Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pistons wanavyojenga makali ya Cunningham bila mpira

Muktasari:

  • Cade Cunningham na Ausar Thompson, mastaa wawili wa Pistons walikuwa wakiboresha zaidi uelewano wao walioujenga katika misimu yao mitatu pamoja na papo hapo mkongwe mpya Taurean Prince aliungana nao katika michezo ya ‘pickup’ dhidi ya mchezaji mpya wa Memphis Grizzlies, Cam Boozer, pacha wa Thompson, Amen, mlinzi wa Miami Heat Davion Mitchell na wengine.

MIAMI, MAREKANI, NDANI ya ukumbi wa mazoezi wa Chuo Kikuu cha Miami marekebisho yamekuwa yakifanyiwa kazi ambayo yanaweza kuibadilisha Detroit Pistons kuwa timu inayowania ubingwa wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) msimu ujao.

Cade Cunningham na Ausar Thompson, mastaa wawili wa Pistons walikuwa wakiboresha zaidi uelewano wao walioujenga katika misimu yao mitatu pamoja na papo hapo mkongwe mpya Taurean Prince aliungana nao katika michezo ya ‘pickup’ dhidi ya mchezaji mpya wa Memphis Grizzlies, Cam Boozer, pacha wa Thompson, Amen, mlinzi wa Miami Heat Davion Mitchell na wengine.

Cunningham na Thompson walipokezana kuwashambulia walinzi na kuboresha uwezo wao wa kushambulia, ambapo kila mmoja atakuwa na nafasi muhimu katika mafanikio yoyote ambayo Detroit inataka kuyajenga msimu ujao, lakini kwa namna tofauti.

Tukianza na Cunningham, kutumiwa zaidi katika nafasi za kucheza bila mpira kunaweza kunufaisha uwezo wake wa kushambulia binafsi pamoja na Pistons kwa ujumla. Pamoja na thamani kubwa ya Cunningham anapokuwa na mpira mikononi, kuna sehemu moja ya mchezo wake ambayo kwa ulazima haijatumika sana; uwezo wake wa kufunga akiwa tishio bila mpira.

Cunningham alikuwa na asilimia 48.8 ya mitupo ya pointi tatu kwenye majaribio 41 ya ‘catch-and-shoot’ katika hatua ya mchujo msimu uliopita, huku akiwa na asilimia 75 ya mitupo ya umbali huo baada ya kudribo mara moja na asilimia 50 baada ya kudribo mara mbili.

Idadi ya ukimbiaji na mpira wake ni ndogo zaidi na sasa akijaribu mitupo minane mpaka 10 mtawalia ili kutafuta ubora. Lakini kiwango chake katika mechi za mchujo zilizopita pamoja na uwezo wa kimwili vinaongezeka katika hatua hiyo ya maandalizi ya msimu na inaweza kuwa sababu ya kujaribu mara kwa mara mipango ya kumwezesha kufunga bila kuwa mchezaji anayeanzisha shambulizi.

Kwa sasa ameonyesha utayari wa kuwaacha wengine waanzishe mashambulizi, iwe Thompson au Daniss Jenkins. Isaiah Joe (ana asilimia 42.3), John Collins (40.6), Prince (43.6) na hata Gary Harris (41.2) wote waliosajiliwa katika kipindi hiki cha mapumziko ya msimu katika maandalizi haya ya msimu wamekuwa angalau na asilimia 40 kutoka nje ya mstari wa pointi tatu ikiwa ni maboresho mazuri zaidi  wakijifua kuusaka ubingwa msimu ujao.

Kikosi cha Pistons msimu huu kinaweza kuwa chenye uwezo mkubwa zaidi wa kutupia pointi tatu kuwahi kujengwa kumzunguka Cunningham.

Ingawa ni kazi kubwa kufikia kiwango cha ufungaji wa mitupo ya aina hiyo, lakini haliwezi kuwa jambo lisilowezekana kwa Pistons.

Na hii ni hasa ikiwa kocha ohn-Blair Bickerstaff iwapo anaweza kuwa mbunifu vya kutosha katika mipango yake ili kuchanganya vizuri nafasi za Cunningham akiwa na mpira na bila mpira, huku akibaki kuwa mshambuliaji tegemeo. Cunningham ni mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa zaidi katika ligi hiyo anapokuwa na mpira muda mwingi, na hawapaswi kumuondolea fursa nyingi za kuweza kuwaangamiza wapinzani.

Lakini, faida ya mara kwa mara kumruhusu Cunningham kutoka kwenye pindown (kizuizi cha kumtoa mchezaji kwenye nafasi yake), badala ya kutegemea sana mfumo wa pick-and-roll (mchezaji wa pili anaweka kizuizi kwa mlinzi anayemzuia mchezaji mwenye mpira), inaweza kuwa na athari nzuri kwa timu nzima.

Na hii siyo tu kwamba Cunningham anaweza kuhifadhi nguvu kwa dakika za mwisho za mchezo, lakini anaweza kutumia mvuto wake kuwavuta walinzi na kutengeneza nafasi za wazi kwa mastaa wenzake waliotajwa hapo juu, huku pia akimweka mchezaji kama Thompson katika nafasi bora zaidi ya kufanya mashambulizi.

“Wakati mwingine timu zinaamua kumfuata Cade uwanja mzima, na kwa sababu ya mvuto alionao baadhi ya wachezaji humkomalia sana,” anasema Bickerstaff na kuongeza:

“Unaweza kutumia faida inayopatikana kupitia yeye, lakini sasa (ikiwa siyo yeye anayeanzisha shambulizi) mlinzi wake atalazimika kupita kwenye fasta au kufuatia mabadiliko ya mwelekeo. Hiyo inamfanya kuwa mchezaji bora zaidi wakati watu hawawezi kumzuia kwa mikono, kumvuta au kumzuia kabisa.”

Katika mazoezi yanayoendelea Thompson alionyesha dalili za kuwa mchezaji mzuri wa kuanzisha mashambulizi kutokea pembeni katika vipindi fulani msimu uliopita, ambapo asilimia yake bora ya pasi za kutengeneza nafasi katika taaluma yake, 15.5, iliwekwa katika asilimia 73 ya juu miongoni mwa wachezaji wa pembeni.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ana uwezo wa kimwili wa kufanya hivyo, kuanzia urefu wa mikono yake hadi kasi na misuli yenye nguvu ambavyo vinapaswa kumfanya kuwa mgumu kuzuiwa.

“Tunataka kuweka mpira mikononi mwa Thompson zaidi. Na kisha kumtoa Cade kwenye mchezo wa bila mpira kunaleta mwelekeo mwingine katika mashambulizi yetu. Tunapoendelea kujenga msingi wa mashambulizi na mifumo yetu katika pande zote mbili za uwanja, daima tutatafuta kuongeza vitu tofauti vinavyoweza kutufanya kuwa bora zaidi,”  anasema kocha huyo.

Mienendo ya mchezo wa bila mpira ambayo Cunningham alifanya vizuri zaidi katika mchujo ilikuwa mitupo ya kawaida akiwa amesimama kwenye nafasi na mitupo bila kutembea na mpira umbali mrefu baada ya kupokea mpira kupitia wenzake.