Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saddig Bey avuna mabilioni NBA

NBA Pict

Muktasari:

  • Mkataba pia una kipengele kinachoweza kumpa Bey bonasi ya hadi asilimia 15 ya mshahara wake uliobaki endapo Pelicans watamuuza timu nyingine.

NEW ORLEANS, MAREKANI: NYOTA wa kikapu wa New Orleans Pelicans, Saddiq Bey, amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya dola milioni 56 (Sh.144 bilioni), utakaomuweka kwenye timu hiyo hadi msimu wa 2029-30.

Mkataba pia una kipengele kinachoweza kumpa Bey bonasi ya hadi asilimia 15 ya mshahara wake uliobaki endapo Pelicans watamuuza timu nyingine.

Bey, mwenye umri wa miaka 27, amepata mkataba huo baada ya kuonyesha kiwango bora msimu uliopita, akicheza michezo 72 na kuanza katika michezo 64.

NB 01

Katika msimu huo, ameweka wastani wa pointi 17.7 kwa mchezo, huku akidaka mipira 5.6 iliyopigwa na kukosa na kutoa pasi 2.5 zilizozaa pointi kwa kila mchezo. Wastani huo wa pointi ulikuwa rekodi yake bora tangu aanze kucheza NBA.

Mafanikio hayo yamekuwa muhimu zaidi kutokana na historia yake ya majeraha. Bey alikosa msimu mzima wa 2024-25 baada ya kuumia goti akiwa na Atlanta Hawks, Machi 2024.

Baada ya kupona, alijiunga na Pelicans na kurejea uwanjani akiwa katika kiwango kilichomfanya timu hiyo kuamua kumlinda kwa kumpa mkataba wa muda mrefu.

NB 02

Katika msimu wake wa kwanza New Orleans, Bey pia alifunga pointi 42 dhidi ya Utah Jazz, ikiwa ni moja kati ya michezo yake yenye pointi nyingi zaidi katika NBA. Pia alifunga pointi 36 dhidi ya Memphis Grizzlies na 34 dhidi ya Philadelphia 76ers.

Bey alianza safari yake NBA mwaka 2020, baada ya kuchaguliwa katika nafasi ya 19 kwenye usaili wa wachezaji wapya na Brooklyn Nets, kabla ya kuhamia Detroit Pistons.

NB 03

Kisha  akazichezea Atlanta Hawks na Washington Wizards, kabla ya kutua New Orleans kupitia uhamisho wa timu tatu mwaka 2025.

Kwa sasa, mkataba huo mpya unamfanya Bey kuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu ya Pelicans, ambao wanatarajia kuendelea kujenga kikosi chao kuelekea msimu mpya wa NBA utakaoanza Oktoba 20, 2026.