Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo hafikirii kuondoka Al Nassr

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 40 alishinda taji lake la tatu akiwa na timu ya taifa kwa kuichapa Hispania kwa mikwaju ya penalti 5-2 baada ya sare ya mabao 2-2 katika dakika 120.

LISBON, URENO: SUPASTAA Cristiano Ronaldo amefunguka juu ya hatima ya soka lake baada ya Ureno kunyakua taji la Nations League usiku wa kuamkia Jumatatu.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 40 alishinda taji lake la tatu akiwa na timu ya taifa kwa kuichapa Hispania kwa mikwaju ya penalti 5-2 baada ya sare ya mabao 2-2 katika dakika 120.

Ronaldo alifunga bao la kusawazisha na kufanya ubao usomeke 2-2 katika mechi hiyo ya fainali iliyofanyika Uwanja wa Allianz Arena, huko Munich, Ujerumani.

Staa huyo wa zamani wa Manchester United, Ronaldo alionekana akimwaga machozi baada ya Ureno kufunga mikwaju yake yote mitano ya penalti na kutetea taji hilo.

Baada ya hapo, Ronaldo alisema: “Haya ni machozi ya furaha. Unaposhinda kitu fulani kwa ajili ya Ureno, siku zote kinakuwa spesho, hakuna kitu kizuri kama kushinda ukiwa na timu ya taifa kwa maoni yangu. Hiki kizazi kinastahili hii kitu.

“Tulifahamu mambo yangekuwa magumu, lakini tulistahili na hii inatusaidia kupata hali ya kujiamini na kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia tukiwa wenye kujiamini zaidi.”

Ronaldo mkataba wake kwenye klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia utafika ukomo mwishoni mwa msimu huu. Staa huyo mshindi mara tano wa Ballon d’Or awali alionekana kutokuwa na uhakika wa maisha yake kwenye klabu hiyo na kuposti kitu kwenye mtandao wa kijamii, wakati alipoandika: “Ukurasa umefungwa. Stori? Bado inaandikwa. Nawashukuru nyote.”

Lakini, kwa sasa Ronaldo anaonekana kubadili mipango yake na alipoulizwa Jumapili baada ya fainali juu ya hatima yake alisema: “Siwezi kubadili chochote. Al-Nassr, ndio. Unajua umri wangu kwa sasa, naelekea mwisho kuliko kuwa mwanzoni. Lakini, ni lazima nifurahia kila tukio. Kama sitakuwa nimepata majeraha makubwa, nitaendelea kucheza.”

Ronaldo alijiunga na timu hiyo ya Saudia mwaka 2023 na amekuwa kinara wa mabao wa Saudi Pro League kwa misimu miwili iliyopita. Rais wa Fifa, Gianni Infantino alisema Ronaldo angekwenda kucheza kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu Marekani.

Ronaldo mwenyewe alikiri kupokea ofa nyingi za kumtaka kwenda kujiunga na timu itakayocheza michuano hiyo itakayofanyika Marekani mwezi huu. Lakini, kwa kauli yake ya Ijumaa iliyopita amefuta mipango ya kwenda kucheza kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia la Klabu kwa kubaki Al Nassr.

Mkurugenzi wa michezo wa Al-Nassr, Fernando Hierro alisema mwezi uliopita kwamba ana uhakika Ronaldo atasaini dili jipya kwenye klabu hiyo.