Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shabiki adai... Ukiwa na Osimhen unaongoza 1-0

SHABIKI Pict

Muktasari:

  • Shabiki huyo alifika katika kambi ya Super Eagles wakati wa AFCON 2025 kuonyesha sapoti yake kwa mshambuliaji nyota wa Nigeria.

RABAT, MOROCCO: SHABIKI wa kutupwa wa Galatasaray amepeleka mapenzi yake kwa mshambuliaji wa Super Eagles, Victor Osimhen, nje ya mipaka ya Istanbul, imeripotiwa.

Shabiki huyo alifika katika kambi ya Super Eagles wakati wa AFCON 2025 kuonyesha sapoti yake kwa mshambuliaji nyota wa Nigeria.

Shabiki huyo mwenye shauku kubwa, aliyetambulika kwa jina la Hussein na Soccernet.ng, alisafiri kutoka Ulaya kufuatilia safari ya Osimhen katika mashindano hayo yanayoendelea Morocco.

Akizungumza pembeni mwa mazoezi ya Super Eagles, Hussein alishindwa kueleza kwa maneno mapenzi yake kwa Osimhen. Alimuelezea mshambuliaji huyo wa zamani wa Napoli kama mchezaji wa kipekee sana katika soka la kisasa.

Kwa mujibu wake, mvuto wa Osimhen hauishii kwenye mabao pekee, bali unatokana na njaa yake ya mafanikio na haiba yake ya kipekee.

“Yeye ni wa aina yake. Ni wa kipekee, mnyenyekevu, mkamilifu ndiyo maana tunampenda,”€  amesema Hussein.

Aliongeza kuwa Osimhen aliziba pengo kubwa la kihisia kwa mashabiki wa Galatasaray baada ya majeraha ya Mauro Icardi.

Hussein alisisitiza kuwa mchango wa Osimhen huonekana mara moja kila anapokanyaga uwanja, iwe ni Italia, Uturuki au katika jukwaa la AFCON akiwa na Nigeria.

Alidai kuwa timu pinzani tayari huingia kwenye presha kubwa pindi tu wanapojua Osimhen yupo uwanjani.

“Kama una Osimhen, tayari unaongoza 1-0,”€  amesema. “Anasukumiza timu mbele. Daima anataka zaidi. Anaweza kufunga mabao 10 na bado anataka la 11. Hakuna wa kumzuia.”€

Shabiki huyo wa Galatasaray alifichua kuwa tayari alimwona Osimhen katika hoteli ya timu na hata alialikwa binafsi kuhudhuria mazoezi ya Super Eagles, akiwa na matumaini ya kukutana tena na mshambuliaji huyo na kupiga naye picha baada ya mazoezi. Osimhen alitarajia kuwapo uwanjani Jumanne wakati Nigeria ilipocheza mechi ya mwisho ya Kundi C la Afcon 2025 dhidi ya Uganda.