Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ratcliffe akataa dili la Robert Lewandowski

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Lewandowski, ambaye alitua Camp Nou 2022 akitokea Bayern Munich, amefunga mabao 65 katika mechi 99 akiwa na Barca. Hata hivyo, Ratcliffe anaamini Man United inapaswa kuwekeza kwa wachezaji vijana badala ya kutumia fedha kwa nyota wenye umri mkubwa.

MMILIKI mwenza wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, ameripotiwa kuzuia mpango wa klabu hiyo kumsajili mshambuliaji mkongwe wa Barcelona na timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski, 37, ambaye anatarajiwa kuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utakuwa unamalizika.

Lewandowski, ambaye alitua Camp Nou 2022 akitokea Bayern Munich, amefunga mabao 65 katika mechi 99 akiwa na Barca. Hata hivyo, Ratcliffe anaamini Man United inapaswa kuwekeza kwa wachezaji vijana badala ya kutumia fedha kwa nyota wenye umri mkubwa.

Vyanzo vya ndani kutoka Old Trafford vinasema Ratcliffe anataka wachezaji ambao watakuwa na umri wa miaka 26 au chini na pia wasizidi miaka 30.

Ratcliffe, ambaye kwa sasa anamiliki asilimia 27 ya hisa za United kupitia kampuni yake ya INEOS, anaamini utaratibu huo utaipa nguvu zaidi timu.


Dominic Solanke

KOCHA wa Tottenham Hotspur, Thomas Frank, anaripotiwa kutovutiwa na uwezo wa mshambuliaji wa timu hiyo, Dominic Solanke, 28, na huenda akamruhusu kuondoka Januari mwakani.

Solanke aliyesajiliwa kutoka Bournemouth kwa dau la Pauni 42 milioni mwaka jana, tangu kuanza kwa msimu huu hajafunga bao hata moja katika mechi tatu za EPL alizocheza. Timu kadhaa za EPL ikiwamo West Ham na Crystal Palace zinatajwa kutaka huduma yake.


Antoine Semenyo

INAELEZWA Bournemouth ilikataa ofa mbili kubwa kutoka Tottenham na Man United zilizohitaji kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Ghana, Antoine Semenyo, 25, katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Semenyo aliyesajiliwa na Bournemouth kutoka Bristol City mwaka 2023, amekuwa katika kiwango bora tangu ajiunge na timu hiyo. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Samu Aghehowa

TOTTENHAM inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa FC Porto na Hispania, Samu Aghehowa, 21, ambaye anaonekana kung’ara tangu ajiunge na timu hiyo. Hata hivyo, dili hilo linaonekana kuwa gumu kwao kwani wanakumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa Arsenal, Newcastle na Nottingham Forest ambazo pia zinahitaji huduma ya mshambuliaji huyu ambaye hadi sasa ameshacheza timu za vijana za taifa za Hispania.



Morgan Rogers

KIUNGO wa Aston Villa, Morgan Rogers mwenye umri wa miaka 23, yuko kwenye hatua za mwisho za mazungumzo ya kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho kwa muda mrefu zaidi.

Rogers, aliyesajiliwa kutoka Middlesbrough Januari 2024, amekuwa mchezaji muhimu kwa kocha Unai Emery, hasa katika mashindano ya kimataifa.

Msimu huu amefunga bao moja na kutoa asisti mbili. Mkataba mpya utamwezesha kusalia Villa Park hadi mwaka 2032.


Daniel Munoz

BARCELONA imewasilisha ofa ya takribani Euro 30 milioni kwenda Crystal Palace kwa ajili ya kumsajili beki wa kulia wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Colombia, Daniel Munoz mwenye umri wa miaka 29.

Munoz, ambaye ameonyesha kiwango cha juu katika EPL msimu huu, anachukuliwa kama suluhisho sahihi la tatizo la beki wa kulia katika kikosi cha Barca.

Palace hawako tayari kumuachia kwa sasa ingawa inaweza kufanya hivyo ikiwa Barcelona itakubali kushusha bei yake.


Malo Gusto

JUVENTUS inafuatilia kwa karibu beki wa kulia wa Chelsea, Malo Gusto, 22, ambaye ameomba kuondoka ili kupata nafasi zaidi ya kucheza.

Gusto, ambaye amekuwa akishindania namba na mastaa kama Reece James, anahusudiwa sana na benchi la ufundi la Juventus ambalo linatamani kumpata hata kwa mkopo wa nusu msimu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa  Ufaransa, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Casemiro

MANCHESTER United inaripotiwa kuwa haina mpango wa kumuongeza mkataba mpya kiungo wao wa kimataifa wa Brazil, Casemiro mwenye umri wa miaka 33, hatua ambayo inaweza kumruhusu kuondoka bure mwishoni mwa msimu huu.

Casemiro alisajiliwa na Man United kutoka Real Madrid mwaka 2022 kwa Pauni 60 milioni na amekuwa katika kiwango bora tangu wakati huo.

Mchezaji huyo wa Brazil analipwa takriban Pauni 350,000 kwa wiki, na Man United inaona haiwezi kuendelea kumpa kiasi hicho, hivyo ili asaini tena atatakiwa kukubali kupunguziwa mshahara wake jambo ambalo hadi sasa bado hajalikubali.