Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shoo Madonna, Shakira, wawasha moto, Gaucho, Ronaldo bonge ‘Suprise’

SHOO Pict

Muktasari:

  • Tamasha hilo lililofanyika wakati wa mapumziko ya mchezo kati ya Hispania na Argentina katika Uwanja wa New York New Jersey, lilidumu kwa dakika 27 na sekunde 22, na kuwa mapumziko marefu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Kombe la Dunia.

NEW YORK, MAREKANI: Tamasha la mapumziko la fainali ya Kombe la Dunia 2026 limeandika historia baada ya kuwakutanisha mastaa wakubwa wa muziki duniani akiwemo Madonna, Shakira, Justin Bieber na BTS, huku magwiji wa soka Ronaldinho na Ronaldo wakitoa sapraizi iliyowasisimua maelfu ya mashabiki.

Tamasha hilo lililofanyika wakati wa mapumziko ya mchezo kati ya Hispania na Argentina katika Uwanja wa New York New Jersey, lilidumu kwa dakika 27 na sekunde 22, na kuwa mapumziko marefu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Kombe la Dunia.

Madonna ndiye aliyefungua pazia kwa kutumbuiza wimbo wake maarufu Music, akitokea chini ya jukwaa akiwa ndani ya gari lililoendeshwa na gwiji wa Brazil, Ronaldo Nazario, huku Ronaldinho akiwa ameketi upande wa abiria.

SHO 04

Ronaldo aendesha gari

Katika mwanzo wa onyesho la Madonna, Ronaldo mwenye umri wa miaka 49 alikuwa nyuma ya usukani wa gari lililombeba mwanamuziki huyo huku akiimba wimbo wake maarufu Music.

Pembeni yake alikuwapo Ronaldinho, ambaye aliketi kwenye kiti cha abiria.

Baada ya gari kusimama katikati ya uwanja wa New York New Jersey, wawili hao walishuka na kusimama pamoja na Madonna kabla ya tamasha kuendelea.

Tukio hilo liliwashangaza mashabiki wengi waliojaa uwanjani na mamilioni waliokuwa wakifuatilia kupitia televisheni.

SHO 03

Mitandao yalipuka

Baada ya picha hizo kusambaa, mashabiki walifurika kwenye mitandao ya kijamii wakieleza mshangao wao.

Mmoja aliandika:”Ronaldinho, Ronaldo na Madonna... nini kinaendelea hapa?”

Mwingine alisema:”Ronaldo na Ronaldinho wakimpeleka Madonna kwenye shoo ya mapumziko ya Kombe la Dunia... Hili sikulitegemea kabisa.”


Shabiki mwingine aliandika:

“Kombe hili la Dunia limekuwa la kichaa. Hili la Ronaldinho na Ronaldo kumuingiza Madonna uwanjani halikutarajiwa kabisa.”

Mwingine alitania:”Kweli hawa Ronaldinho na Ronaldo wanaendesha gari? Hii ni filamu au nini?”

Naye mwingine alieleza:”Huenda hii ikawa moja ya picha bora zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya soka. Ronaldinho na Ronaldo wakimleta Madonna kwenye jukwaa la Kombe la Dunia.”


Ronaldo amzawadia Trump

Mbali na kushiriki kwenye tamasha hilo, Ronaldo pia alizua mjadala wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo.

Nyota huyo wa zamani wa Brazil alionekana akimpa Rais wa Marekani, Donald Trump, nafasi ya kuligusa Kombe la Dunia kabla ya mchezo kuendelea.

Picha za tukio hilo zilipoonyeshwa kwenye runinga, baadhi ya mashabiki walionyesha kutoridhishwa nazo kupitia mitandao ya kijamii.

Licha ya mjadala huo, ushiriki wa Ronaldinho na Ronaldo kwenye shoo ya mapumziko uliibuka kuwa moja ya matukio yaliyovuta hisia zaidi katika fainali ya Kombe la Dunia 2026, tamasha ambalo lilichanganya soka, muziki na burudani kwa kiwango kisichowahi kushuhudiwa.

SHO 01

Shakira na BTS wang’ara

Nyota wa Colombia, Shakira, aliungana tena jukwaani na mwanamuziki wa Nigeria, Burna Boy, baada ya wawili hao pia kutumbuiza kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia jijini Mexico City mwezi uliopita.

Kundi maarufu la K-Pop, BTS, nalo lilifanya maonyesho yake ya kwanza makubwa baada ya kurejea kutoka mapumziko ya miaka mitatu yaliyotokana na wanachama wake kutimiza huduma ya lazima ya kijeshi nchini Korea Kusini.

Justin Bieber naye aliwavutia mashabiki kwa uimbaji wake, huku tamasha hilo likikamilishwa na maonyesho ya mastaa wengine wakiwemo Nicole Scherzinger, Robbie Williams, Laura Pausini na Post Malone aliyepanda jukwaani kuimba wimbo wake maarufu Wow.

SHO 02

Tom Cruise atoa ujumbe

Kabla ya mchezo kuanza, mwimbaji na mwigizaji Jennifer Hudson aliimba wimbo wa taifa wa Marekani akiongozana na bendi ya moja kwa moja.

Baada ya hapo, mwigizaji maarufu wa Hollywood, Tom Cruise, aliingia uwanjani na kutoa hotuba ya kuhamasisha mashabiki.

“Kutoka kila kona ya dunia tumeshuhudia ubora na kushiriki nyakati za furaha. Soka ni lugha inayozungumza bila maneno, ni nguvu inayowaunganisha watu,” alisema Cruise.

Mwimbaji wa Italia, Laura Pausini, alisema alipata msisimko mkubwa baada ya Robbie Williams kumwalika kutumbuiza naye kwenye tamasha hilo.

SHO 05

Mapumziko yazua mjadala

Licha ya kuvutia mashabiki wengi, muda wa tamasha hilo uliibua mjadala mkubwa.

Kanuni za Bodi ya Kimataifa ya Sheria za Soka (IFAB) zinaeleza kuwa mapumziko ya kawaida ya mechi yanapaswa yasizidi dakika 15, lakini safari hii yaliongezwa hadi zaidi ya dakika 27 ili kutoa nafasi kwa tamasha hilo.

Mshambuliaji wa zamani wa England, Wayne Rooney, ambaye alikuwa mchambuzi wa BBC wakati wa fainali hiyo, hakufurahishwa na maonyesho hayo.

“Ninawapenda wengi wa wasanii waliotumbuiza, lakini kwa maoni yangu tamasha hilo halikuwa zuri kabisa,” alisema Rooney.

Licha ya maoni hayo tofauti, shoo ya mapumziko ya Kombe la Dunia 2026 imeingia kwenye historia kama moja ya matamasha makubwa zaidi kuwahi kufanyika kwenye fainali ya mashindano hayo.