Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mainoo mambo safi! kusaini dili jipya Manchester United

Muktasari:

  • Mkataba wa sasa wa Mainoo unatarajiwa kumalizika 2027, na awali alionekana kuwa na uwezekano wa kuondoka baada ya kutopewa nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man United chini ya Ruben Amorim.

KIUNGO wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka, 21, ameripotiwa kufikia makubaliano ya maneno ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho cha Mashetani Wekundu.

Mkataba wa sasa wa Mainoo unatarajiwa kumalizika 2027, na awali alionekana kuwa na uwezekano wa kuondoka baada ya kutopewa nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man United chini ya Ruben Amorim.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 25 za michuano yote na kutoa asisti mbili ambapo kwa kiasi kikubwa amecheza baada ya Michael Carrick kupewa mikoba ya ukocha.

Katika mkataba huo mpya, Mainoo atakunja mshahara unaofikia Pauni 150,000 kwa wiki ikiwa ni takribani mara tatu ya ule wa sasa. Klabu kadhaa ikiwemo Chelsea na Juventius zilionyesha nia ya kumsajili wakati ambao hapati nafasi kubwa ya kucheza.


Randal Kolo Muani

LIVERPOOL inamwangalia mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Randal Kolo Muani, 27, kama mmoja wa wachezaji inaotaka kuwasajili  dirisha lijalo la kiangazi ili achukue nafasi ya Mohamed Salah anayeondoka mwisho wa msimu huu. Kolo Muani, anayecheza kwa mkopo Tottenham akitokea PSG mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028. Katika harakati hizo, Liverpool inakutana na ushindani kutoka Juventus ambayo pia inahitaji yake.


Bernardo Silva

KIUNGO wa Manchester City na timu ya taifa ya Ureno, Bernardo Silva, 31, anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu ameingia katika rada za Arsenal na Barcelona zikitajwa kutamani  kumsajili hasa baada ya kugundua  atapatikana bure. Silva ni mmoja wa viungo wenye ubora Ulaya na uzoefu, jambo lililomfanya kuwa chaguo la klabu nyingi. Arsenal kupitia Mikel Arteta ambaye amewahi kufanya kazi na Silva inadaiwa kuanza kupambana kumsajili.


Elliot Anderson

MANCHESTER United inaangalia mchezaji atakayekuwa chaguo mbadala la kiungo Casemiro anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu na hadi sasa ina majina mawili. Moja ni kiungo wa Nottingham Forest na England, Elliot Anderson, 23, na yule wa Real Madrid na Ufaransa, Aurelien Tchouameni, 26, ambaye anatajwa kuwa huenda akauzwa mwisho wa msimu. Hadi sasa haijajulikana yupi atatua.


James Trafford

BRIGHTON inaangalia uwezekano wa kumsajili kipa wa Manchester City na timu ya taifa ya England, James Trafford, 23, katika dirisha la majira ya kiangazi. Trafford anatafuta timu itakayompa nafasi zaidi ya kucheza mara kwa mara, jambo ambalo limekuwa changamoto Man City kutokana na ushindani mkubwa langoni. Brighton imemhakikishia kuwa atakuwa kipa  namba moja ikiwa atakubali kujiunga nayo, jambo ambalo limemvutia.


Alex Scott

CHELSEA na Manchester United ni miongoni mwa timu zinazomfuatilia kwa karibu kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, 22. Scott ameendelea kuonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu England akivutia kwa ubunifu na uwezo wa kumiliki dimba. Chelsea na Man United zinatafuta viungo wenye umri mdogo kwa ajili ya kusuka upya maeneo hayo. Hata hivyo, Bournemouth haionekani kuwa tayari kumwachia mchezaji huyo kirahisi.


Eduardo Conceicao

BARCELONA inaongoza mbio za kuwania saini ya mshambuliaji chipukizi wa Brazil, Eduardo Conceicao, 16, anayekipiga Palmeiras. Hata hivyo, Barca inakabiliwa na ushindani kutoka Man City, Man United na Newcastle United. Kutokana na kanuni za usajili wa wachezaji wa kimataifa wenye umri mdogo, Conceicao hatahamia Ulaya hadi atakapofikisha miaka 18 hata kama atasajiliwa.


Teun Koopmeiners

MANCHESTER United na Galatasaray zinajiandaa kupambana kuwania saini ya kiungo wa Uholanzi, Teun Koopmeiners, 28, anayekipiga Juventus. Koopmeiners ana uwezo wa kucheza namba sita na nane, na klabu yake inahitaji zaidi ya Pauni 40 milioni ili kumuuza. Kiasi hicho cha pesa kinaonekana kuwa kikubwa kwa timu zinazomhitaji, hivyo zinafanya mazungumzo na wawakilishi wa Juventus ili kupunguziwa.