimiza ahadi ya kumsajili moja kwa moja.

TEVE 02

Akizungumza katika kipindi cha Rio Ferdinand Presents, Tevez amesema United ilikuwa imekubaliana naye mkataba wa mkopo wa miaka miwili, huku kukiwa na mazungumzo kwamba angeweza kusajiliwa moja kwa moja baada ya mwaka mmoja endapo angeonyesha kiwango kizuri.

“Ferguson aliniambia, ‘Carlos, sasa nitalipia mkataba wako na utabaki Manchester’. Timu ilikwenda kwenye maandalizi ya msimu mpya. Nakumbuka mazungumzo hayo na Ferguson. Amesema angelipia usajili wa Berbatov, lakini kuhusu mimi nisiwe na wasiwasi kwa sababu angenisajili na tungefanya mkataba,” amesema Tevez.

Hata hivyo, ahadi hiyo haikutimizwa, huku United ikikataa kulipa ada iliyohitajika ili kumsajili moja kwa moja. Tevez aliendelea kubaki klabuni hapo kwa mwaka mwingine kabla ya kuondoka.

TEVE 03

Akizungumzia namna mashabiki wa United walivyopokea uamuzi wake wa kujiunga na City, Tevez amesema wengi hawakuwa na ufahamu wa kilichotokea nyuma ya pazia kati yake na Ferguson.

“Kwa upande wangu, naamini watu wanaelewa. Lakini hawaelewi kuhusu Ferguson kuzungumza nami na mambo yaliyotokea nyuma ya pazia. Kilichotokea kati yangu na Ferguson, nafikiri watu hawakielewi,” amesema.

Tevez ameongeza kuwa Ferguson alikuwa na muda wa hadi miezi sita tangu walipozungumza kutimiza ahadi yake, lakini badala yake alianza kumuweka benchi.

“Kilichoniumiza zaidi ni kwamba Ferguson alikuwa na hadi miezi sita ya kutimiza ahadi yake, lakini hakufanya hivyo. Kinyume chake, alianza kuniacha benchi. Nilihisi alikuwa ananisukuma pembeni ili kupunguza thamani yangu,” amesema.

TEVE 04

Aliyekuwa beki wa United, Rio Ferdinand, alionyesha kuelewa upande wa Tevez, akidai kuondoka kwa mshambuliaji huyo kulikuwa pigo kwa klabu hiyo, ambayo haijashinda tena taji la Ligi Kuu England tangu mwaka 2013.

Licha ya yaliyotokea, Tevez amesema bado ana kumbukumbu nzuri za kipindi chake Manchester United, ingawa aliumizwa na namna alivyohisi kutendewa baada ya kutoa mchango wake kwa timu hiyo.

“Kwangu ilikuwa ngumu, Rio. Nilihisi nimeutoa moyo wangu kwa United, lakini sikuhisi kupokea kitu kilekile. Tulishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu, lakini baadaye walipoleta mchezaji mwingine, nilihisi walikuwa wanajaribu kupunguza thamani yangu,” amesema.

Tevez alikiri kuwa baada ya kujiunga na Manchester City, aliiona hatua hiyo kama njia ya kulipiza kisasi kwa United.

“Nilikuwa na wakati mzuri sana United. Lakini City, kwangu, ilikuwa kama kulipiza kisasi. Sikupata kile nilichohisi nilikuwa nimetoa kwa United,” amesema Tevez, ambaye sasa ni kocha na hivi karibuni aliinoa Talleres ya nchini Argentina.