Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sterling hatarini kufungwa England

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea na Manchester City alisimama kizimbani na kukubali mashtaka matatu, juzi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Basingstoke kusikiliza jinsi alivyoendesha gari kwa muda mrefu na kwa uzembe kwenye barabara za M25 na M3, huku akivuta puto zenye nitrous oxide, kabla ya kugongesha gari lake lenye thamani ya Pauni 270,000 kwenye ukuta.

LONDON, ENGLAND; RAHEEM Sterling amekiri kosa la kuendesha gari vibaya na anaweza kufungwa jela baada ya kuendesha Lamborghini yake kwa zaidi ya saa moja kwenye barabara kuu wakati wa msongamano wa magari, huku akivuta 'nitrous oxide'.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea na Manchester City alisimama kizimbani na kukubali mashtaka matatu, juzi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Basingstoke kusikiliza jinsi alivyoendesha gari kwa muda mrefu na kwa uzembe kwenye barabara za M25 na M3, huku akivuta puto zenye nitrous oxide, kabla ya kugongesha gari lake lenye thamani ya Pauni 270,000 kwenye ukuta.

Sterling alipigwa marufuku kuendesha gari na kupewa dhamana hadi Novemba 25, ambapo adhabu yake itaamuliwa au kesi kupelekwa Mahakama nyingine kwa usikilizwaji zaidi.

Hata hivyo, mchezaji huyo pia alikiri kumiliki nitrous oxide na kukataa kutoa sampuli kwa ajili ya kipimo ili kujua alikuwa amelewa kiasi gani.

Adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha miaka miwili jela, ingawa inaaminika zaidi anaweza kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 hadi 18 na, kutokana na sababu za kupunguza adhabu kinaweza kusitishwa.

Kati ya saa 1.45 asubuhi na saa 2.52 asubuhi, Mei 28, polisi walipokea simu nyingi zikitoa taarifa kuhusu uendeshaji hatari wa gari muda mfupi baada ya Sterling kurejea England baada ya kuwa kwa mkopo Feyenoord, ambako alikuwa akijaribu kufufua tena maisha yake ya soka.

Video iliyorekodiwa na kamera ya gari la mtu mwingine na kutolewa kwa polisi na mmoja wa mashahidi ilionyesha gari la Sterling likibadilisha njia za barabarani na kukaribia kugonga kizuizi cha katikati ya barabara. Mashahidi waliripoti kumuona dereva akivuta kitu kutoka katika puto huku akiendesha.

Video kutoka kwenye kamera zilizokuwa kwenye miili ya maofisa wa polisi waliofika eneo la tukio zilizochezwa mahakamani zilimuonyesha Sterling, mwenye umri wa miaka 31 akiwa ameketi kwenye kiti cha abiria akiwa na mitungi miwili mapajani kabla ya kuthibitisha kuwa ndiye aliyekuwa akiendesha gari.

Indaiwa kwamba Sterling alionekana kuwa na nia ya kuhamisha puto iliyokuwa imepungua kutoka pembeni yake na kuiweka kwenye kiti cha nyuma cha abiria. Mate yake yalifanyiwa vipimo na hakukuwa na dalili za matumizi ya bangi au cocaine, lakini baadaye alikataa kutoa sampuli ya damu kwa ajili ya kupima uwepo wa dawa nyingine.

Hakimu aliamuru kuandaliwa kwa ripoti kabla ya hukumu na kuahirisha kusikilizwa kwa kesi hiyo, akisema bado hajaamua kama ataendelea kusikiliza kesi hiyo au kuipeleka katika mahakama ya juu. Mahakama ya Hakimu haiwezi kutoa hukumu ya kifungo cha zaidi ya miezi 12.

“Nitakuachia kwa dhamana bila masharti. Usipofika (mahakamani), hati ya kukamatwa itatolewa dhidi yako. Kuanzia leo nakupiga marufuku kuendesha gari. Kuanzia leo hupaswi kuendesha gari lolote kwenye barabara. Nitaamua muda wa marufuku hiyo iwapo nitakuhukumu, vinginevyo suala hilo litashughulikiwa na Mahakama ya Crown. Hupaswi kuendesha gari ukiwa umepigwa marufuku ukiendesha i ukiwa umepigwa marufuku, utakuwa umetenda kosa linaloweza kukufanya kufungwa jela,” alisema hakimu.