Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Parrott aitingisha tena Spurs

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Parrott alikuzwa katika vikosi vya vijana vya Spurs, kabla ya kuuzwa AZ Alkmaar ya Uholanzi ambako alikiwasha vilivyo kisha akaondoka na kutimkia Real Betis wakati wa dirisha kubwa la usajili la msimu huu.

REAL Betis haina hofu kuhusu uwezekano wa kumpoteza mshambuliaji Troy Parrott kwa waajiri wake wa zamani, Tottenham Hotspur, ambao watalazimika kulipa mkwanja kulingana na kifungu cha kuvunja mkataba chenye thamani ya Dola 112.5 milioni ili kukamilisha uhamisho huo.

Parrott alikuzwa katika vikosi vya vijana vya Spurs, kabla ya kuuzwa AZ Alkmaar ya Uholanzi ambako alikiwasha vilivyo kisha akaondoka na kutimkia Real Betis wakati wa dirisha kubwa la usajili la msimu huu.

Hata hivyo akiwa Betis kiwango chake kimeendelea kuongezeka na kuzifanya timu nyingi kuanza kuvutiwa naye ili kumsajili huku klabu kubwa za Hispania, Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid kila moja ikimfuatilia kwa karibu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Spurs, mabosi wamekuwa wakikuna vichwa kumshawishi nyota huyo arudi kikosini kwao licha ya kwamba wakati anaondoka kulikuwa hakuna maelewano mazuri kutokana na namna ambavyo makocha mbalimbali walishindwa kumtumia, suala ambalo ameendelea kulilalamikia. Kinachosubiriwa kwa sasa ni kuona iwapo atashawishi tena kurudi mahali alipoanzia kujenga jina lake katika ulimwengu wa soka.


Alex Scott

BOURNEMOUTH wanadaiwa kuwa hawana mpango wa kumpoteza kiungo Alex Scott katika dirisha la usajili la Januari, licha ya kuvutiwa kwake na Chelsea pamoja na Liverpool. Hata hivyo, klabu hiyo inamwangalia kiungo wa Wolverhampton Wanderers, Fer Lepez, kama mbadala iwapo itashindwa kumzuia kuondoka.



Virgil van Dijk

BEKI wa kimataifa wa Uholanzi, Virgil van Dijk anaweza kusaini mkataba mpya kubakia Liverpool, baada ya kumshawishi kocha Andoni Iraola kuhusu uwezo wake wa kuendelea kuwa na manufaa katika timu hiyo zaidi ya msimu huu. Awali, Iraola alitaka kuachana na nahodha huyo Januari, mwakani.



Scott McTominay

SCOTT McTominay, kiungo wa Napoli, anatarajiwa kuondoka na kurejea Ligi Kuu England msimu ujao wa kiangazi, huku mazungumzo ya mkataba mpya Napoli yamesimama kwa sasa. Manchester United walijaribu kumsajili tena mchezaji huyo aliyekulia katika akademi yao wakati wa kiangazi, huku Aston Villa pia ikifanya juhudi za kumsajili.



Vangelis Pavlidis

LICHA ya kudaiwa kubaniwa na klabu yake mshambuliaji wa Benfica, Vangelis Pavlidis, anayewaniwa na Aston Villa na Tottenham Hotspur bado ana ndoto ya kuhamia katika timu inayocheza Ligi Kuu England ama Januari mwakani au wakati wa usajili wa dirisha kubwa lijalo.



Luka Vuskovic

MANCHESTER United, Liverpool na Real Madrid zote zinadaiwa kupambana chini kwa chini kutaka kumsajili beki wa kati Luka Vuskovic kutoka Brighton ifikapo Januari mwakani. Hata hivyo, inaelezwa kwamba timu yake haitaki kumuachia wakati wa dirisha dogo isipokuwa lile kubwa linalofuata.



Breno Bidon

KIUNGO Mbrazili Breno Bidon anayekipiga katika timu ya wa Corinthians anawindwa na Arsenal ambayo iko tayari kulipa kiasi kisichopungua a Dola 28 milioni kilichowekwa kwenye mkataba wake ili kuuvunja. Bidon, 21, ni miongoni mwa vipaji vinavyochipua kwa kasi Brazil kwa sasa.



Giorgi Mamardashvil

LIVERPOOL wako tayari kusikiliza ofa kutoka klabu zinazotaka kumsajili kipa Giorgi Mamardashvili na hawaamini tena kuwa ana uwezo wa kuwa mrithi wa muda mrefu wa Alisson Bercker. Mamardashvili alisajiliwa kutoka Valencia mwaka jana, lakini anaonekana kushindwa kumpa changamoto mkongwe, Becker.



Joao Felix

BARCELONA inadaiwa kuvutiwa na uwezekano wa kuungana tena na mshambuliaji wa Al Nassr, Joao Felix ifikapo Januari, mwakani, lakini wanatambua kuwa ujio wake huenda ukasababisha kuondoka kwa kiungo mshambuliaji Dani Olmo ambaye anaweza kuhamia Bayern Munich ambako amekuwa akipigiwa hesabu za kutakiwa.



Endrick

LICHA ya Arsenal na Tottenham Hotspur kuvutiwa na huduma ya mshambuliaji wa Real Madrid, Endrick, inadaiwa kwamba Real Madrid hawapo tayari kumuuza katika dirisha la usajili la Januari, lakini wako tayari kumruhusu kuondoka kwa mkopo wa miezi sita, kisha arejee kikosini kwao.