Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yataka kitonga kwa Dayot Upamecano

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Upamecano, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akiwindwa na vigogo wengi na Bayern inahitaji takribani Pauni 52 milioni katika dirisha dogo lijalo la Januari ili kumuuza staa huyu licha ya kwamba atakuwa amebakisha miezi tu katika mkataba wake.

CHELSEA imepanga kusubiri hadi mwisho wa msimu huu ili kuokoa hadi Pauni 52  milioni katika kumsajili beki wa kati wa Bayern Munich na timu ya taifa ya  Ufaransa Dayot Upamecano, ambaye mkataba wake utakuwa unamalizika wakati huo.

Upamecano, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akiwindwa na vigogo wengi na Bayern inahitaji takribani Pauni 52 milioni katika dirisha dogo lijalo la Januari ili kumuuza staa huyu licha ya kwamba atakuwa amebakisha miezi tu katika mkataba wake.

Mabosi wa Chelsea wanaona kiasi hicho cha pesa ni kikubwa hivyo wanapanga kusubiri hadi mwisho wa msimu ili kumpata bure.

Hata hivyo, mpango wao huo unaweza ukafeli kwani Bayern inapambana kumsainisha mkataba mpya na endapo itashindwa itamuuza Januari.

Mbali ya Chelsea, staa huyu pia anawindwa sana na Liverpool, Manchester United na Real Madrid ambazo zote zinaonekana kuwa tayari kumnunua ingawa inaweza kuwa kwa kiasi pungufu ya kile ambacho Bayern inakihitaji.


Morten Hjulmand

LICHA ya kiungo wa kati wa Sporting Lisbon, Morten Hjulmand, 26, kuwa na kipengele cha kununuliwa kwa Pauni 70 milioni, Manchester United ina imani kuwa inaweza kumpata kwa ada ya uhamisho ya takribani Pauni 50 milioni tu.

Hjulmand amekuwa na wakati mzuri katika ligi ya Ureno kiasi cha kuvutia vigogo mbalimbali barani Ulaya. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Aleksandar Pavlovic

MANCHESTER United imeungana na Manchester City katika harakati za kumfuatilia kiungo wa Bayern Munich, Aleksandar Pavlovic, mwenye umri wa miaka 21.

Staa huyu wa kimataifa wa Ujerumani ambaye alicheza mechi 24 msimu uliopita na kufunga mabao mawili, amekuwa akiimbwa kama 'Andres Iniesta wa Kijerumani' kutokana na ufundi wake.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Kenan Yildiz

REAL Madrid ipo tayari kulipa Euro 100 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Uturuki, Kenan Yildiz, 20.

Yildiz, ambaye amekuwa akifanya vizuri akiwa na Juventus tangu apandishwe kutoka timu za vijana, msimu huu amefunga mabao matano na kutoa asisti sita katika mechi 14 za michuano yote.

Juventus imeonekana kutohitaji kumuuza kwa sasa, lakini bado hiyo haijakatisha tamaa vigogo mbalimbali wanaohitaji saini yake.


Said El Mala

MANCHESTER City, Chelsea, na Manchester United zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya winga kinda wa FC Koln, Said El Mala, mwenye umri wa miaka 19.

El Mala amekuwa katika kiwango bora msimu huu akifunga mabao matatu na kutoa asiti moja katika mechi nane za michuano yote.

Timu nyingi zimevutiwa na uwezo wake wa kutengeneza mashambulizi kwa kasi kiasi cha kusaidia timu yake kutengeneza mashambulizi kwa urahisi zaidi.


Gabriel Jesus

MSHAMBULIAJI wa Arsenal na timu ya taifa ya Brazil, Gabriel Jesus, mwenye umri wa miaka 28, amethibitisha kuwa hataki kuondoka Arsenal kabla ya mkataba wake kumalizika mnamo Juni 2027.

Fundi huyu anaamini bado anaweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha washika mitutu wa Jiji la London licha ya kuwa na changamoto za majeraha ya mara kwa mara.

Atletico Madrid na Juventus zinadaiwa kuwa zilihitaji sana huduma yake hata kwa mkopo katika dirisha lijalo.


Christantus Uche

CRYSTAL Palace huenda ikamsainisha mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Getafe na timu ya taifa ya Nigeria, Christantus Uche, 22, ambaye anacheza kwa mkopo wa msimu mmoja katika kikosi chao.

Katika makubaliano yao na Getafe kuhusu mchezaji huyo, Palace italazimika kulipa Euro 6 milioni na kumsajili jumla fundi huyo ikiwa atacheza mechi 10 au zaidi za Ligi Kuu England.

Hadi sasa, Uche amecheza mechi mbili za EPL, lakini katika mashindano mengine amecheza mechi tano.


Joel Ordonez

NEWCASTLE United inaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumsajili beki wa kimataifa wa Ecuador, Joel Ordonez kutoka Club Brugge ya Ubelgiji.

Kwa mujibu wa tovuti ya Caught Offside, klabu hizo mbili zinatamani sana kumsajili fundi huyu kwa sababu imevutiwa sana na uwezo wake wa kucheza kama beki wa kulia na beki wa kati.

Staa huyu mwenye umri wa miaka 21, ana takwimu nzuri za kuwa beki aliyepiga pasi nyingi sahihi katika Ligi Kuu Ubelgiji.