Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hat trick za Kelvin John mtihani CECAFA U-20

KELVIN Pict
KELVIN Pict

Muktasari:

  • Katika orodha ya wafungaji, kinachosubiriwa ni kuona kama kuna atakayefunga mabao mengi ikiwamo Hat trick ambayo katika historia ya michuano hiyo, rekodi inashikiliwa na mshambuliaji wa Mtanzania, Kelvin John.

Wakati michuano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA U-20 ikiendelea kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kuna mambo mengi yanatarajiwa kutokea ikiwamo ufungaji wa mabao.

Katika orodha ya wafungaji, kinachosubiriwa ni kuona kama kuna atakayefunga mabao mengi ikiwamo Hat trick ambayo katika historia ya michuano hiyo, rekodi inashikiliwa na mshambuliaji wa Mtanzania, Kelvin John.

Ndiyo. Kelvin ndiye anayeshikilia rekodi ya kipekee katika ya kuwa mchezaji pekee tangu mwaka 2010 kufunga hat-trick katika matoleo mawili tofauti ya mashindano hayo.

Hat-trick yake ya kwanza aliifunga mwaka 2019 mashindano hayo yalipofanyika Uganda, mshambuliaji huyo alifunga mabao hayo dhidi ya Zanzibar, Ngorongoro iliposhinda mabao 5-0.

Kelvin alifungua akaunti ya mabao dakika ya 51, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti, kisha kukamilisha hat-trick hiyo dakika ya 90.

KELV 01

Mwaka mmoja baadaye, katika CECAFA U-20 ya 2020, mshambuliaji huyo alirudia rekodi hiyo wakati Ngorongoro Heroes ilipoichapa Somalia 8-1.

Nyota huyo Kelvin alifunga mabao yake katika dakika za 29, 34 na 48, akitengeneza hat-trick yake ya pili katika mashindano hayo.

Rekodi hiyo inamweka Kelvin katika nafasi ya kipekee kwenye historia ya CECAFA U-20, kwani hakuna mchezaji mwingine tangu mwaka 2010 aliyefanikiwa kufunga hat-trick katika matoleo mawili tofauti ya michuano hiyo.

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga Aalborg ya Denmark kiwango bora alichoonyesha kwenye mashindano hayo ndio kilimpa fursa ya kuonekana kimataifa na kutabiriwa kuja kufanya makubwa baadae.

KEL 02

Sasa inasubiriwa kama rekodi hiyo itafikiwa au kuvunjwa katika michuano ya mwaka huu baada ya alichokifanya Kelvin ambaye msimu wa 2022/23 alisajiliwa Genk ya Ubelgiji klabu ambayo aliwahi kukipiga nahodha wa Tanzania, Mwabana Samatta.


KELV 03

REKODI YA LOKALE TISHIO CECAFA U-20

MSHAMBULIAJI wa Kenya, Sydney Lokale ana rekodi ya kipekee katika historia ya soka la vijana Afrika Mashariki baada ya kuwa mchezaji pekee tangu mwaka 2010 kufunga mabao manne katika mechi moja ya michuano ya CECAFA U-20.

Mshambuliaji huyo wa Kenya aliweka rekodi hiyo mwaka 2019, wakati Kenya ilipoichapa Zanzibar mabao 5-0 katika mashindano hayo, katika dakika ya 33, 38, 71 na 80.

Lokale amewahi kuzichezea klabu kadhaa ikiwemo Kariobangi Sharks, KCB FC na AFC Leopards za Kenya, pamoja na HIFK ya Finland na FC Saint Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Rekodi hiyo inamfanya Lokale kuwa mmoja wa wachezaji walioacha alama kubwa katika historia ya michuano hiyo, hasa kutokana na idadi ya mabao aliyofunga katika mechi moja.

Kwenye michuano hii je kuna mshambuliaji atavunja rekodi ya mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga St Eloi Lupopo.