Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid yapambana kumzuia Vinícius kutimkia Arsenal

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwanza na OneFootball na Le Journal du Real, Real Madrid imelazimika kuchukua hatua za haraka kwa kuwasilisha ofa rasmi ya kuongeza mkataba kwa wawakilishi wa mchezaji huyo.

MADRID, HISPANIA: SOKO la usajili Ulaya linaendelea kushika kasi, huku mhusika mkuu saa za karibuni akiwa ni Vinícius Junior, ambapo mshambuliaji huyo nyota wa Real Madrid ameibuka kuwa kitovu cha mvutano kati ya uongozi na Arsenal inayomshawishi kuhamia England.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwanza na OneFootball na Le Journal du Real, Real Madrid imelazimika kuchukua hatua za haraka kwa kuwasilisha ofa rasmi ya kuongeza mkataba kwa wawakilishi wa mchezaji huyo.

Awali, mazungumzo yalikuwa yamesimama kwa miezi kadhaa, lakini sasa yamepata nguvu kutokana na hofu ya klabu hiyo kumpoteza mshambuliaji huyo.

Haraka hiyo ya viongozi wa Real Madrid inatajwa kuchochewa na ofa kubwa ya kifedha ambayo Arsenal inaiandaa, na kwa mujibu wa Sport na   The Telegraph, Washika Mitutu wako tayari kutoa mkataba wenye thamani kubwa ili kumshawishi nyota huyo wa Brazil ahamie Ligi Kuu England.

Taarifa zinaeleza kuwa kikosi hicho kinataka kumpa Vinicius mshahara wa Euro 400,000 kwa wiki, sawa na zaidi ya Euro 20 milioni kwa msimu baada ya makato ya kodi.

Kiasi hicho kitamfanya Mbrazili huyo kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya Arsenal.

Vyanzo vingine akiwemo mwanahabari bingwa wa usajili Florian Plettenberg pamoja na tovuti ya Bolavip, vinaeleza kuwa Arsenal haijaishia kwenye mazungumzo ya mshahara pekee, bali pia inaandaa ofa ya kwanza rasmi ya usajili itakayowasilisha kwa Real Madrid.

Lengo ni kufanya usajili mkubwa wa majira ya kiangazi na kumfanya Vinícius kuwa kiongozi wa mradi wao wa kisoka.

Kutokana na hali hiyo, Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, pamoja na viongozi wa klabu hiyo wameongeza kasi ya mazungumzo ya kumbakisha nyota huyo.

Kambi ya Vinicius imekuwa ikihitaji kuboreshwa kwa kiwango kikubwa mshahara wake, ikitaka afikie takribani Euro 30 milioni kwa mwaka kabla ya makato ya kodi. Kwa ofa mpya iliyowasilishwa, viongozi wa Real Madrid wana matumaini ya kufikia makubaliano ya mwisho siku chache zijazo na kumaliza suala hilo.

Kutoka England pia kuna taarifa zinazodai kuwa iwapo mazungumzo yatafeli, Real Madrid haitakuwa tayari kumuuza kirahisi. Vyombo mbalimbali, ikiwemo Libertad Digital vinaeleza kuwa klabu hiyo inamthaminisha Vinicius kwa ada inayokaribia Euro 160 milioni 160.