Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Supercomputer yampa Harry Kane Ballon d’Or, Yamal asubiri

KANE Pict

Muktasari:

  • Utabiri huo umetolewa na mfumo wa kompyuta maalumu wa kampuni ya Canadian Sports Betting, ambao umechambua uwezekano wa washindani wa tuzo hiyo na kutaja pia wachezaji wanaoweza kutwaa tuzo hiyo katika miaka 10 ijayo.

LONDON, ENGLAND: MSHAMBULIAJI HARRY Kane ametabiriwa kutwaa tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka huu, huku Lamine Yamal wa Barcelona akitabiriwa kuwa mchezaji atakayokusanya tuzo nyingi zaidi katika muongo ujao, akitarajiwa kushinda mara tatu ifikapo mwaka 2036.

Utabiri huo umetolewa na mfumo wa kompyuta maalumu wa kampuni ya Canadian Sports Betting, ambao umechambua uwezekano wa washindani wa tuzo hiyo na kutaja pia wachezaji wanaoweza kutwaa tuzo hiyo katika miaka 10 ijayo.

Kane, mshambuliaji wa Bayern Munich, amepewa nafasi ya asilimia 58 ya kushinda tuzo hiyo kutokana na kiwango chake bora, baada ya kufunga mabao 61 katika msimu uliopita akiwa na klabu hiyo na kufikisha mabao 73 kwa ujumla akijumuisha mechi za klabu na timu ya taifa.

Nyota huyo wa England anachuana na Yamal wa Barcelona na Kylian Mbappe wa Real Madrid katika kinyang’anyiro hicho, huku Yamal akipewa nafasi ya asilimia 18 ya kutwaa tuzo hiyo mwaka huu.

KAN 03

Hata hivyo, licha ya kutabiriwa kukosa tuzo ya mwaka huu, Yamal anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kutawala tuzo hiyo katika miaka ijayo. Mfumo huo unatabiri kuwa atarejea kwa nguvu na kutwaa Ballon d’Or ya mwaka 2027.

Baada ya hapo, kiungo wa Real Madrid na England, Jude Bellingham, anatabiriwa kutwaa tuzo ya mwaka 2028, hatua itakayomfanya kuwa Mwingereza mwingine kushinda tuzo hiyo baada ya Kane, kama utabiri wa mwaka huu utatimia, na Michael Owen aliyeshinda mwaka 2001.

Nyota wa Bayern Munich, Michael Olise, anatabiriwa kutwaa tuzo ya mwaka 2029, kabla ya mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, kupewa nafasi ya kushinda mwaka 2030.

Yamal anatarajiwa kutwaa tuzo yake ya pili mwaka 2031, huku mshambuliaji wa Real Madrid, Endrick, akitabiriwa kuandika historia yake kwa kushinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2032.

KAN 01

Mwaka 2033, beki wa Barcelona, Pau Cubarsi, anatabiriwa kuwa beki wa kwanza kutwaa tuzo hiyo tangu Fabio Cannavaro wa Italia aliposhinda mwaka 2006.

Kiungo wa Real Madrid, Arda Guler, ametajwa kuwa mshindi anayetarajiwa wa mwaka 2034, kabla ya Yamal kutwaa tuzo yake ya tatu mwaka 2035.

Utabiri huo unafungwa na kinda wa Chelsea, Estevao, ambaye anatarajiwa kutwaa tuzo ya mwaka 2036.

Tuzo ya mwaka huu inatarajiwa kumpata mshindi mpya baada ya Ousmane Dembele wa Paris Saint-Germain kutwaa tuzo ya mwaka 2025.

Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo, ambayo itakuwa toleo la 70, inatarajiwa kufanyika London kwa mara ya kwanza, katika ukumbi wa London Palladium, huku ikitarajiwa kuongozwa na nyota wa CBS Sports, Thierry Henry na Kate Scott.

Licha ya kutajwa kuwa nyuma ya Kane katika utabiri huo, Yamal anaamini anastahili kutwaa tuzo hiyo kutokana na mafanikio yake ya msimu uliopita, akiwamo kutwaa taji la La Liga na Kombe la Dunia, kama ilivyonukuliwa katika taarifa ya chanzo.

KAN 02

"Nadhani ninastahili kushinda mwaka huu kutokana na yale niliyoshinda," amesema Yamal.

Alipoulizwa angempa nani tuzo hiyo, alijibu: "Mchezaji bora zaidi duniani. Wao watampa nani? Hilo ni mjadala mrefu sana."

Utabiri wa washindi wa Ballon d’Or hadi 2036

- 2026 – Harry Kane

- 2027 – Lamine Yamal

- 2028 – Jude Bellingham

- 2029 – Michael Olise

- 2030 – Erling Haaland

- 2031 – Lamine Yamal

- 2032 – Endrick

- 2033 – Pau Cubarsí

- 2034 – Arda Güler

- 2035 – Lamine Yamal

- 2036 – Estevao