Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jobe Bellingham atua anga za Man United

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa gazeti la Express, Man  United inavutiwa sana na maendeleo ya kinda huyo raia wa England  ambaye ni mdogo wa Jude Bellingham.

MANCHESTER United inafikiria kumsajili kwa mkopo katika dirisha lijalo la usajili kiungo wa Borussia Dortmund, Jobe Bellingham, mwenye umri wa miaka 20.

Kwa mujibu wa gazeti la Express, Man  United inavutiwa sana na maendeleo ya kinda huyo raia wa England  ambaye ni mdogo wa Jude Bellingham.

Jobe aliyejiunga na Dortmund kutoka Sunderland katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2024, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 16 za michuano yote, amefunga bao moja na kutoa asisti tatu.

Maskauti wa Man United wanadaiwa kuwa Ujerumani kwa sasa wakiendelea kumfuatilia kwa karibu na ripoti ya awali inaonyesha wamependekeza asajiliwe kwa mkopo wa nusu msimu ambao utakuwa na kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu ikiwa ataonyesha kiwango bora.

Mkataba wa wa sasa wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2030, baadhi ya timu za England zilikuwa  zikihitaji kumsajili lakini alizipiga chini na kuamua kwenda Dortmund akiamini atapata muda mwingi zaidi wa kucheza.


Joshua Zirkzee

WEST Ham United na Sevilla zinadaiwa kuwa katika vita kali ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya  Uholanzi Joshua Zirkzee, mwenye umri wa miaka 24.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Mirror, Zirkzee ambaye amekuwa akipambana kupata nafasi ya kwanza tangu ajiunge na Man United akitokea Bologna mwaka jana ameomba kuondoka ili kupata timu itakayomchezesha na hatimaye ajumuishwe katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kitakachoshiriki Kombe la Dunia mwakani.


Anthony Gordon

LICHA ya kufanya usajili mkubwa katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, Liverpool inaripotiwa kuwa bado inafikiria kufanya usajili wa washambuliaji wawili katika dirisha lijalo.

Miongoni mwa washambuliaji ni pamoja na Anthony Gordon kutoka Newcastle United na Antoine Semenyo wa Bournemouth.

Liverpool inataka kuongeza kasi na ubunifu katika safu yao ya ushambuliaji na inataka kufanya usajili huo kwa sababu haina uhakika wa kuendelea kuipata huduma ya  Mohamed Salah ambaye huenda akatimkia Saudi Arabia mwisho wa msimu huu.


Ezri Konsa

TOTTENHAM Hotspur na Manchester City zinaripotiwa kuwa zinamfuatilia kwa karibu beki wa Aston Villa na England, Ezri Konsa mwenye umri wa miaka 28.

Licha ya vigogog tajwa hapo juu, ripoti zinadai kuwa klabu kama Chelsea, Liverpool na Manchester United pia zimekuwa zikimfuatilia kwa muda mrefu.

Konsa, ambaye anaweza kucheza kama beki wa kati au kulia, alipewa nafasi katika kikosi cha England kwa mara ya kwanza mwaka 2024 na amekuwa mhimili wa Villa katika safu ya ulinzi.


Hayden Hackney

BRIGHTON, Newcastle United, Fulham, na Brentford zinaripotiwa kuvutiwa na kiungo wa Middlesbrough, Hayden Hackney, mwenye umri wa miaka 23.

Kwa mujibu wa TBR Football, Hackney amekuwa mmoja wa wachezaji wanaoongoza  takwimu za kupora mipira na kupiga pasi sahihi katika Ligi  Daraja la kwanza msimu huu.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu huu amecheza mechi 13 za michuano yote.


Pierre Kalulu

NEWCASTLE United na Tottenham Hotspur zinaripotiwa kuwa zinavutiwa sana na beki wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Pierre Kalulu, mwenye umri wa miaka 25.

Kwa mujibu wa tovuti ya Italia ya TuttoJuve, Kalulu amekuwa akipata dakika chache msimu huu baada ya kurejea kutoka  katika majeraha na Juventus imepanga kumuuza ili kupata pesa itakazotumia katika usajili.

Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Mason Greenwood

BARCELONA imetuma maskauti Ufaransa kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maendeleo ya mshambuliaji wa kimataifa wa Jamaica, Mason Greenwood, mwenye umri wa miaka 24, anayeichezea  Olympique Marseille.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, maskauti hao wamehudhuria michezo kadhaa ya Marseille msimu huu kumuangalia Greenwood, ambaye anaonkana kuimarika siku hadi siku.

Msimu huu Greenwood ni  mmoja wa wachezaji wanaoongoza kwa mabao katika Ligue 1, akifunga nane  katika mechi 12.


Piotr Zielinski

INTER Milan ipo tayari kupokea ofa kwa ajili ya  kiungo wao wa kimataifa wa  Poland, Piotr Zielinski, mwenye umri wa miaka 31, ambaye amekuwa akihusishwa na  Leeds United ya England.

Inaelezwa Inter ipo tayari kumwachia mchezaji huyo Januari mwakani  ili kupunguza gharama za mishahara.

Zielinski, aliyewahi kung’ara akiwa Napoli, ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa katika Serie A na mashindano ya Ulaya, akiwa amecheza zaidi ya michezo 350 katika ligi hiyo.