Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford achora tattoo mpya Man United

Muktasari:

  • Winga huyo, ambaye kwa misimu miwili iliyopita alicheza kwa mkopo Aston Villa na Barcelona mtawalia, huku akiwa hajaanza katika kikosi cha kwanza cha Manchester United kwa siku 626 hadi wiki iliyopita, hakuhama katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi lililofungwa wiki hii.

MANCHESTER, ENGLAND; MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Marcus Rashford ameonyesha tattoo mpya yenye nembo ya Manchester United baada ya kujihakikishia kwamba ataendelea kubaki katika klabu hiyo msimu huu.

Winga huyo, ambaye kwa misimu miwili iliyopita alicheza kwa mkopo Aston Villa na Barcelona mtawalia, huku akiwa hajaanza katika kikosi cha kwanza cha Manchester United kwa siku 626 hadi wiki iliyopita, hakuhama katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi lililofungwa wiki hii.

Kabla ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha kocha Michael Carrick kilichoichapa Ipswich Town 5-2 Jumapili iliyopita, ilitangazwa kuwa nyota huyo angevaa jezi namba 9, na sasa hilo limeonekana pia katika tattoo yake mpya.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliwapa mashabiki nafasi ya kuiona tattoo yake tumboni, ambayo ina namba tano za jezi alizowahi kuvaa katika maisha yake ya soka. Namba 10, 19 na 39, ambazo aliwahi kuzivaa Manchester United zilikuwa tayari tumboni kwake, huku 14 aliyovaa Barcelona msimu uliopita nayo ikiwa imeongezwa.

Rashford pia aliwahi kuvaa jezi namba 9 alipokuwa Aston Villa, hivyo tattoo hiyo mpya imemsaidia kuweka kumbukumbu ya namba hizo mbili kwa wakati mmoja. Namba hizo za jezi zimechorwa chini ya maneno, “kile macho yako yanachoona kinaweza kukupotosha, usihukumu kitabu kwa jalada lake.”

Baada ya kuiweka picha yenye michoro hiyo kwenye akaunti zake za mitandaoni, Rashford aliandika kwenye maelezo yake: “Namba mpya, dhamira ileile…” Pia amechorwa tattoo mpya shingoni yenye maneno: “Penda na acha mambo yaende.”

Tattoo hizo zilichorwa na mchoraji maarufu wa tattoo huko England, Dale McGovern, ambaye pia amewahi kufanya kazi na watu mashuhuri akiwemo mshawishi wa mitandao ya kijamii Molly Smith, beki wa Leeds Jayden Bogle na pia mchezaji mwenzake Rashford, Ayden Heaven.

Rashford sasa atakuwa na matumaini ya kutulia Man United baada ya awali kuonekana kana kwamba hakukuwa na nafasi ya kurejea klabuni hapo. Baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa kwanza wa msimu dhidi ya Hull, Rashford alianza dhidi ya Ipswich na sasa anaonekana kuwa chaguo muhimu la Michael Carrick katika nafasi ya winga.

Kwa upande mwingine, beki Harry Maguire anaamini Rashford akiwa “na furaha, mwenye ari na mwenye njaa ya mafanikio” anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Manchester United msimu huu. Barcelona ilikataa kutumia fursa ya kumsajili moja kwa moja baada ya kipindi chake cha mkopo kumalizika msimu huu, hivyo akarudi Manchester huku kukiwa na maswali mengi kuhusu kama angeweza kurejeshwa katika kikosi.

Katika mchezo dhidi ya Ipswich, alianza katika kikosi cha Manchester United kwa mara ya kwanza baada ya siku 626, tangu mwaka 2024.