Rodri: Barcelona haina ubavu UEFA
Muktasari:
- Kwa mujibu wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania, siyo lazima timu bora zaidi ndiyo itakayoshinda Ligi ya Mabingwa, kwa kuwa mashindano hayo mara nyingi huamuliwa na matukio na nyakati muhimu katika michezo.
BARCELONA, HISPANIA; KIUNGO wa Barcelona, Rodrigo Hernández Cascante maarufu Rodri amesisitiza kuwa timu hiyo siyo miongoni mwa zile zinazotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Kwa mujibu wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania, siyo lazima timu bora zaidi ndiyo itakayoshinda Ligi ya Mabingwa, kwa kuwa mashindano hayo mara nyingi huamuliwa na matukio na nyakati muhimu katika michezo.
“Siifikirii Barcelona kuwa ndiyo timu inayofikiriwa zaidi kushinda Ligi ya Mabingwa. Bila shaka, wachezaji kama mimi tulisajiliwa kwa ajili ya kufikia lengo hilo,” Rodri alisema, kwa mujibu wa Mundo Deportivo.
“Lakini nafikiri Ligi ya Mabingwa siyo lazima ishindwe na timu bora zaidi, bali ni mashindano yanayoamuliwa na matukio na nyakati,” aliongeza.
Rodri alijiunga na Barcelona akitokea Manchester City katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka huu.