Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo, kocha kuna jambo Al nassr

Muktasari:

  • Al Nassr ilifanya ‘comeback’ ya kuvutia kutoka nyuma kwa mabao mawili na kuichapa Al Ettifaq 3-2 Jumanne, lakini Ronaldo hakuwa sehemu ya ushindi huo baada ya kuondolewa kabla ya kuanza kipindi cha pili.

RIYADH, Saudi Arabia. UHUSIANO wa Cristiano Ronaldo na kocha mpya wa Al Nassr, Ange Postecoglou, umeanza kuingia kwenye shaka baada ya matukio ya mchezo wa tatu pekee wa msimu huu.

Al Nassr ilifanya ‘comeback’ ya kuvutia kutoka nyuma kwa mabao mawili na kuichapa Al Ettifaq 3-2 Jumanne, lakini Ronaldo hakuwa sehemu ya ushindi huo baada ya kuondolewa kabla ya kuanza kipindi cha pili.

Ronaldo, ambaye anaripotiwa kulipwa kiasi kikubwa cha Pauni 488,000 kwa siku, alianza mchezo huo kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kurejea kutoka mapumziko ya baada ya Kombe la Dunia.

Hata hivyo, mambo yalianza vibaya kwa mabingwa hao baada ya kipa Bento kupewa kadi nyekundu dakika ya 12 kufuatia kumchezea vibaya kiungo wa zamani wa Fulham, Mousa Dembele, nje ya eneo la hatari baada ya kutoka langoni kujaribu kuokoa hatari.

Al Ettifaq ilitumia faida ya kuwa na mchezaji mmoja zaidi, Ondrej Duda na Alvaro Medran wakifunga mabao yaliyoiwezesha timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Ronaldo, 41, alionekana kukerwa alipokuwa akielekea vyumbani wakati wa mapumziko, akionyesha hasira na kuonekana kuvua kitambaa cha unahodha alipokuwa akipita kwenye njia ya kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo.

Kabla ya kuanza kipindi cha pili, Postecoglou alifanya uamuzi wa kushangaza wa kumtoa Ronaldo, uamuzi ambao baadaye ulionekana kuzaa matunda.

Al Nassr ilianza kurejea mchezoni dakika ya 74 kupitia Sadio Mane, kabla ya beki Abdulelah Al Amri kusawazisha dakika tatu baadaye.

Mane alikamilisha ‘comeback’ hiyo dakika ya 90 kwa kufunga bao lake la pili na kuipa Al Nassr ushindi wa mabao 3-2.

Katika shangwe za baada ya mchezo, Ronaldo hakuonekana kushiriki kwa kiwango kikubwa katika kusherehekea ushindi huo.

Postecoglou, hata hivyo, alikataa kuzungumzia kwa kina uamuzi wake wa kumtoa Ronaldo.

“Nadhani kuna jambo kubwa zaidi la kuzungumzia leo, nalo ni jinsi wachezaji 10 wa Al Nassr walivyokuwa bora. Hilo ndilo jambo pekee mnapaswa kuandika leo; mengine hayana umuhimu,” alisema.

Kocha huyo akaongeza:

“Haijalishi ni timu gani. Ukiwaona wachezaji 10 wakicheza katika mazingira yale kwa muda mrefu, wakiwa nyuma 0-2 na kisha kurejea na kushinda, hilo ndilo jambo la kuzungumzia leo.”


RONALDO AWAHI KUZUNGUKWA NA UTATA

Utata umeonekana kumfuata Ronaldo tangu alipojiunga na Al Nassr Januari 2023, baada ya kuondoka Manchester United kufuatia mgogoro wa wazi na klabu hiyo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Ronaldo aligoma kushiriki baadhi ya shughuli za klabu kutokana na kile alichoamini kuwa Al Nassr haikuwa ikiwekewa nguvu za kutosha kifedha ikilinganishwa na wapinzani wao wa ubingwa, Al Hilal.

Al Nassr na Al Hilal zinamilikiwa kwa kiwango kikubwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF).

Ronaldo aliamini Al Hilal ilikuwa ikipewa upendeleo, huku akikerwa zaidi na usajili wa wachezaji wakubwa katika dirisha la Januari, akiwemo aliyekuwa mchezaji mwenzake Real Madrid, Karim Benzema.

Viongozi wa Saudi Arabia nao walishangazwa na malalamiko ya Ronaldo kutokana na mshahara wake unaokadiriwa kufikia karibu Pauni 500,000 kwa siku.

Licha ya kuwa sura kubwa ya Ligi Kuu Saudi Arabia (SPL), ligi hiyo ilitoa taarifa ikisisitiza kwamba Ronaldo hana mamlaka ya kuamua kinachoendelea kwenye klabu nyingine.

“Ligi Kuu Saudi Arabia imejengwa kwa kanuni rahisi: kila klabu inafanya kazi kwa uhuru chini ya kanuni zilezile,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa kila klabu ina bodi yake, viongozi wake na uongozi wake wa soka, hivyo maamuzi kuhusu usajili, matumizi ya fedha na mikakati yanafanywa na klabu husika ndani ya mfumo wa kifedha unaolenga kuhakikisha ushindani na uendelevu wa ligi.

Ronaldo amekuwa sehemu muhimu ya ukuaji na malengo ya Al Nassr tangu alipowasili, lakini mamlaka ya kuamua masuala ya klabu nyingine hayapo mikononi mwake.

Msimu uliopita, Ronaldo alitwaa ubingwa wake wa kwanza wa ligi akiwa na Al Nassr, akiongeza taji hilo kwenye rekodi yake ndefu ya mafanikio.