Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saka aumia, Arteta aingia hofu

SAKA Pict

Muktasari:

  • Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema ana wasiwasi kuhusu hali ya mchezaji huyo wa England, ambaye alionekana kupata maumivu makali baada ya kupiga mpira kwa sehemu ya ndani ya mguu na kuanguka chini huku akionyesha kupata maumivu makali.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imepata pigo baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Bukayo Saka kulazimika kutoka uwanjani dakika za mwanzo za mchezo dhidi ya Bayern Munich kutokana na jeraha lililomfanya ashindwe kuendelea na mchezo.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema ana wasiwasi kuhusu hali ya mchezaji huyo wa England, ambaye alionekana kupata maumivu makali baada ya kupiga mpira kwa sehemu ya ndani ya mguu na kuanguka chini huku akionyesha kupata maumivu makali.

Madaktari wa timu waliingia uwanjani kumhudumia Saka kabla ya kuamua kuwa hangeweza kuendelea na mchezo. Alipotoka, alizungumza kwa muda mfupi na Arteta huku akionyesha eneo la paja lake lililokuwa likimuumiza.

SAK 01

Akizungumza baada ya mchezo huo uliomalizika kwa sare 2-2, Arteta amesema: “Madaktari wana wasiwasi kiasi. Mchezaji anapotakiwa kutoka uwanjani kutokana na maumivu makali ya ghafla, kwa kawaida hiyo si habari njema, lakini tunapaswa kusubiri na kuona.”

Picha za kipekee zilizorekodiwa na SunSport zilimwonyesha Saka akitembea kwa kuchechemea alipoondoka katika Uwanja wa Allianz Arena. Hata hivyo, aliweza kutembea mwenyewe bila kusaidiwa wala kutumia magongo.

Kutoka kwa Saka kulimpa nafasi Eberechi Eze kuingia uwanjani, huku Noni Madueke akihamishwa kutoka winga ya kushoto kwenda kulia.

SAK 02

Eze, ambaye alitolewa kipindi cha kwanza katika mchezo uliopita dhidi ya Nottingham Forest, alitumia nafasi hiyo kujionyesha baada ya kufunga bao kwa mkwaju wa mguu wa kushoto dakika ya 25.

Bao hilo awali lilionekana kuwa la kuotea, lakini baada ya kupitia mfumo wa VAR, mwamuzi alilikubali na kuifanya Arsenal kurejea mchezoni.

Licha ya Arsenal kupoteza huduma ya Saka, Bayern pia ilianza mchezo huo bila nyota wake Michael Olise na Luis Diaz. Hata hivyo, mabingwa hao wa Ujerumani walijibu kwa kusawazisha kupitia Alphonso Davies wa Canada.

Kipindi cha pili kiliendelea kuwa na ushindani mkali, huku Harry Kane akiipa Bayern uongozi kwa mkwaju wa penalti kabla ya Declan Rice kuisawazishia Arsenal kwa bao lililotokana na shambulizi lililoandaliwa vizuri, zikiwa zimesalia dakika 10 za mchezo.

SAK 03

Diaz, ambaye awali alikosekana kama tahadhari kutokana na hali yake ya kiafya, aliingia akitokea benchi, lakini alilazimika kutolewa tena baada ya kucheza kwa chini ya dakika 20.

Hali ya Saka sasa inasubiriwa kwa karibu na Arsenal, huku majibu ya uchunguzi wa kitabibu yakitarajiwa kutoa picha iliyo wazi zaidi kuhusu ukubwa wa jeraha lake na muda anaoweza kukaa nje ya uwanja.