Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs, Arsenal bado zina jambo na Victor Osimhen

Muktasari:

  • Wiki mbili zilizopita Spurs iliwasilisha ofa ya awali yenye thamani ya Pauni 55 milioni kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji huyo. Hata hivyo, mabingwa hao wa Uturuki walitaka Pauni 65 milioni ili kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 27.

ARSENAL na Tottenham Hotspur zimeanza kupigana vikumbo kuhakikisha kwamba zinamg’oa straika wa kimataifa wa Nigeria, Victor Osimhen katika kikosi cha Galatasaray ya Uturuki.

Wiki mbili zilizopita Spurs iliwasilisha ofa ya awali yenye thamani ya Pauni 55 milioni kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji huyo. Hata hivyo, mabingwa hao wa Uturuki walitaka Pauni 65 milioni ili kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 27.

Na kuanzia juzi Arsenal inadaiwa kufanya mazungumzo na kambi ya mchezaji huyo ambaye aliachana na Napoli msimu uliopita na kutua Galatasaray alikocheza awali kwa mkopo msimu mmoja,.

Osimhen  amekuwa akiwindwa na timu mbalimbali Ulaya na Saudi Arabia ambako wachezaji wengi wamekuwa wakikimbilia karibuni.

Katika msimu uliopita mchezaji huyo alifunga mabao 21 na asisti 11 katika mashindano yote ya ndani na nje ya Uturuki, lakini anadaiwa kwamba tangu alipotua nchini humo hana furaha, hivyo ofa yoyote nono itakayomwezesha kutimka inaweza kupokewa kwa mikono miwili na kambi inayomsimamia.

Tangu kuanza dirisha la usajili msimu ujao anadaiwa kupokea ofa zaidi ya tano.


Ibrahim Mbaye

MSHAMBULIAJI wa PSG, Ibrahim Mbaye, amepewa nafasi ya kujiunga na Liverpool au Manchester City baada ya mawakala wake kueleza kuwa hatajiunga na Aston Villa msimu huu ambako anaamini kwamba siyo sehemu sahihi kwake kwani huenda akakumbana na ushindani mkali wa namba. Mbaye, 18, ni mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal ambaye amekuwa akisugua sana benchi PSG


Joshua Zirkzee

MANCHESTER United inadaiwa kuingia kwenye mazungumzo ya hatua za juu ya kumpeleka kwa mkopo mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, katika kikosi cha Juventus msimu mmoja. Inadaiwa kwamba iwapo itakamilika mkataba unatarajiwa kuwa na kipengele cha kumuuza moja kwa moja kwa thamani ya Pauni milioni 30.


Jacobo Ramon

REAL Madrid hawajafanya uamuzi wa kutumia kipengele cha kumnunua beki wao wa zamani Mhispania Jacobo Ramon, 21, ambaye kwa sasa anaichezea Como ya Italia. Kutokuwa na uhakika kwa Madrid kunaweza kuipa Chelsea nafasi ya kuingia kwenye mbio za kumsajili beki huyo. Jacobo alitokea Madrid wakati anatua Como na mkataba wake una kipengele ambacho kinaipa nafasi kumsajili tena.


Jack Grealish

ATLETICO Madrid inafikiria kufanya uhamisho wa winga wa England na Manchester City, Jack Grealish ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika kikosi cha Everton. Mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 30 pia anawindwa na Everton pamoja na klabu yake ya zamani, Aston Villa.


Ruben Vargas

SEVILLA imetangaza bei ya Ruben Vargas ambaye iko tayari kumuuza kwa Euro milioni 20, sawa na takribani Pauni milioni 17 kutokana na utitiri wa timu zinazomtaka huko Ulaya. Brighton, Newcastle United na Aston Villa ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu England zinazovutiwa na winga huyo wa kimataifa wa Uswisi mwenye umri wa miaka 22.


Raphael Le Guen

CRYSTAL Palace inadaiwa kufikia makubaliano binafsi na beki wa kati wa Brest, Raphael Le Guen, ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 19 anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho baada ya mazungumzo kufikia hatua nzuri. Kinachoelezwa kwa sasa ni kwamba pande mbili, yaani mchezaji na Palace wanakamilisha makubaliano ya kimkataba.


Cody Gakpo

TOTTENHAM Hotspur imefanya mazungumzo mazuri na mshambuliaji wa Liverpool na Uholanzi, Cody Gakpo, lakini Liverpool haina mpango wowote wa kumuuza nyota huyo mwenye umri wa miaka 26. Katika dili hilo, Spurs imewasilisha mpango wake wa miaka mitatu mezani kwa Gakpo kwa ajili ya kusoma na kuuelewa kabla hajafanya uamuzi.


Mohamed-Ali Cho

HULL City inadaiwa kuwa karibu kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Nice, Mohamed-Ali Cho kwa ada ya takribani Pauni 17 milioni ambapo nyota huyo wa kimataifa wa Mfaransa mwenye umri wa miaka 22 atasaini kuitumikia kwa miaka mitano. Hata hivyo, pande mbili zingali zinajadiliana juu ya vipengele vingine muhimu.


Manuel Locatelli

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, anatajwa kuwa na nia ya kumsajili kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Italia, Manuel Locatelli, 28, katika dirisha hili. De Zerbi anaamini Locatelli anaweza kuwa nyongeza muhimu katika mfumo, hivyo amemjumuisha katika orodha ya mastaa anaowataka. De Zerbi anapambana kuhakikisha Spurs inafanya vizuri msimu huu.