Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruben Amorim hana amani Man United, Sunderland yashika hatima yake

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Amorim raia wa Ureno, anakabiliwa na shinikizo kubwa la kuondoka klabuni hapo, kufuatia mashabiki na baadhi ya viongozi kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi cha Man United, ambacho kimeshindwa kurejea kwenye hali ya ushindani kwenye mechi za Ligi ya England kama ilivyokua miaka ya nyuma.

KOCHA wa Man United, Ruben Amorim amekiri yupo kwenye wakati mgumu, na huenda akapoteza kazi kama atapata matokeo mabaya kwenye mechi ya leo dhidi ya Sunderland.

Amorim raia wa Ureno, anakabiliwa na shinikizo kubwa la kuondoka klabuni hapo, kufuatia mashabiki na baadhi ya viongozi kutoridhishwa na mwenendo wa kikosi cha Man United, ambacho kimeshindwa kurejea kwenye hali ya ushindani kwenye mechi za Ligi ya England kama ilivyokua miaka ya nyuma.

Vyanzo kutoka ndani ya klabu ya Man United vinasisitiza kuwa Amorim bado anaungwa mkono na baadhi ya viongozi, huku wengine wakishinikiza aondolewe na kuletwa kocha mwingine, lakini yeye binafsi anaamini ana nafasi finyu kuendelea kubaki klabuni hapo kama mambo yataendelea kuwa vibaya kuanzia mchezo wa leo wa Premier.

Taarifa nyingine zinadai kuwa, baadhi ya viongozi wanaompinga Amorim wameanza kushinikiza kutafutwa makocha ambao wanaweza kuchukua nafasi ya kocha huyo ambaye ameshinda mechi tisa tu za ligi katika kipindi chake cha miezi 11.

AMO 02

Alipoulizwa kama amepata hakikisho lolote kutoka kwa mabosi wake, Amorim amesema: “Sijali kuhusu hilo na hakuna mtu hapa ambaye ni mjinga. Tunajua tunahitaji matokeo ili kuendeleza mambo mazuri hapa klabuni.

"Tutafikia hatua ambayo hali itakuwa ngumu kwa kila mtu, kwa sababu hii ni klabu kubwa sana yenye wadhamini wengi, na wamiliki wawili. Kwa hiyo ni kazi ngumu inayonikabili kwa sasa. Ikishindikana ninaweza kuondoka.”

Baada ya kichapo cha 3-1 wiki iliyopita dhidi ya Brentford, Amorim amevuna alama 34 tu kutoka kwenye mechi 33 tangu akiwa kocha wa Man United.

Japo ana wasiwasi wa kupoteza kibarua chake, Amorim amesisitiza kuwa mwenye uamuzi wa mwisho wa kumuondoka klabuni hapo ni bodi ya Man United, ambayo ina mamlaka ya kutoa kauli ya kubaki ama kuondoka kwake.

Hata hivyo kocha huyo wa zamani wa Sporting, amewataka wachezaji wake kujibu kwa vitendo uwanjani ili kupata ushindi muhimu kwenye mechi ya leo.

Pia ameendelea kusisitiza kuwa, hana mpango wowote wa kubadili mfumo wake wa 3-4-3 anaouamini.

Amorim amesema: “Siyo wakati wa kusema, ni wakati wa kuonyesha kwa vitendo uwanjani. Ninataka kuona timu yangu ikishinda au ikipoteza, lakini ikicheza kwa mtindo ule ule, kitu ambacho hatufanyi kwa sasa.

AMO 01

"Tatizo langu kubwa ni kwa wachezaji wangu kuanza kuamini nyinyi mnaposema kuwa tatizo letu ni mfumo wa uchezaji. Hilo linaniumiza sana kichwa.

"Naweza kuwaonyesha jinsi tunavyocheza kwa mifumo tofauti. Kutoshinda au kushindwa kunaniumiza zaidi.”

Wakati huohuo, wachezaji wa Man United watavaa vitambaa vyeusi mkononi na watashiriki dakika moja ya ukimya kabla ya mechi ya leo dhidi ya Sunderland, ili kuonyesha heshima kwa wahanga wa shambulio la sinagogi lililotokea wiki hii huko Manchester.