Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Steve McManaman: Diego Simeone ni ‘ndumilakuwili’ hana nidhamu

SIMIONE Pict

Muktasari:

  • Sehemu ya mashabiki wameunga mkono kauli yake kuhusu nidhamu ya Atletico, huku wengine wakiamini kuwa VAR ndiyo chanzo cha vurugu zote zinazotokea uwanjani kwa sasa.

GWIJI wa soka na mchambuzi wa michezo, Steve McManaman, amemlipua kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, akitaja tabia yake kuwa ni ‘fedheha’ kufuatia matukio yaliyotokea katika sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

McManaman, ambaye alikuwa akifanya uchambuzi wa mechi hiyo, amekerwa na kitendo cha Simeone na benchi lake la ufundi kumshambulia mwamuzi kwa maneno na kumzunguka wakati akielekea kwenye VAR kwa ajili ya kufanya uamuzi muhimu.

"Ni tabia ya hovyo na fedheha," amesema McManaman akizungumza kwa hisia kali.

McManaman amesema vitendo vya Simeone havina nafasi katika soka la kisasa na vinadhalilisha mchezo huo.

SIMI 02

"Ni tabia ya hovyo, ni fedheha, na haina nafasi kabisa katika soka. Walikuwa wakimzunguka mwamuzi na kumshinikiza wakati akijaribu kutumia VAR. Inasikitisha kuona kocha mkubwa anafanya hivyo," amesea McManaman.

Gwiji huyo ameongeza kuwa, Simeone ana tabia ya ‘ndumilakuwili’.

"Kama tukio hilo lingetokea upande wa pili, Simeone angekuwa wa kwanza kuruka na kudai penalti kwa nguvu zote.

Mbali na kumshambulia Simeone, McManaman ameonyesha kukasisrishwa na teknolojia ya VAR, akidai kuwa imekuwa kikwazo kwa ladha ya soka na inachangia kuongeza utovu wa nidhamu uwanjani.

Kwa msisitizo mkubwa, McManaman alisikika akisema: "Naichukia VAR, naichukia, naichukia, naichukia!" Akieleza kuwa VAR imekuwa ikikatisha mtiririko wa mchezo na kuleta migogoro isiyo ya lazima kati ya waamuzi na makocha, jambo ambalo linaonekana kumpandisha hasira mara kwa mara tangu kuanzishwa kwake.

SIMI 01

Sare hiyo ya 1-1 imeiacha Arsenal ikiwa na kazi ya ziada kuelekea mchezo wa marudiano jijini London, lakini maoni ya McManaman yamegeuka kuwa mjadala mkuu.

Sehemu ya mashabiki wameunga mkono kauli yake kuhusu nidhamu ya Atletico, huku wengine wakiamini kuwa VAR ndiyo chanzo cha vurugu zote zinazotokea uwanjani kwa sasa.