Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga Princess, JKT Queens vitani kumwani kinda

VITA Pict

Muktasari:

  • Taarifa zinaeleza mmoja wa wachezaji waliopo kwenye orodha ya mabosi wa Yanga Princess ni nahodha wa Alliance Girls, Milembe John, ambaye amekuwa na kiwango bora msimu uliopita.

BAADA ya Yanga Princess kuachana na viungo watatu muhimu, Agnes Pallangyo, Maimuna Khamis 'Mynaco' na Lydia Akoth inaelezwa iko kwenye harakati za kuwania saini ya kiungo kinda, Milembe John wa Alliance Girls.

Taarifa zinaeleza mmoja wa wachezaji waliopo kwenye orodha ya mabosi wa Yanga Princess ni nahodha wa Alliance Girls, Milembe John, ambaye amekuwa na kiwango bora msimu uliopita.

Ingawa JKT Queens inaelezwa ndiyo iliyo mbele zaidi katika mbio za kuipata saini ya nyota huyo baada ya kuwasilisha ofa mapema, Yanga Princess inafuatilia kwa karibu dili hilo.

Milembe amekuwa mmoja wa wachezaji waliovutia zaidi katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja. Anaweza kutumika kama kiungo mshambuliaji, kiungo wa kati, winga na hata kiungo mkabaji, jambo linalomfanya kuwa chaguo linalofaa kwa mfumo wowote.

"Yupo kwenye listi ya wachezaji wanaotakiwa na Yanga kuna mazungumzo yanaendelea ingawa bado hawajafikia makubalioano maalumu hata hivyo JKT nao wameingia kwa hiyo mchezaji anaangalia ofa na sehemu ambayo ataweza kucheza," kilisema chanzo.

Baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi Yanga Princess inafanya maboresho makubwa msimu huu, baada ya kuwatangaza kuachana na wachezaji watatu inaelezwa pia kuna panga lingine linapita.

Miongoni mwa wachezaji wenye nafasi ndogo ya kusalia kikosini hapo ni winga Aregash Kalsa raia wa Ethiopia ambaye inaelezwa amekataa kuongeza mkataba mpya akitaka kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Mwingine ni nahodha, Igwe Uzoamaka ambaye amekuwa na msimu bora tangu alipojiunga na Yanga akitokea Nigeria.

Mbali na Milembe Yanga inahusishwa na kumfuatilia kwa karibu kiungo mshambuliaji wa Fountain Gate Princess, Rehema Mohamed.