Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sasa Basi! Game 7 kuamua Mfalme wa NBA 2025

NBA Pict

Muktasari:

  • Ni Oklahoma City Thunder ambao ni wenyeji na Indiana Pacers wanakutana kwa ajili ya mechi ya saba ‘Game 7’ ya Fainali za NBA 2025  ikiwa ni mechi ya mwisho ya kuamua bingwa wa msimu huu.

OKLAHOMA CITY: WAKATI mshale wa saa ukielekea kesho, Jumatatu saa 3:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki, macho na masikio ya wapenzi wa mpira wa kikapu yataelekezwa  kwenye Uwanja wa Paycom Center katika jimbo la Oklahoma, nchini Marekani.

Ni Oklahoma City Thunder ambao ni wenyeji na Indiana Pacers wanakutana kwa ajili ya mechi ya saba ‘Game 7’ ya Fainali za NBA 2025  ikiwa ni mechi ya mwisho ya kuamua bingwa wa msimu huu.

Hii ni mara ya nane katika miaka 45 fainali za NBA kupelekwa Game 7 jambo linalodhihirisha ukubwa na ugumu wa safari ya msimu huu.

Kwa Thunder ni nafasi ya kuthibitisha ubora msimu huu. Kwa Pacers ni ndoto ya ‘Cinderella’ kuandika historia kuwa bingwa wa kwanza kutoka Mashariki tangu Milwaukee Bucks 2021.

NB 01

“Hii ni mechi ya maisha yetu,” alisema Timothy McConnell aliyekuwa shujaa wa Pacers katika Game 6.

“Tuna nafasi moja ya kubadilisha maisha yetu na historia ya klabu zetu.”

Kwa Thunder mvua ya ushindi itakamilika? Oklahoma City Thunder ilimaliza msimu wa kawaida na ushindi wa mechi 68 ikiwa na recodi ya 40-1 dhidi ya timu za ukanda wa Mashariki - kiwango ambacho kilionyesha ubora wa safu za ya ulinzi na mashambulizi. Kwa mujibu wa  takwimu za NBA, ilikuwa na tofauti ya wastani ya pointi +10.7 - kiwango bora zaidi tangu Warriors ilipofanya hivyo 2016.

NB 02

Mchezaji  wake wa kiwango cha juu, Shai Gilgeous-Alexander alitwaa tuzo ya Kia MVP 2025 akiwa na wastani wa pointi kwa mchezo 30.4, asisti 6.9, rebaundi 5.8 akiongoza pia kwa dakika bora (36.7) kwa kila mechi.

Katika fainali hizo, Shai amecheza Game 6 chini ya kiwango, lakini katika mechi nne nyingine alifunga zaidi ya pointi 30 akiibeba timu na kusababisha ushindi katika Game 4 na 5.

“Wamepambana mwaka mzima, lakini sasa ni dakika 48 tu zinazoamua kila kitu,” alisema Kocha Mark Daigneault wa Thunder.

NB 03

Kutoka kuzomewa hadi Game 7

Indiana Pacers ilikuja kama ‘underdogs’ msimu huu. Ilikuwa na rekodi ya 47-35 msimu wa kawaida, lakini  iliamka tangu mwaka mpya ikiwa na rekodi bora zaidi ukanda wa  Mashariki baada ya Januari Mosi.

Ikiwa chini ya Kocha Rick Carlisle iliwatoa Boston Celtics (mabingwa wa Mashariki), Bucks, na Knicks kwa mfululizo bora kabla ya kuingia fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000.

NB 04

Mchezaji wake nyota, Tyrese Haliburton, licha ya kuuguza jeraha la mshipa wa nyuma wa mguu ameonyesha uongozi bora akifunga wastani wa pointi 21.3 kwa mechi, huku akitoa asisti 8.6 kwa mchezo katika fainali hizo.

“Tunajua tunachopigania. Tunataka taji. Tunataka historia,” alisema Haliburton.

Katika Game 6, Pacers  ilitumia nguvu ya benchi lake kwa kiwango kikubwa. T.J. McConnell alitoa pointi 18, akiiba mipira mara 4, Bennedict Mathurin alifunga pointi 15, Obi Toppin na Caruso waliongeza pointi muhimu katika robo  ya mwisho.

NB 05

NGUVU YA BENCHI

Katika kila mechi sita za fainali hizo, timu iliyoongoza kwa pointi kutoka benchi ilishinda mchezo husika.

Kwa mfano katika mechi ya tatu ‘Game 3’, Bennedict Mathurin alifunga pointi 27 katika dakika 22 akiibeba Pacers. Kwa mechi ya tano ‘Game 5’ Cason Wallace wa Thunder alifunga pointi 1 muhimu kutokea benchi.

Katika mechi ya sita ‘Game 6’ Caruso na McConnell walimzima Shai, wakiisaidia Pacers kusawazisha mfululizo na kuwa 3-3.

Kwa mujibu wa ESPN, Pacers ina wastani wa utupiaji pointi 38.1 kutoka benchi kwa kila mchezo mmoja, huku Thunder ikitoa na wastani wa 33.4 tofauti ikiwa ni ndogo, lakini muhimu wakati timu hizo zinakwenda kukutana katika Game 7 ili kuamua mbabe wa NBA 2025.