Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford, Barcelona mambo yapo hivi

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa fundi huyu unatatajiwa kumalizika mwaka 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao 12.

BARCELONA inapambana kumbakisha mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Marcus Rashford, 28, kwa mkopo msimu ujao badala ya kulipa ada ya Pauni 26 milioni inayohitajika ili kumnunua mazima staa huyo.

Inaelezwa Barcelona bado inathamini sana mchango wa Rashford kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa katika kikosi chao kwa mkopo msimu huu, lakini changamoto kubwa ni hali yao ya kiuchumi.

Hata hivyo, mpango huo wa kuomba kumpata tena kwa mkopo unadaiwa kukataliwa na Man United ambayo inahitaji kiasi cha pesa ili kuzitumia kufanya usajili wa wachezaji inaowahitaji katika dirisha lijalo.

Hadi sasa hakuna mwafaka uliofikiwa ingawa inaonekana itakuwa ni ngumu jambo hilo kutokea na kuna asilimia kubwa Rashford akarudi tena Man United ama akauzwa kwa timu nyingine itakayokuwa tayari kutoa pesa kwa ajili ya kumnunua mazima.

Mkataba wa fundi huyu unatatajiwa kumalizika mwaka 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao 12.


Mateus Fernandes

PARIS Saint-Germain imeanzisha mawasiliano na wawakilishi wa kiungo wa Ureno, Mateus Fernandes, 21, anayekipiga West Ham United.

PSG ipo katika mchakato wa kutafuta wachezaji wenye vipaji zaidi ikiwa ni sehemu ya sera yao mpya iliyoonekana kuwasaidia baada ya ile ya awali ya kusajili wachezaji wenye majina makubwa.

Kiungo huyo amekuwa akitazamwa na maskauti wa PSG tangu mwanzo wa msimu huu na wanaonekana kuridhishwa sana na kiwango chake.

Mazungumzo yamefikia hatua nzuri na kuna uwezekano wakafikia mwafaka kabla ya msimu huu kumalizika.


James Trafford

KIPA wa Manchester City na England, James Trafford, 23, ameibua vita kubwa ya usajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Miongoni mwa klabu zinazohitaji saini ya kipa huyo ni pamoja na Liverpool, Chelsea, Tottenham, Aston Villa na Newcastle United.

Trafford anatazamwa kama mmoja wa makipa vijana bora wa kizazi kipya, akiwa na uwezo mkubwa wa kucheza na mpira mguuni.

Kutokana na ushindani huo mkubwa, Manchester City inaweza kuhitaji takribani Pauni 70 milioni ili kumuuza.


Alisson Becker

JUVENTUS  imemweka kipa wa Liverpool na timu ya taifa ya Brazil, Alisson Becker, 33, katika orodha yao ya mastaa inaotaka kuwasajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Alisson ambaye bado ni kipa namba moja wa Liverpool anaonekana kuwa huenda akafuata mstari wa Andy Robertson na Mohamed Salah ambao wanaondoka mwisho wa msimu.

Mabosi wa Juventus wamekuwa katika harakati za kusuka upya kikosi chao baada ya kuwa katika vipindi vya mpito kwa takribani misimu mitatu sasa.


Alex Scott

INAELEZWA Manchester United inaendelea kumfuatilia kiungo wa Bournemouth na England, Alex Scott, 22, na inahitaji kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Scott amekuwa akionyesha maendeleo mazuri katika Ligi Kuu England na inadaiwa amefikiria kuondoka katika kikosi cha Bournmouth baada ya kuona Kocha Andoni Iraola anaweza akaondoka mwisho wa msimu.

Kwa sasa mkataba wa Scott unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 36 za michuano yote.


Richard Rios

MANCHESTER United inaendelea kumfuatilia kiungo wa Benfica na Colombia, Richard Ríos, 25, ili akawe mbadala wa Casemiro anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo, Benfica huenda wakawa wagumu kumwachia fundi huyo kirahisi kutokana na umuhimu wake kwenye kikosi chao na ripoti zinaeleza ili kukamilisha dili hilo inaweza kuhitajika takribani Pauni 70 milioni kama ada ya uhamisho.

Rios ambaye msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Malik Tillman

BOURNEMOUTH imeingia kwenye mbio za kumsajili kiungo wa kimataifa wa Marekani, Malik Tillman, 23, anayekipiga katika kikosi cha Bayer 04 Leverkusen.

Tillman amekuwa akivutia kutokana na uwezo wake wa kucheza kama kiungo mshambuliaji na maeneo ya pembeni. Hata hivyo, dili hilo linaoekana kuwa gumu kwa Bournemouth kwani timu nyingine Ulaya pia zimeonyesha nia ya kumsajili fundi huyu ambaye msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote.


Arda Guler

ARSENAL inaendelea kumfuatilia kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uturuki, Arda Guler, 21, ili kumsajili katika dirisha lijalo. Hata hivyo, ripoti zinaeleza Guler hana mpango wa kuondoka kwa sasa kwa sababu anapata nafasi kubwa kikosi cha kwanza na anaonekana kuwa katika ubora wake.

Arsenal inamwona fundi huyu kama nyongeza muhimu ya ubunifu katika safu yao ya kiungo. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.