Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Seth Curry afungua milango ya kubaki Warriors

CURRY Pict

Muktasari:

  • Seth, ambaye ni mdogo wa nyota wa Warriors, Stephen Curry amesema msimu uliopita haukuwa mzuri kwake kutokana na kusumbuliwa na majeraha yaliyomfanya kucheza mechi 10 pekee, lakini bado ana mapenzi makubwa na klabu hiyo.

SAN FRANCISCO, MAREKANI: Seth Curry amesema yupo tayari kuendelea kuitumikia Golden State Warriors ikiwa pande zote zitafikia makubaliano katika kipindi hiki cha usajili wa wachezaji huru (free agency).

Seth, ambaye ni mdogo wa nyota wa Warriors, Stephen Curry amesema msimu uliopita haukuwa mzuri kwake kutokana na kusumbuliwa na majeraha yaliyomfanya kucheza mechi 10 pekee, lakini bado ana mapenzi makubwa na klabu hiyo.

Akizungumza katika mashindano ya American Century Championship yaliyofanyika South Lake Tahoe, Curry amesema kwa sasa kipaumbele chake ni kurejea katika utimamu wa asilimia 100 kabla ya kufanya uamuzi kuhusu hatua inayofuata katika maisha yake ya soka la kikapu.

“Ninajaribu kwanza kuwa fiti kabisa kisha nione kitakachotokea Julai na Agosti katika soko la wachezaji huru. Kuna mabadiliko mengi yanayoendelea kwenye ligi, hivyo ninatafuta mazingira bora zaidi kwa ajili yangu,” amesema.

CUR 01

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Warriors Desemba mwaka jana, lakini yeye na kaka yake Steph waliweza kucheza pamoja mechi tatu tu za msimu wa kawaida kutokana na majeraha yaliyowakabili wote wawili.

Alipoulizwa kama angekubali kurejea Warriors, Seth hakusita kujibu.

“Bila shaka. Sikupata nafasi ya kufanya kila nilichotaka uwanjani msimu uliopita, lakini nina heshima kubwa kwa klabu hii na mashabiki wake. Ni sehemu yenye mazingira ya kiwango cha juu,” amesema.

Licha ya kucheza mechi chache, Seth alionyesha uwezo wake wa kupiga mashuti ya mbali. Katika mechi yake ya kwanza msimu uliopita alifunga pointi 14 kwa usahihi mkubwa wa upigaji, huku akimaliza msimu akiwa amefunga mashuti 12 kati ya 25 ya alama tatu.

CUR 02

Kwa sasa Seth ni mchezaji huru, huku mustakabali wake ukiendelea kuwa gumzo. Amesema hatafikiria sana kuhusu muda uliobaki katika taaluma yake, akisisitiza ataendelea kufanya maamuzi msimu kwa msimu.

“Nimecheza NBA kwa miaka 13. Nilipoingia nilikuwa na ndoto ya kucheza angalau miaka 10. Nilianzia bila kuchaguliwa kwenye Draft na nililazimika kupambana kwa kila hatua. Sijaridhika kabisa, lakini ninajivunia nilichofanikisha. Sasa nitaangalia kila msimu mmoja baada ya mwingine, hasa unapokumbwa na majeraha kama haya,” amesema.

Warriors sasa wanasubiri kuona kama watafikia makubaliano mapya na Seth kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa NBA.