Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RONALDO TIME : Saa 12 za mkanganyiko za Ronaldo juzi

Cristiano Ronaldo.

Muktasari:

Ilianza asubuhi. Ilikuwa hivi. Juzi asubuhi Ronaldo alimpora kipaza sauti mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha CMTV cha kwao Ureno na kukitupa mtoni wakati wachezaji wa Ureno walipokwenda kupunga upepo kando ya mto huo ulio katika Jiji la Lyon.

ITS Cristiano Ronaldo time. Baada ya kuwa kimya, akionekana amedorora na kuanza kudharauliwa, sasa muda wake ndio huu. Amerudi tena kivingine na kwa nyodo zake za ndani na nje ya uwanja. Siku yake ya juzi ilikuwa ndefu kweli kweli.

Ilianza asubuhi. Ilikuwa hivi. Juzi asubuhi Ronaldo alimpora kipaza sauti mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha CMTV cha kwao Ureno na kukitupa mtoni wakati wachezaji wa Ureno walipokwenda kupunga upepo kando ya mto huo ulio katika Jiji la Lyon.

Baadaye ilidaiwa kwamba Ronaldo hakuwa amekerwa na swali lolote kutoka kwa mwandishi huyo isipokuwa ana uhusiano mbovu na kituo hicho ambacho inasemekana kimekuwa kikimfuatafuata sana katika maisha yake binafsi na kutangaza mabaya mengi juu yake.

Jioni, Ronaldo alitupia mabao mawili murua katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Hungary katika pambano kali ambalo nusura Ureno itupwe nje ya michuano baada ya Hungary kuongoza mara tatu katika pambano hilo.

Bao jingine la Ureno lilifungwa na staa mwenzake wa zamani wa Manchester United, Luis Nani aliyepokea pasi murua ya Ronaldo.

Baada ya kufunga mabao mawili na kupika moja, Ronaldo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa pambano hilo. Lakini licha ya kuchaguliwa huko, yeye ni nahodha wa Ureno na alipaswa kuongea na vyombo vya habari baada ya mechi.

Matokeo yake Ronaldo alikacha kuongea na waandishi wa habari huku waandishi hao wakitaarifiwa na Uefa kwamba ni wao Uefa ndio ambao wangemuuliza maswali Ronaldo badala ya waandishi wengine wa kawaida.

Badala yake Uefa ndio ilitoa taarifa ya Ronaldo kwa vyombo vya habari ambapo ilimkariri Ronaldo akisema: “Tumecheza mechi nzuri. Ilishangaza kidogo. Hungary ilikuwa inafunga na Ureno ilikuwa inafunga. Na kulikuwa na joto kali sana.

“Binafsi nilifurahishwa na juhudi za timu. Mara tatu ilibidi tutoke nyuma kwenda kusawazisha. Kwangu ni fahari kutajwa kuwa mchezaji bora wa mechi, lakini dhumuni letu lilikuwa kushinda mechi, hata hivyo tumeshindwa. Kitu cha msingi zaidi tulitaka tufuzu,” alisema Ronaldo kupitia taarifa aliyotolewa na Uefa.

Kuna hisia kwamba Ronaldo na watu wake ndio ambao, walitengeneza zengwe kuhusu taarifa hiyo kupitia Uefa bila ya Ronaldo kuwepo wala kujibu maswali baada ya kitendo chake cha asubuhi kutupa kipaza sauti kwenye mto.

Hata hivyo, kocha wake, Fernando Santos alimtetea na kumsifu staa huyo wa Real Madrid ambaye mechi iliyopita dhidi ya Austria alikosa penalti muhimu huku kiwango chake kikiingia katika shutuma kubwa kwa wachambuzi wa soka na mashabiki.

“Hivi ndivyo Cristiano alivyo. Anahitaji kufunga kwa sababu ni mshindi na mfungaji. Anacheza mbele hapo na huwa amejaa mabao. Nadhani hili litaongeza uwezo wake wa kujiamini. Amepania na anajiamini na hili litaongeza uwezo wake wa kujiamini katika mechi ijayo dhidi ya Croatia,” alisema kocha huyo. Kwa kufunga mabao hayo mawili, Ronaldo amefikisha idadi ya mabao manane tangu aanze kucheza michuano ya Euro na sasa anatazamiwa kuipiku rekodi ya mshambuliaji mahiri wa zamani wa Ufaransa, Michael Platini ambaye ana mabao tisa mpaka sasa.

Staa huyo wa zamani wa Manchester United pia ameingia katika rekodi ya kufunga mabao katika kila michuano aliyoshiriki akianzia michuano ya mwaka 2004 kisha 2008, 2012 na 2016.

Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwanaspoti au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz