Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yaitibulia AC Milan dili la Akanji

TETESI Pict

Muktasari:

  • Staa huyu ambaye pia anawindwa na AC Milan na Crystal Palace ni miongoni kwa wachezaji ambao Man City ipo tayari kuwauza dirisha hili.

TOTTENHAM Hotspur inaongoza katika vita ya kuiwania saini ya beki wa Manchester City, Manuel Akanji, 30, katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Staa huyu ambaye pia anawindwa na AC Milan na Crystal Palace ni miongoni kwa wachezaji ambao Man City ipo tayari kuwauza dirisha hili.

Akanji ambaye alisajiliwa akitokea Borussia Dortmund mwaka 2022, amecheza jumla ya mechi 60 akiwa na timu ya taifa ya  Switzerland.

Awali Milan ndiyo ilionekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumpata fundi huyu baada ya mazungumzo yao na Man City juu ya ada ya uhamisho kwenda vizuri.

Pia, Milan ilikutana na wakala wa Akanji wikiendi iliyopita kujadili masuala ya mshahara na ilionekana kuwa changamoto kidogo kwani beki huyo anahitaji mshahara sawa na ule ambao anaupokea kwa sasa wa Euro 5 milioni kwa mwaka akiwa na Man City.

Spurs imeonyesha kuwa tayari kulipa kiasi hicho cha pesa jambo ambalo linaanza kutia ugumu kwa Milan ambayo inaona pesa hiyo ni nyingi. Mkataba wa sasa wa Akanji unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Rodrygo

REAL Madrid imethibitisha winga wao raia wa Brazil, Rodrygo, 24,  ataendelea kubaki Bernabeu msimu huu licha ya kuwindwa na timu mbalimbali Ulaya dirisha hili zikiwamo Liverpool na Arsenal. Rodrygo amecheza zaidi ya mechi 200 na kufunga mabao 54 tangu alipojiunga Madrid mwaka 2019 na alihusishwa kutaka kuondoka dirisha hili kwa sababu hakuwa anaona kama atapata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza chini ya kocha mpya Xabi Alonso.


Fermin Lopez

BARCELONA kupitia kocha wao Hansi Flick, imethibitisha kiungo wao mshambuliaji, Fermin Lopez, 22, ambaye amecheza mechi mbili akiwa na timu ya taifa ya Hispania, hataondoka dirisha hili la usajili licha ya kuhusishwa na Chelsea ambayo inadaiwa kuwa tayari kulipa takribani Euro 90 milioni ili kumsajili. Lopez ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Barca na mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Fabio Vieira

WEST Ham United imeingia katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo fundi kutoka Ureno anayeichezea Arsenal, Fabio Vieira, 25.

Staa huyu pia anawindwa na Stuttgart na klabu nyingine kubwa ya Bundesliga. Vieira alijiunga na Arsenal mwaka 2022 akitokea FC Porto kwa Euro 35 milioni lakini anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Arsenal.

Tangu atue hajafikisha hata mechi 40 za Ligi Kuu England.



Noussair Mazraoui

JUVENTUS inataka kumsajili beki wa kimataifa wa Morocco, Noussair Mazraoui, 27, ambaye kwa sasa anaichezea Manchester United. Mazraoui alisajiliwa na Man United mwaka jana akitokea  Bayern Munich alikoshinda taji la Bundesliga mara mbili. Staa huyu pia alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kilichofika nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022.


Harvey Elliott

RB Leipzig inataka kumsajilj kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya England kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21, Harvey Elliott, 22, kama mbadala wa Xavi Simons aliyetimkia Tottenham. Hata hivyo, Leipzig haiko tayari kulipa dau kubwa la ada ya uhamisho inayohitajika na Liverpool. Liverpool inahitaji takribani Pauni 40 milioni ili kumuuza staa huyo.


Bilal El Khannouss

LEEDS United inamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Morocco, Bilal El Khannouss, 23, kutoka Leicester City, baada ya dili lao la kumsajili Facundo Buonanotte wa Brighton kufeli. El Khannouss aling’ara akiwa Genk kabla ya kuhamia Leicester. Alikuwa sehemu ya kikosi cha Morocco kilichocheza AFCON 2023. Leeds inaamini itampata fundi huyu kwa sababu anahitaji kucheza Ligi Kuu England msimu huu.


Enzo Boyomo

TAARIFA zinaeleza Aston Villa inamnyemelea beki wa kati wa Osasuna na timu ya taifa ya Cameroon, Enzo Boyomo, 23, ambaye inataka kumsajili kwa dau la takribani Pauni 21.25 milioni. Kocha Unai Emery anataka kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi ya Villa kwa ajili ya kuhakikisha anafanya vizuri katika michuano ya ndani na kimataifa msimu huu. Mkataba wa Boyomo unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, msimu uliopita alicheza mechi 40 za michuano yote.


Lucas Paqueta

ASTON Villa inafanya mazungumzo na West Ham ili kumsajili kwa mkopo kiungo wa timu hiyo na Brazil, Lucas Paqueta, dirisha hili. Vyanzo vimeiambia BBC Sport Villa inataka kumsajili staa huyo kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua mazima kwa Pauni 50 milioni mwisho wa msimu huu, ikiwa itaridhishwa na kiwango chake.

Mkataba wa Paqueta na Villa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.