Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldinho kurejea uwanjani kesho baada ya miaka 11

Muktasari:

  • Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 46, ambaye aliwahi kuzichezea Barcelona na AC Milan, anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Ravenna tangu alipojiunga na klabu hiyo inayoshiriki Serie C mwezi Agosti mwaka huu.

MILAN, Italia: BAADA ya miaka 11, gwiji wa soka la Brazil, Ronaldinho anatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza cha Ravenna kitakachomenyana na wapinzani wao wa karibu, Forli, katika mchezo wa Ligi Daraja la Tatu nchini Italia utakaochezwa Jumapili.

Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 46, ambaye aliwahi kuzichezea Barcelona na AC Milan, anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Ravenna tangu alipojiunga na klabu hiyo inayoshiriki Serie C mwezi Agosti mwaka huu.

Mchezo wake wa mwisho wa ushindani ulikuwa Septemba 2015, alipokuwa akiitumikia klabu ya Fluminense ya Brazil. Hivyo, kurejea kwake uwanjani kutakuwa baada ya zaidi ya miaka 11.

Kocha wa Ravenna, Andrea Mandorlini, alithibitisha Ijumaa kuwa Ronaldinho ataanza kwenye mchezo huo akiwa miongoni mwa washambuliaji watatu wa kikosi chake.

"Atacheza kuanzia mwanzo, hakuna shaka kuhusu hilo. Baadaye tutaamua kwa pamoja muda atakaocheza," alisema Mandorlini.

"Ni mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi katika zama za soka la kisasa. Hata hivyo, tunahitaji kupata matokeo. Sisi hucheza kwa kutumia washambuliaji watatu na yeye atakuwa mmoja wao."

Ronaldinho, ambaye aliwahi kutwaa tuzo ya Ballon d'Or, alijiunga na Ravenna mwezi Agosti akiwa mwekezaji, lakini pia alieleza nia yake ya kurejea uwanjani ili kufunga bao moja la mwisho na kufikisha mabao 300 katika maisha yake ya soka.

Mmiliki wa klabu hiyo, Ignazio Cipriani, alisema awali kuwa lengo la Ronaldinho lina mvuto wa kipekee, akitaka kufunga bao lake la mwisho kabla ya kuhitimisha safari yake ya soka.

"Lengo lake lina mvuto wa kihisia, anataka kujaribu kufunga bao lake la mwisho. Ushiriki wake si wa maonyesho tu wala mbinu ya kutangaza klabu ili watu wazungumzie kuhusu sisi," alisema Cipriani.

Mbrazil huyo aliwasili nchini Italia Ijumaa na atakuwa na nafasi ya kufanya mazoezi mara moja tu na wachezaji wenzake kabla ya mchezo wa Jumapili.

Kutokana na matarajio makubwa ya mashabiki kutaka kumuona nyota huyo akicheza, uongozi wa Ravenna umejenga jukwaa la muda katika Uwanja wa Stadio Bruno Benelli ili kuongeza nafasi kwa mashabiki watakaohudhuria mchezo huo.

Ronaldinho, ambaye aliwahi kutwaa Kombe la Dunia akiwa na Brazil, anatarajiwa kuvuta mashabiki wengi wanaotaka kumshuhudia akicheza kwa mara nyingine, huenda ikiwa ni moja ya nafasi za mwisho kumuona akifanya alichokizoea uwanjani.

Kwa upande wake, mshambuliaji wa Ravenna, Simone Rabbi amefichua kuwa Ronaldinho ndiye atakayepiga penalti zitakazopatikana kwa timu hiyo katika mchezo huo.

Ravenna inaingia katika mchezo huo ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 13.