Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PATAMU! Real Madrid ilivyoipiga bao jingine Barcelona

MAHASIMU Pict

Muktasari:

  • Real Madrid na Barcelona zinatajwa kuwa miongoni mwa klabu zinazovutia zaidi wachezaji. Licha ya utajiri wa klabu za Ligi Kuu England, zinapata wakati mgumu kuwazuia wachezaji wao bora pale vigogo hao wawili wa Hispania wanapowahitaji.

MADRID, HISPANIA: LIGI Kuu Hispania (LaLiga), ni nyumbani kwa timu mbili kubwa zaidi duniani, Real Madrid na Barcelona, ambazo zinatawala mjadala wa soka nchini humo. Madrid ndiyo timu yenye mafanikio makubwa zaidi ikiwa na mataji 36 ya LaLiga, huku Barcelona ikiwa nayo 29. Atletico Madrid inashika nafasi ya tatu ikiwa na mataji 11.

Real Madrid na Barcelona zinatajwa kuwa miongoni mwa klabu zinazovutia zaidi wachezaji. Licha ya utajiri wa klabu za Ligi Kuu England, zinapata wakati mgumu kuwazuia wachezaji wao bora pale vigogo hao wawili wa Hispania wanapowahitaji.

Hali ya kifedha katika soka imebadilika kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, jambo linaloonekana wazi katika LaLiga kwa sasa.

Mgawanyo wa mapato ya matangazo ya televisheni unaipa Real Madrid na Barcelona sehemu kubwa zaidi, hali inayochangia tofauti kubwa ya kifedha kati yao na klabu nyingine.

MAHA 04

Klabu zilizo nje ya vigogo hao watatu haziwezi kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika ada za usajili, tofauti na matumizi makubwa ya klabu za England.

Klabu za Ligi Kuu England zilitumia Euro 4.1 bilioni katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi lililopita, huku LaLiga zikitumia Euro 756 milioni pekee.

Tofauti hiyo ya kifedha kati ya klabu za LaLiga inaonekana pia unapochambua gharama za usajili wa wachezaji waliounda vikosi vyao, kwa kutumia takwimu zinazotolewa na Transfermarkt.

MAHA 02

GHARAMA USAJILI VIKOSI 20 LALIGA

Ni vikosi vitano pekee vya LaLiga vilivyogharimu zaidi ya Euro 100 milioni kuvijenga, licha ya vikosi 14 kuwa na thamani ya soko inayozidi Euro 100 milioni. Jambo la kuvutia ni kwamba kikosi cha Real Madrid kiligharimu Euro 420 milioni zaidi ya Barcelona katika ada za usajili, hali inayoeleza tofauti ya mifumo ya biashara ya klabu hizo.

Matatizo ya kifedha ya Barcelona katika miaka ya karibuni yamefahamika kwa kiasi kikubwa, jambo lililoifanya klabu hiyo kuweka mkazo mkubwa katika kukuza vipaji kutoka akademi yake maarufu ya La Masia.

Wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza cha Hansi Flick, kwa mujibu wa Transfermarkt, wamelelewa katika akademi hiyo. Miongoni mwao ni Lamine Yamal, ambaye kwa sasa anashika nafasi ya mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi duniani. Wingi wa wachezaji waliolelewa katika akademi ya Barcelona ni sababu kubwa inayochangia gharama ndogo ya usajili wa kikosi hicho.

MAHA 04 (1)

Barcelona inashika nafasi ya 15 duniani kwa gharama za usajili wa kikosi, ikiwa nyuma ya Brighton, licha ya kuwa na kikosi cha tano kwa thamani kubwa zaidi ya soko kwa mujibu wa Transfermarkt. Real Madrid ina kikosi chenye thamani kubwa zaidi duniani, kikikadiriwa kufikia Euro 1.5  bilioni, lakini gharama ya kukisajili ni Euro 910 milioni, inayoiweka katika nafasi ya saba.

Los Blancos wameachana na sera yao maarufu ya kusajili nyota wakubwa kwa gharama kubwa, maarufu kama ‘Galacticos’, na badala yake wameelekeza nguvu katika kusajili wachezaji wenye majina makubwa kwa uhamisho wa bure. Miongoni mwa wachezaji hao ni Ibrahima Konate aliyetokea Liverpool baada ya kumaliza mkataba wake, Kylian Mbappe (PSG) na Trent Alexander-Arnold (Liverpool).

Atletico Madrid inashika nafasi ya tatu, ikiwa na kikosi kilichogharimu Euro 447 milioni kukijenga, ambapo kiasi hicho ni Euro 12 milioni tu chini ya Barcelona, na inawezekana kuipita katika dirisha la usajili la Januari 2027. Jambo jingine la kuvutia ni kwamba kikosi cha Malaga kimegharimu Euro 680,000 pekee, na ndicho pekee katika ligi tano kubwa za Ulaya kilichogharimu chini ya Euro 1 milioni katika ada za usajili.


MAHA 01

YAMAL, MBAPPE

Winga wa Barcelona, Lamine Yamal mwenye umri wa miaka 19, anashika nafasi ya kwanza akiwa na thamani ya Euro 220 milioni sawa na mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, mwenye umri wa miaka 26. Wawili hao ndio wanasoka ghali duniani kwa sasa.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Mbappe, anashika nafasi ya tatu akiwa na thamani ya Euro 200 milioni, huku kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich, Michael Olise, akikamata nafasi ya nne kwa Euro 180 milioni baada ya kupanda kwa Euro 10 milioni katika tathmini ya hivi karibuni, ilhali kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham, anakamilisha tano bora akiwa na thamani ya Euro 160 milioni.